Katika hali hiyo ndipo kijana mmoja wa kundi lisilomuunga Zito akajikuta akipewa za fasta na njemba moja lenye halijali polisi kwani walikuwa karibu kabisa na eneo la mabishano.
Hatua hiyo ilisababisha Askari wa Jeshi la Polisi kuingilia kati, huku wakiungana na upande wa Chadema na kuwatwanga marungu wafuasi wa Zitto waliokuwa na mabango kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.
Kesi hiyo ilifunguliwa jana na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku wakili wa Chadema Tundu Lissu akiweka pingamizi,hata hivyo Jaji John Utumwa wa Mahakama hiyo alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.
Kesi imehairishwa hadi Jumatatu saa 4:00 asubuhi.
Jaji John Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.Hata hiyo baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na kundi linalo muunga Zitto Kabwe.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment