Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa waziri wa fedha amefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikolazwa kwa maradhi yaliyomsumbua mda mrefu.
Mgimwa aliyezaliwa January 20, 1950 alikuwa amelazwa katika hospitali ya Milpark ambayo pia Dk. Sengondo Mvungi. alilazwa kwani hospitali hiyo inaumaarufu wa kusaidia kuwatibu watanzania.
Dk. Mgimwa alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Benki mkoani Mwanza, kabla ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Tutazidi kukujulisha kila matukio yanayoendelea.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment