Thursday, January 9, 2014

Yule mdada aliyeshikwa na madawa ya kulevya juzi alidanganya kameza 61 wakati sasa katoa 72 kwa haja kubwa na anazidi kuzifurumusha.


Mwanamke aliyekamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, anaendelea kutoa pipi za heroin kupitia njia ya haja kubwa ikiwa ni zaidi ya idadi aliyoisema mwanzoni kazimeza. Pia mdada huyo amekataa kuwataja watu waliomtuma licha ya kubanwa.

Kamishna wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa Yude dada aliyedakwa juzi“Anaendelea kutoa kete zaidi na ndiyo maana hatukuweza kusema idadi kamili ya mzigo alioumeza kwa sababu wakati mwingine wanadanganya, hawasemi ukweli kuhusu kiasi cha mzigo walioumeza, wana mbinu nyingi hawa,” alisema Godfrey.

Alisema baada ya kushikwa mtuhumiwa aliwaambia polisi kuwa amemeza pipi 61, lakini baadaye alisema amemeza pipi 40.

Hadi kufikia jana mchana alikuwa ametoa pipi 72.Mtuhumiwa huyo, alikamatwa juzi akiwa mbioni kwenda China, kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

“Hatuwapi kitu chochote cha kuwafanya wazitoe, lakini anapoendelea kukaa, akila chakula basi na zenyewe kupitia mfumo wa mwili hutoka. Ndiyo maana huyu mwanamke mpaka sasa anaendelea kuzitoa taratibu, mpaka zitakapoisha,”

Nzowa alisema endapo itatokea pipi hizo hazikufungwa vyema zinaweza kupasukia tumboni na aliyemeza kupoteza maisha na kwamba kwa mtuhumiwa jinsi anavyozitoa taratibu upo uwezekano wa kupasuka.

“Ikitokea zikapasuka tumboni mwake hatuna la kufanya kwa sababu jambo hilo lipo kama ambavyo unawasikia vijana wengi wanapoteza maisha kwa njia hiyo,” alisemma

Chanzo cha habari hii:Mwananchi.


Ushauri wa Bure pia umetolewa na waziri wa Uchukuzi kwa Vijana ambao hajaoa kuwa makini na wadada watanashati kwani ukiwaona usoni huwezi amini kuwa wanashugulika na biashara ya pipi na hivi siku za karibuni biashara hiyo imeonekata wadada wengi ndio huifanya ukilinganisha na idadi ya wakaka.
Heroin ni noma jamani achana na hiyo kitu kabisa tafuta biashara nyingine hiyo ni sawa na biashara ya mauaji kwani wengi wamepoteza maisha kwa kutumia madawa ya kulevya.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top