Tuesday, January 7, 2014

Sikiliza alichokisema Mwenyekiti wa Chadema Temeke aliyetekwa na kupigwa vibaya usiku wa kuamkia leo.


Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.

Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja..

Ttulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’




sikiliza audio yake hapa

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top