Saturday, January 4, 2014

Mapokezi ya mwili wa aliyekuwa waziri wa fedha Dk.William Mgimwa yalivyokuwa,na Ratiba ya Mazishi.

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa umewasili nchi hii leo kwa ndege ya shirika la Kenya (KQ) na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue pamoja na Mawaziri mbalimbali na Wabunge.



Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini.




Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.




Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto)akisalimiana na baadhi wa Watu waliofika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Leo Jijini Dar es Salaam.

TAREHE 4/ 01/ 2013

    MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIA KUWASILI UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE TERMINAL II, SAA7: 00 MCHANA. BAADA YA KUWASILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWA MAREHEMU MIKOCHENI B.
    SAA 11:00 JIONI MWILI UTAPELEKWA HOSPITALI YA LUGALO.

TAREHE 5/ 01/ 2013

    SAA 3:00 HADI SAA 4:00 ASUBUHI:- CHAKULA NYUMBANI KWA MAREHEMU.
    SAA 4:30 ASUBUHI :- MWILI KUWASILI NYUMBANI MIKOCHENI B.
    SAA 5:30 HADI SAA 8:00 MWILI UTAPELEKWA UKUMBI WA KARIMJEE KWA AJILI YA SHUGHULI ZA IBADA NA HESHIMA ZA MWISHO.
    SAA 8:10 MWILI UTAPELEKWA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE TERMINAL I.
    SAA 10:00 MWILI UNATARAJIA KUWASILI IRINGA UWANJA WA NDULI  NA KUAGWA KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO-IRINGA
    SAA 11:30 JIONI MWILI UTASAFIRISHWA KUELEKEA KIJIJI  CHA MAGUNGA.

TAREHE 6/ 01/ 2013 



    SAA 6:00 MCHANA SHUGHULI ZA MAZISHI KIJIJINI KWA MAREHEMU MAGUNGA. 

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI;

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top