
Upande wa mbele wa Hekalu la Freemason lililopo karibu na hoteli ya Hyatt Regency Posta, Dar es Salaam.
Taharuki hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason.
PACHA WA KANUMBA HUYU HAPA; KWELI WAMEFANANA YAANI NI KAMA KWELI VILE.
Baadhi ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo.

Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Kufuatia taarifa za chanzo hicho, gazeti hili lilimsaka msanii huyo na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo alifafanua kuhusu suala hilo."Aah! Dah, nyie habari hizo mmezipataje, mbona pale sijaona mwandishi yeyote? Ukweli pale mimi nilipaki gari tu kwa ajili ya kufanya mambo yangu maeneo yale lakini ghafla nikashangaa umati umenivaa, kila mtu anataka kuniona laivu na kuongea na mimi.
“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha.
Kumekuwa na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye.

0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment