Wanakwaya kadhaa wa kanisa katoliki la Mt Kalory maeneo ya USA River mkoani arusha wamelipukiwa na kitu kinachozaniwa kuwa ni bomu na wamelazwa katika hospitali ya Misheni ya Tengeru.
Sita kati yao ni majeruhi na mmoja hali yake ni mbaya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
amezungumza na na waandishi wa habari, akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kuahidi kulifuatilia kufaham chanzo cha tukio hilo.

"Taarifa
nimezipata lakini uchunguzi unaendelea kujua chanzo na muhusika
sambamba na ukweli wa mlipuko huo ili kujua kama kweli ni bom na ni la
aina gani".
Wakizungumza
na mtandao huu, kwa nyakati tofauti katika hospitali ya Tengeru iliyopo
wilayani Arumeru, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo walisema kuwa siku
ya mkesha wa kuupokea mwaka 2014 walipokuwa wakitoka kanisani (Kanisa
katoliki parokia ya USA river) waliweza kusikia mlio mkubwa wa kitu kama
bom la kurusha ndipo baadhi yao walioangukiwa na bom hilo kuweza
kujeruhiwa vibaya na kuanguka chini huku wakivuja dam nyingi sehem
mbalimbali za mwili.
Kwa
upande wake Askofu mkuu wa kanisa la katoliki jimbo kuu la Arusha,
Josephat Lobulu akizungumzia tukio hilo alisema kuwa ni tukio la
kulaaniwa, hivyo ameliomba jeshi la polisi kushughulikia jambo hilo.
Alisema
kuwa amesikitishwa na tukio hilo, lakini yeye kama mtumishi wa Mungu
anapaswa kuwaombea wote walioathrika na tukio hil ikizingatiwa wamepatwa
na tukio hilo mita chache tu kutoka katika nyumba ya Mungu (Kanisani).
Tutazidi kukujuza repoti kutoka polisi ikitolewa.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment