Friday, September 5, 2014

DOKII AMZAWADIA KIWANJA LUCY KOMBA.

 Msanii wa filamu na muziki, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’ ambaye pesa imemtembelea ameonyesha kuwa na ushoga uliopitiliza na msanii mwenzake Lucy Komba baada ya kumzawadia kiwanja kwenye kicheni pati yake iliyofanyika hivi karibuni.

Msanii wa filamu na muziki, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’.

Dokii akiwa mmoja wa mastaa waliopamba vyema sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar, wakati wa kutoa zawadi alisema, yeye na Lucy wametoka mbali na ili kudhihirisha walivyoshibana, anampa kiwanja kilichopo maeneo ya Bagamoyo.

Msanii wa filamu Bongo, Lucy Komba akiwa kwenye kicheni pati yake.

“Mimi na Lucy tumetoka mbali, tumeshirikiana katika mengi na kudhihirisha upendo wangu kwake namzawadia kiwanja cha eka moja kilichopo Bagamoyo, naamini itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya urafiki wetu,” alisema Dokii.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

MKE WA KAMANDA BARLOW AFUKUZWA KWA MAPANGA KABURINI KWA MUMEWE!
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

NISHA AZUA TAHARUKI HEKALU LA FREEMASON.

STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha', Jumanne iliyopita alijikuta akizua taharuki kufuatia kuegesha gari lake nje ya Hekalu la Freemason lililopo nyuma ya Hyatt Regency Dar es Salaam The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam.


Upande wa mbele wa Hekalu la Freemason lililopo karibu na hoteli ya Hyatt Regency Posta, Dar es Salaam.

Taharuki hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason.
PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
Baadhi ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo.

Chanzo chetu kilidai kuwa msanii huyo baada ya kuona amezingirwa na watu alisimama na kuzungumza nao kisha akabadili uamuzi, alirudi ndani ya gari na kuondoka eneo hilo ambapo baadhi ya watu walidai huenda alitaka kuingia kwenye hekalu hilo kama mastaa wenzake ambao mara nyingi huonekana wakiingia na kutoka.

Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Kufuatia taarifa za chanzo hicho, gazeti hili lilimsaka msanii huyo na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo alifafanua kuhusu suala hilo."Aah! Dah, nyie habari hizo mmezipataje, mbona pale sijaona mwandishi yeyote? Ukweli pale mimi nilipaki gari tu kwa ajili ya kufanya mambo yangu maeneo yale lakini ghafla nikashangaa umati umenivaa, kila mtu anataka kuniona laivu na kuongea na mimi.

“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na  kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha.

Kumekuwa na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki.

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWAMKE WA KAMANDA BARLOW AFUKUZWA KWA MAPANGA KABURINI KWA MUMEWE!
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

MUME: KAJALA NITOE GEREZANI.



Kajala na mumewe siku ya ndoa
ANA hoja? Siku chache baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda, toleo la Jumatatu iliyopita kuripoti juu ya utajiri mkubwa wa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’, mumewe Faraji Agustino amempigia saluti na kumuomba amtoe gerezani.

Kajala na mumewe wakiwa mahakamani.

KWANI ILIKUWAJE?
Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi kama wanavyoita mastaa wa Kibongo.

UTAJIRI WA GHAFLA
Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla.

HOJA YA MSINGI
Baada ya kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa.

MUME AZIMIA BAADA YA KUZIONA PICHA ZA UCHI ZA MKE WAKE MITANDAONI, !

GEREZANI SEGEREA
Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.

Akizungumza kwa huruma, Faraji alisema habari za Kajala kuwa na utajiri wa kutupwa alianza kuzisikia kwa ndugu zake hivyo kumuomba staa huyo kumkumbuka kwenye ufalme wake.

Jamaa huyo alisema kila akikaa huwa anakumbuka good time (kipindi cha matanuzi) yao ambapo ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hasa nyakati za wikiendi.

Kwa mujibu wa mtu wetu huyo, Faraji alimwambia: “Mwambieni K akumbuke yeye ni mke wangu. Nimemsaidia kwa mengi, asiniache nateseka huku yeye anachezea pesa ambazo anaweza kunilipia na nikatoka kifungoni. Pia akumbuke ahadi yetu ya ndoa kanisani na jinsi tulivyoishi kwa upendo.

“Bado ni mke wangu, bado nampenda sana. Nilisikia alishavua pete ya ndoa lakini ukweli ni kwamba bado mapenzi yetu yapo palepale. Kama kweli Kajala amepata utajiri naomba anitoe gerezani, sitamsahau maisha yangu yote. Kama nilivyoahidi kanisani, nitampenda na kumtunza hadi kifo kitutenganishe.”

Chanzo hicho kilidai kwamba Faraji alisema Kajala amuonee huruma, azungumze na wadau wake wote wamtoe gerezani halafu atajua jinsi ya kurejesha fedha hizo.Habari nyingine kuhusu suala hilo ilisemekana kwamba jamaa huyo ametengeneza netiweki akiwa gerezani kupitia kwa watu wake wanaomtembelea ambao wapo tayari kuungana na staa huyo ili kufanikisha jambo hilo.

INAWEZEKANA?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wanasheria wenye uzoefu na kesi za mastaa aliyeomba hifadhi ya jina alisema kwamba jambo hilo linawezekana endapo mteja (mume wa Kajala) ataomba kesi yake ifanyiwe ‘reference’ (mapitio).

“Unajua haya ni mambo ya kisheria, kwa mtu wa kawaida anaweza asiyaelewe kirahisi lakini uwezekano upo bila hata kukata rufaa.“Faraji alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (Dar). Kitakachofanyika ni kwamba kama akitaka kesi yake itafanyiwa reference kwenye mahakama ya juu.
“Baada ya hapo Faraji au wakili wake anaweza kuomba kulipa faini badala ya kifungo kwa sababu hukumu ilisema kifungo cha miaka saba au faini ya hiyo shilingi milioni 200.

“Kama kweli Kajala ana hiyo fedha si mbaya akafanya hizo process (taratibu), akamtoa mumewe,” alisema ‘loya’ huyo.

KAJALA ANASEMAJE?
Baada ya kujazwa data hizo, Jumatano iliyopita Ijumaa lilimtafuta Kajala ambaye simu yake haikuwa hewani kila ilipopigwa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo lakini kwenye makabrasha kulikuwa na maelezo yake juu ya mumewe alipohojiwa siku kadhaa zilizopita.

Kwa mujibu wa Kajala, Faraja bado ni mumewe na huwa anakwenda gerezani kumuona kila wikiendi na anatamani awe huru ili waendelee na maisha kwani hawakuwa wamefaidi penzi lao, hata mtoto walikuwa hawajapata.

MARAFIKI WANASEMAJE?
Marafiki wa wanandoa hao waliozungumza na Ijumaa walisema kwamba kama kweli Kajala ana nia hiyo, basi afanye hiv yo kwani itakuwa thawabu kubwa kwake kama alivyofanyiwa na Wema aliyemnusuru kifungo cha miaka mitano jela.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Thursday, September 4, 2014

A woman is hacked to death with machete in garden at North London.

     Woman found dead in back garden in Nightingale Road, Edmonton
    Press Association reports she had been beheaded with machete but police spokesman yet to confirm
    Police were initially called to reports of a man attacking a dog or cat
    Taser used and armed police officer believed to have suffered suspected broken wrist
    Police say one man was arrested at the scene on suspicion of murder and is being treated in hospital
    No indication of any terrorism motive

Police have now confirmed that Palmira Silva was the victim of the killing in north London today.

The 82-year-old, who is believed to be of Italian descent, was found dead outside a house in Edmonton.

Scotland Yard said that while formal identification has yet to take place, its officers were satisfied that she was the victim discovered in Nightingale Road.


A 25-year-old man was Tasered and arrested on suspicion of murder at the scene by armed officers, some of whom were injured in a struggle.

He is currently under guard in hospital.
8:08 pm

Sky News are reporting that the suspect is thought to have tried to attack two other people before the death of 82-year-old Palmira Silva.

A number of eye witnesses reported a man 'went on a rampage' in back gardens in Nightingale Road, Edmonton.

A 25-year-old man has been arrested and inquiries are continuing.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

MUME AZIMIA BAADA YA KUZIONA PICHA ZA UCHI ZA MKE WAKE MITANDAONI, !

PICHA HIZI NI MBAYA KWA WATOTO HIVYO KAMA HUJAFIKISHA MIAKa 18 USIJE KUJARIBU KUBOFYA HAPO CHINI.
KUZIONA BOFYA HAPA



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

MAMBO Ma 5 YANAYOUMIZA WENGI KATIKA MAHUSIANO HAYA HAPA.

1. Kuna jambo huwezi ficha: Kuna jambo hata ukijaribu kulificha, ukweli wake utajulikana tuu hususani kama utakuwa na mahusiano ya muda mrefu na mtu husika. Jambo hilo ni ukweli  kama unampenda kwa dhati mwenza wako au la. Mpenzi wako akiwa makini atagundua ‘kufeki’ kwako , kutokana na matendo yako hususani vile unavyojali hisia zake, usikivu wako kwake, heshima yako kwake, na unavyojali umoja na kudumu kwa uhusiano wenu.
MKE WA KAMANDA BARLOW AFUKUZWA KWA MAPANGA KABURINI KWA MUMEWE!
2. Fedha sikuzote itawasumbua: Hata kama mtajitahidi kupuuzia umuhimu wa fedha katika mahusiano yenu, fedha itabaki kuwa mhimili mkubwa wa mahusiano yenu. Hata kama nyote mna ingiza kipato kuna changamoto mtazipata kama vile kupanga kwa pamoja jinsi ya kutumia fedha zenu, au kujieleza kuhusu matumizi fulani ambayo mwenzi wako atahoji.

3. Kazi ya ziada: Haijalishi una hisia na makusudio mazuri sana, bila matendo yanayomridhisha mpenzi wako, hautoweza kujenga furaha ya kweli katika mahusiano yenu. Ni muhimu pia kutambua kwamba pamoja na kuwa na makusudio na matendo mazuri, inakupasa kutilia mkazo kuwa matendo yako na makusudio yako yanaaminika kwa mpenzi wako.

4.Kuna mambo hautokaa ujue ukweli wake: Haipendezi ila ndio uhalisia kuwa pamoja na ukweli kwamba nyie mmeshibana katika mahusiano yenu, bado kutakuwepo na siri ambazo haitaambiana. Mbaya zaidi katika siri hizo, inaweza kuwepo siri ya hisia halisi kuhusu upendo wa mpenzi wako kwako, au upendo wako kwake. Mfano, wapo waliooana lakini mmoja wapo sio kwamba kweli anampenda mwenzake, ila alitaraji kujenga upendo akiwa kwenye ndoa, na kweli anapokuwa kwenye ndoa anajikuta amejenga kumjali mpenzi wake, hatimaye anajikuta ameweza kumpenda moja kwa moja.
PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
5.Makosa haya ni magumu sana kusahaulika: Kwa kawaida binadamu wengi hukumbuka mabaya kwa urahisi kuliko mazuri tunayowafanyia. Na katika mahusiano, makosa haya mawili ; kwanza ni ‘ku cheat’ na pili kutokuonyesha mvuto wa kimapenzi kwa mpenzi wako, yanaweza kuwa makosa ambayo si rahisi kusahaulika, ingawaje mtu atajitahidi kusamehe, na kujaribu kufanya mahusiano yaende kawaida.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

KAMA HUMTAKI WEWE: PICHA 10 ZA NYUMBA ATAKAYOISHI MARIO BALOTELI UINGEREZA .

Mario Balotelli ndio kwanza amerejea England, kwa mara ya pili, lakini inaonekana haijamchukua muda mrefu kugonga vichwa vya habari, safari hii kwa kuonesha "ladha" ya mitindo na mambo anayopenda.

Mchezaji huyo wa Liver...pool aliyenunuliwa kutoka AC Milan kwa pauni milioni 16, amekuwa akitafuta nyumba, na inasemekana ameichagua hii (katika picha) iliyopo nje ya mji, - eneo la Helsby, Cheshire - na kufanya ndio "keja".

Na kama picha hizi pamoja na habari ambazo zimeandikwa na magazeti na tovuti kadhaa hapa Uingereza ni za kuaminika, basi inaonekana Balotelli ameonesha 'staili' yake kwa 'kuteua' jumba hili ambalo thamani yake ni pauni milioni 4.7.

Nyumba hii ina vyumba vitano, ikiwa pamoja na kila kitu ambacho mchezaji soka , Kijana, milionea anahitaji. Vitu 'muhimu' kama bwawa la kuogelea, sauna, chumba cha kuhifadhia mvinvyo (wine cellar), sehemu ya kutua helikopta, uwanja wa mpira.
 CREDIT:http://kalumbimbi.blogspot.com

PICHA ZAIDI HAPO CHINI








HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA 

PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU 

MKE WA KAMANDA BARLOW AFUKUZWA KWA MAPANGA KABURINI KWA MUMEWE!

habari kamili :: read more...

KILE KIKAO CHA UKAWA NA RAIS KIKWETE KILIISHA HIVI.

Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Tuligoma mbele ya Rais Jakaya Kikwete kuruhusu wajumbe wao kurejea katika Bunge Maalumu la Katiba, walipokutana katika kikao cha kusaka suluhu ya mkwamo wa mchakato wa Katiba.Mkutano wa jana ulikuwa na sehemu mbili kuu, wa kwanza ulifanyika katika Ikulu ya Kilimani, Dodoma ambako viongozi hao walikutana na Rais Kikwete na mwingine katika Hoteli ya St. Gasper ambao uliwashirikisha viongozi na maofisa wa vyama vilivyoshiriki bila Rais Kikwete.Mkutano huo ni matunda ya jitihada zinazofanywa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambacho kiliratibu mazungumzo hayo yaliyochukua zaidi ya saa mbili na nusu, katika Ikulu ya Kilimani, wakati yale ya St. Gaspar yalichukua takriban saa moja na nusu.

Viongozi walioshiriki kikao hicho cha Ikulu ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Tanzania Bara), Magdalena Sakaya.Wengine ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Katibu Mkuu wake, Mosena Nyambabe, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Mwenyekiti wa UDP ambaye pia ndiye mwenye zamu ya uenyekiti wa TCD, John Cheyo na Mwenyekiti wa UPDP pamoja na mwakilishi wa vyama visivyokuwa na wabunge ndani ya TCD, Fahmi Dovutwa.

CHAMA CHA MAPINDUZI UK CHAPATA MWENYEKITI MPYA.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Rais Kikwete baada ya kuanza kwa kikao hicho alitoa fursa kwa kila aliyekuwapo kuzungumza na hapo zilijitokeza hoja mbalimbali, nyingi mwelekeo wake ukiwa ni kutaka kusitishwa kwa Bunge Maalumu ili kutoa fursa kwa nchi kuendelea na masuala mengine makubwa.Chanzo chetu kilisema: “Rais amekuwa msikivu kweli, amewasikiliza wote lakini ugumu ulianza kuonekana pale ilipotolewa kauli ya kuwauliza wale watu wa Ukawa kama wanaonaje wakirejea halafu hoja zao zikazungumzwa ndani ya Bunge Maalumu, yaani hawataki kabisa kusikia hilo.

”Kuhusu hoja ya kusitishwa kwa Bunge, habari zinasema ilijadiliwa kwa kirefu na wataalamu wa sheria wakijaribu kutoa uzoefu wao, lakini kikwazo kilichoonekana ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo haimpi Rais mamlaka ya kusitisha Bunge.

“Rais alisema hoja zao ni nzuri na zina mashiko, lakini suala kubwa likawa ni kwamba tunafikaje huko wanakopendekeza? Maana sheria iko kimya kuhusu mamlaka ya Rais kusitisha Bunge Maalumu, ndiyo maana sasa tulitoka Ikulu tukaenda St. Gaspar ili kujadili, ngoja tusubiri hiyo tarehe 8 maana siyo mbali,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.Kauli ya TCDBaada ya kikao cha St. Gasper, Mwenyekiti wa TCD, Cheyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba mazungumzo na Rais Kikwete yalikuwa mazuri na kwamba wamekubaliana kukutana naye tena Septemba 8, mwaka huu baada ya kuwa wamezifanyia kazi hoja ambazo zilijitokeza kwenye vikao hivyo.

“Kama nilivyowaambia siku ile tulipokutana, tulikuwa na ajenda mbili tu kubwa, kwanza ni mchakato wa Katiba Mpya unavyokwenda na ajenda ya pili ni jinsi tunavyoweza kusonga mbele na kuwa na maandalizi ya uchaguzi mzuri mwakani,” alisema Cheyo lakini akikataa kujibu maswali mengine ya waandishi wa habari.Cheyo alisema baada ya kukutana na Rais Kikwete, waliendelea na kikao cha viongozi wa vyama kwa ajili ya kuona jinsi ya kuyafanyia kazi mambo yaliyojitokeza, hivyo wameamua kuunda kamati ndogo ya watu wanne itakayoongozwa na Mbatia kwa ajili ya kutekeleza wajibu huo.
PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Kinana, Profesa Lipumba na Dk Slaa ambao wamepewa wajibu wa kuwasilisha ripoti yao kwenye kikao cha wenyeviti wa vyama vinavyounda TCD ili ijadiliwe kabla ya kikao cha Septemba 8, ambacho hata hivyo, hakijafahamika kitafanyika wapi.Habari zinasema miongoni mwa mambo yatakayofanyiwa kazi ni pamoja na kuona kama Bunge linaweza kusitishwa bila kuleta athari zozote za kisheria na kisiasa, lakini wakizingatia uwapo wa makundi mengine ndani ya Bunge hilo hasa wabunge wa kuteuliwa kupitia kundi la 201.

“Lakini hapa kuna suala moja kwamba Ukawa wako nje ya Bunge, ni vigumu kuwaamrisha wale walioko ndani ya Bunge ili watekeleze matakwa yao, kwa hiyo kuna kazi kubwa sana ya kufanya,” kilisema chanzo chetu.Mgomo wa UkawaDalili za Ukawa kukataa kurejea bungeni zilianza kuonekana mapema baada ya mazungumzo yasiyo rasmi ambayo yalifanyika katika moja ya kumbi za Hoteli ya Dodoma ambako walikwenda kupata chai baada ya kuwasili.

