Sunday, January 5, 2014

Jose Chameleone na mdogo wake Weasel wamaliza tofauti zao.



Kwa muda mrefu Chameleone na mdogo wake Weasel walikuwa hawaelewani wala kuzungumza. Habari njema ni kuwa mwaka mpya 2014 umekuja na baraka zake ambapo mafahari hao waliamua kuweka tofauti zao pembeni kwenye show ya ‘UG Dance Mix End of Year Party’ iliyofanyika kwenye hoteli ya Sheraton jijini Kampala.


Unaikumbuka beat ya wimbo wa Profesa Jay ‘Nikusaidiaje’ aliomshirikisha Ferooz? Ni beat kali iliyopigwa na Godfather wa Bongo Flava, P-Funk Majani aka Kinywele Kimoja. Beat hiyo ilitumiwa tena miaka saba ijayo na ndugu wa Uganda, Jose Chameleone na Weasel katika wimbo wao uliohit, Bomboklat.

Baada ya kundi la Goodlfye linaloundwa na Radio na Weasel kutumbuiza,  Chameleone alipanda jukwaani akiwa amevalia nguo nyeupe. Aliimba huku fataki zikipigwa hewani kuukaribisha mwaka 2014.
 
 Kisha alisimama na kuwaambia mashabiki amewaandalia surprise ya mwaka.
Chameleone na Weasel wakatumbuiza kwa pamoja wimbo wao, Bomboklat na kuufanya umati uliokuwa ukishuhudia ukulipuka kwa shangwe.

Baadaye Chameleone alimuita Radio na watatu hao wakaahidi kuyaacha yaliyopita ili wagange yajayo.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top