Tuesday, January 7, 2014

picha na matukio ya nje ya mahakama ambapo Zitto Kabwe ameshida dai lake la CHADEMA kutomjadili uanachama wake.

Wafuasi  na  wapenzi  wa  CHADEMA leo walielekeza macho ya nn kitajili katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa   alikuwa  akitoa  hukumu  dhidi  ya  Zitto Kabwe  na CHADEMA....


Zitto ambaye alikuwa   ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho  iliyokutana  tarehe  3  na  4  mwezi  huu  kujadili  hatima  ya  uanachama wake  wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake...

Akisoma  hukumu  ya  kesi  hiyo  baada  ya  kuiahirisha  jana, Jaji  wa mahakama  hiyo,Jaji Utamwa  ameridhia  pingamizi  lililotolewa  na  mh. Zitto Kabwe la  kutojadili  uanachama  wake na  kuitaka  kamati  kuu  ya  CHADEMA  au  chombo  kingine  chochote  kisijadili  uanachama  wake   hadi  kesi  yake  ya  msingi ( rufaa )  itakaposikilizwa  na  baraza  kuu  la  chama  hicho.

Polisi wakihakikisha wafuasi wa Zitto na wale wasiomuunga mkono hawaleti mtafaruku baada ya huku,u kusomwa.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Hii ni message aliyoiandika zitto baada ya kesi katika twitter

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top