Wakati wakitoka kwenye ukumbi huo kuelekea Ikulu Kilimani, baadhi yao walisikika wakipeana tahadhari kwamba wasikubali wazo la kurejea bungeni, ambalo ni dhahiri walikuwa wamepewa wakati wakinywa chai.Baadaye ndani ya basi dogo wakati wakielekea Ikulu, Lissu alisikika akisema: “Eti wanataka turejee, yaani tumekaa nje muda wote huo halafu leo hii tuje hapa kujadili kurudi, eti kurudi haiwezekani kabisa.

”Pia habari kutoka katika Ukumbi wa St. Gaspar zinasema hata katika kikao hicho, viongozi hao walishauriwa kurejea bungeni ili hoja za kuahirishwa kwa Bunge Maalumu zitolewe huko, lakini waligoma.Taarifa zinasema Ukawa walijenga hoja kwamba Bunge Maalumu halipaswi kuendelea kwa sababu kuna kila dalili kuwa muda uliopo hautoshi kukamilisha mchakato na ikizingatiwa kwamba nchi inakabiliwa na mambo mengi ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Pia kulikuwa na hoja kuhusu mambo ya Daftari la Wapigakura na mabadiliko ya sheria ambazo zinagusa taasisi kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi, sheria mbalimbali zinazihusu vyama vya siasa na mambo ya matokeo ya rais kuhojiwa nadhani,” kilieleza chanzo kingine.Kushindwa kupatikana kwa suluhu ya mchakato wa Katiba, kunaendelea kuuweka mchakato huo njiapanda hasa ikizingatiwa kwamba Bunge Maalumu linaendelea kesho kupokea ripoti za kamati kuhusu uchambuzi wa sura 15 za Rasimu ya Katiba.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

JOHARI: BADO NIPO NIPO SANA.

MKONGWE kwenye kilinge cha sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amewataka mashabiki wake wajue kwamba, muda ukifika wa kupata mume wa kufunga naye ndoa, atafanya hivyo lakini kwa sasa anatoa kipaumbele kwenye kazi tu.

Mkongwe kwenye kilinge cha sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.

Akizungumza na Amani, Johari ambaye umri wake upo juu ya miaka 30, alisema watu wengi wanafikiri kuwa ndoa ndiyo kila kitu katika maisha lakini kwa upande wake bado hajaifikiria.

“Kitu ambacho nakiamini mimi ni kwamba ndoa kama nimepangiwa na Mungu ipo na itaendelea kuwepo haijalishi hata kama nitafikisha miaka hamsini,” alisema  Johari.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

KWA MARA YA KWANZA WEMA SEPETU AFUNGUKA KUHUSU KUAJIRIWA NA KAJALA, MSIKILIZE HAPA.

Kupitia mitandao na magazeti siku chache zilizopita ilitoka stori ambayo ilidai Kajala anaelekea kumuajiri Wema Sepetu,leo Wema kapatikana na kakubali kuongelea isue hizo zote ikiwemo hiyo ya Kajala.

Kupitia You heard ya  XXL ya Clouds Fm Soudy Brown alianza kwa kutaka kufahamu kama kweli Kajala anaweza kumuajiri yeye[Wema],Wema Sepetu akamjibu>>’Inawezekana,kila kitu kinawezekana Soudy’  Kuhusu mshahara ambao anataka kulipwa na Kajala,Wema Sepetu amejibu>>’Kwa Kajala mi sihitaji mshahara hata bure nitafanya kazi kwa Kajala,shughuli yoyote nitafanya Soudy’
Soudy Brown alipomuuliza kuhusu fununu za Meninah kutoka na Diamond,Wema amejibu>>’Mimi sijui Soudy bwana na wala sijali’..
MSIKILIZE HAPO CHINI;


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Gari La Rais Lililoibwa Kenya Lapatikana Uganda.

Jumatano ya wiki iliyopita ndio liliibwa hili gari aina ya BMW lisilopenya risasi ambalo huwa linakuwepo kwenye msafara wa Rais Kenyatta, na taarifa ya Ikulu ilisema liliibwa wakati dereva wake ambae ni askari alikua akielekea kwenye makazi ya Polisi Nairobi, njiani akasimamishwa na watu waliokuwa na AK 47 wakamtupa mtaroni baada ya kumvua nguo na kukimbia nalo.

Taarifa mpya ambayo inaripotiwa na Julius Kepkoich toka Kenya inasema gari hili limepatikana kwenye mji wa Tororo Uganda na tayari limepelekwa Kampala baada ya msako uliofanywa na Polisi na kumkamata mshukiwa mmoja hotelini mjini Bungoma.

Kikosi cha Polisi wa Flying squard kikishirikiana na Interpol walivuka boda na kuingia mji wa Tororo Uganda walikohisi kwamba ndiko kulikopelekwa gari hilo.

Polisi wanamshikilia Nelson Topicho aliyekamatwa Bungoma na anatarajiwa kurejeshwa Nairobi ili kuhojiwa zaidi ambapo kikosi kingine cha Nakuru Kenya kinamshikilia Agrey Odhiambo anaetuhumiwa kukarabati gari lililoibwa na kumiliki bunduki huku Nairobi wakitarajiwa kumuhoji upya dereva wa Ikulu David Muchui.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

TAZAMA MAMBO YA AJABU AMBAYO HUTENDEKA KWENYE KUMBI ZA STAREHE.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Ronaldo aka CR7 asema anafikiria kurejea Manchester United siku moja.

The Real Madrid star has reiterated his desire to return to Old Trafford and is confident Angel Di Maria and Radamel Falcao will help the club overcome their poor start
Real Madrid attacker Cristiano Ronaldo has admitted that he is keen to return to Manchester United at some point in the future.

The Portugal international enjoyed a hugely successful time at the Old Trafford side between 2003 and 2009 before leaving United for Madrid in a deal worth a then world-record £80 million.
"I love Manchester. Everyone knows that - I have said it many times. Manchester is in my heart. I left many good friends there, the supporters are amazing and I wish I can come back one day," Ronaldo told the Daily Mail.

"I am happy here at Real Madrid and have four more years, but in the future you never know because they treated me unbelievably at United. I really did love being at Manchester United."

The prolific attacker then went on to discuss Louis van Gaal's side's difficult start to the new season and stressed that he's confident they will improve following the arrival of Angel Di Maria and Radamel Falcao.

He continued: "Believe me, they will be a good team again, I’m sure of it. It is a great club.

"This can happen. Bad moments and good moments. Manchester are passing through a bad moment. Last year it was a horrible season and this year they haven’t started well, either.

"But I do think they did well to buy Di Maria and Falcao. I think the team will be much better. I want to see them better because it is such a fantastic club and they deserve to be better.

"Manchester have not started well, two points in three games, so they need quality players and Falcao is a quality player. And Di Maria, too."

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

TAZAMA MAMBO YA AJABU AMBAYO HUTENDEKA KWENYE KUMBI ZA STAREHE.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

SHILOLE: MPENZI WANGU ANANITIBU VIZURI.


Akizungumza na paparazi bila kung’ata maneno, Shilole alisema wengi wanashindwa kujua kwamba mtu anaweza kuwa na mwanaume mwenye umbo kubwa lakini akawa hayajui mapenzi lakini mwenye umbo dogo kama Nuh, akawa ni bingwa wa mapenzi.
Akiendelea kumwaga data mbele ya kinasa sauti cha Amani, msanii huyo anayetamba na wimbo wa Nakomaa na Jiji alisema kuwa katika mapenzi, umri wala ukubwa wa umbo hauna maana yoyote.

“Yaani kwa kweli Nuh ananimudu na tunaenda sawa katika suala zima la mapenzi, kwa hiyo sioni udogo wake kwangu, kwa upande wangu Nuh ni mkubwa sana watu wasiangalie mwili,” alisema Shilole pasipo kutaja umri wa mpenzi wake huyo.

TAZAMA MAMBO YA AJABU AMBAYO HUTENDEKA KWENYE KUMBI ZA STAREHE.

Shilole aliongeza kuwa, kutokana na mahaba ya nguvu anayoyapata kutoka kwa mpenzi wake huyo, anapata nguvu ya kufanya kazi vizuri siku hadi siku hivyo hapati tamaa.
Staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
“Sina stress za mapenzi na mara nyingi nafanya kazi zangu zinaenda sawa kabisa,” alimalizia Shilole.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

JIONEE PICHA MBALIMBALI ZA BASI KUBWA JIJINI DAR MAARUFU KAMA CITY TRAIN LIKIKATIZA KARIAKOO.
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

ACHOMWA MOTO AKIDAIWA KUIBA BAISKELI MOROGORO.

 Mwili wa kijana huyo ukiwa katika gari la polisi kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
 Gari la polisi likiondoka na mwili wa kijana huyo.
Wanafunzi wa Sekondari ya Alfa James wakishuhudia mahali alipochomewa mtuhumiwa.
Raia wengine waliofika eneo la tukio
KIJANA anayesadikiwa kuwa kibaka na ambaye hajafahamika jina lake, leo asubuhi amechomwa moto hadi kufa akidaiwa kuiba baiskeli maeneo ya Nane Nane mjini Morogoro, jirani na shule ya Sekondari ya Alfa James ambayo ni maarufu kama Shule ya Father Pekupeku.

”Majira ya saa moja asubuhi tumeona vijana wanne wakimfukuza mwenzao, walipofika hapa kwenye mabweni ya shule ya Alfa, wakamkamta akiwa na baiskeli na kumshushia kichapo kikali na baadaye wakamchoma moto wakidai alikuwa ameiba baiskeli yao maeneo ya Tubuyu, ” alisema shuhuda mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Mama Happy.

Mtandao huu ulishuhudia kijana huyo akiendelea kuteketea kwa moto akituhumiwa kuiba baiskeli kuukuu yenye thamani ya shilingi  60,000. Polisi walifika  na kuuchukua mwili huo na kuupeleka Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Spotlight on Nollywood:

A bright young journalist battles homelessness after her drug addicted sister throws her out of the house.

She also fights to keep her job when her demanding boss instructs her to deliver a story that her conscience will not allow.
Starring: Belinda Effah, Ini Edo, Desmond Elliot.
Directed by: Lancelot Oduwa Imasuen

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

MKE WA KAMANDA BARLOW AFUKUZWA KWA MAPANGA KABURINI KWA MUMEWE!
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Pichaz nyingine za harusi ya Angelina Jolie na Brad Pitt!.

 Ilikua ni ndoa ambayo walifunga kwa siri, yani bila kuitangaza kwenye vyombo vya habari ambapo ishu nzima ilifanyika nchini Ufaransa na kuhudhuriwa na watu 22 peke yake.


Mmoja wa watu wao wa karibu amesema wawili hawa kwa sasa wako serious kuhusu uhusiano wao na kuishi pamoja maishani na siku hizi hawana mikwaruzo ya mara kwa mara kama zamani na wanampango wa kubadilisha majina na kuitwa Jolie-Pitt.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Diamond Platnumz azungumza kwa mara ya kwanza mambo 6 kuhusu fujo zilizotokea Ujerumani.


 Kuanzia siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye kiwanda cha burudani Tanzania imehusu fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya Diamond Platnumz huko Stuttgart.

Kilichotokea ni kwamba saa kumi alfajiri ndio promota alimpeleka Diamond kwenye ukumbi kunakofanyika show. Kwa nini ilitokea akamchelewesha? nini kilitokea baadae? hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe kwenye exclusive na millardayo.com

1. ‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’

2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’

3.Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’

4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’

5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia walichokitarajia’


6. ‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule, nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’

Unaweza kumsikiliza Diamond mwenyewe kwa kubonyeza play hapa chini.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Messi retirement is inconceivable for Argentina.

The reports of his international retirement have been greatly exaggerated. Lionel Messi is still sad after Argentina lost the World Cup final to Germany in July, but the Barcelona forward remains committed to his country - despite all of the criticism he continues to receive.

Argentina face Germany on Wednesday in Gerardo Martino's first game as coach, a repeat of the Maracana meeting in July which Joachim Low's side won thanks to Mario Gotze's extra-time goal. And Messi misses the latest match through injury due to a strain in his right adductor picked up in Barca's 1-0 win at Villarreal on Sunday.

In Argentina, some said that was a convenient excuse to sit out the Germany game in Dusseldorf, while other reports claimed the 27-year-old intended to quit his national team altogether.

Neither are true.

What is true is that, this year, Messi's main focus is Barcelona and not Argentina. In the months leading up to the World Cup, the forward geared his fitness programme towards Brazil 2014, was allowed to recover from injury back in his native Rosario and was even granted permission by the Catalan club to fly over the Albiceleste kinesiologist for special training in the lead-up to the tournament.

World Cups come only once every four years and Messi feels it is fair to give his full focus to Barcelona this season - and not Argentina. The 27-year-old will play in the Copa America next summer for his country, but is likely to miss some friendly fixtures for the Albiceleste, concentrating instead on the important dates.

"Lionel isn't leaving the national team," the player's father said this week. "It's just something made up by the press and there is no truth in it." And Barca team-mate Javier Mascherano added: "Leo is more committed than anyone to the national team. It's crazy to think he would give up on the Seleccion."

Messi's career with Argentina has had its difficulties. In the early years, the Barca forward received fierce criticism in his homeland, with many fans accusing him of caring only about making money at the Catalan club or not caring about his national team. Some supporters even believed the Albiceleste should pick playmaker Juan Roman Riquelme instead - even though Messi is a far superior player to the veteran No.10.

Leo was upset by criticism following Argentina's World Cup final defeat, frustrated that he was being blamed for a poor game against Germany after carrying the team through the early stages of the competition almost single-handedly.

But the captain's performances in Brazil and his obvious sadness as he stood with the Golden Ball trophy in Rio instead of the World Cup saw him gain greater popularity in Argentina than ever before. It has taken time, but Messi is finally winning over his compatriots. Against Germany on Wednesday he will be missing, but a future without him remains unthinkable.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Wednesday, September 3, 2014

MAHAKAMA YAMFUNGA JELA MWIZI WA NYAYA ZA TTCL.

Mmoja wa watuhumiwa wa nyaya za simu (Picha na Maktaba).
Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam imemuhukumu kwenda jela miaka minne, Shaibu Muhidin Ndina baada ya kupatikana na kosa la kuiba nyaya za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Hukumu hiyo imetolewa Agosti 25, 2014 katika mahakama hiyo na B. Mashabara baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa hilo la wizi wa nyaya(cables) za kampuni ya TTCL zenye thamani ya shilingi milioni 15.

Awali akisomewa shitaka hilo, Muhidin Ndina anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 11, 2013 maeneo ya Boko Katika Wilaya ya Kinondoni kabla ya kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi namba 12/2013.
“Aliiba nyaya (cables) za thamani ya milioni 15 alitenda kosa hilo Januari 11, 2013 Boko Katika eneo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam ” ilisomeka sehemu ya hukumu ya kesi hiyo.
Uharibifu wa miundombinu ya umma zikiwemo nyaya za simu za Kampuni ya TTCL umekuwa ukishamiri maeneo kadhaa jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kubwa kwa kampuni na usu mbufu kwa wananchi na watumiaji wa huduma za TTCL.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

HUYU NAYE AOTESHWA NDEVU, BAADA YA KULIPUKIWA NA BOMU MIAKA 1O ILIYOPITA.

  Joseph Jones akifanyiwa operesheni ya kupandikizwa vinyweleo vya nyusi na ndevu huko Miami. Kulia ni Dk. Jeffrey Epstein  na msaidizi wake Jose Armas (kushoto).


KIJANA Joseph Jones raia wa Youngstown nchini Marekani ameoteshwa ndevu pamoja na nyusi ikiwa ni baada ya miaka 10 tangu alipojeruhiwa kwa kulipukiwa na bomu barabarani nchini Iraq.

Dk. Jeffrey Epstein akimwekea Joseph Jones alama za wapi atakapootesha ndevu.

Joseph aliyepoteza vinyweleo vya usoni mwaka 2004 baada ya kujeruhiwa na bomu hilo alifanyiwa operesheni ya masaa nane ambapo alipandikizwa vinyweleo zaidi ya 3,000 kwa ajili ya kuotesha ndevu zake na nyusi.

Joseph baada ya kupandikizwa ndevu na nyusi.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Tuesday, September 2, 2014

AFISA USALAMA FEKI AKAMATWA NA POLISI DAR.





Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi.

Kamanda Suleiman Kova akionyesha  silaha zilizokamatwa kwa wanahabari (hawapo pichani).

Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Kova.

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Gunner Meena (40) mkazi wa Kinyerezi, Segerea, Dar es Salaam,  kwa tuhuma za kujifanya  mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa .

Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs 25,000,000/= ama sivyo angechukua hatua chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa.

NDOA YA MWALIMU AIBU KANISA KATOLIKI MAGOMENI; ALITAKA KUFUNGA YA PILI WAPAMBE WAHAIBIKA MBAYA.

Aidha jeshi hilo katika kuendesha oparesheni zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia silaha limefanikiwa kukamata  bastola nne na shot-gun moja wiki hii.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA UBUNGO MAJI ASUBU YA LEO.

 Raia wakijaribu kuokoa maisha ya dada aliyegongwa na gari (daladala) maeneo ya Ubungo maji wakati akivuka bara bara.


Majeruhi (dada huyo) akichukuliwa kwenye gari na wasamaria wema.

HiIi ndilo gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T454 BBV lililomgonga dada huyo.

Mwanamke mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande wa Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster lililodaiwa kuvunja sheria likiwa  linapita kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi.

CHAMA CHA MAPINDUZI UK CHAPATA MWENYEKITI MPYA.

Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

MUME ASIMULIA JINSI ALIVYOFANYIWA USODOMA : KILICHOTOKEA NI HATARI TUPU.


PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top