Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

Sunday, July 12, 2015

MATOKEO YA UCHAGUZI NI John Pombe Magufuli 87%, Balozi Amina Ali 10% na Asha-Rose Migiro 3%.

July 12 2015 Tanzania ilikuwa inasubiri kwa hamu kujua Mgombea yupi anasimamishwa na CCM kwenye nafasi ya Urais 2015, ninayo Ripoti nyingine kutoka Dodoma sasahivi!!
Kura zimepigwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM na matokeo yako hivi
 John Pombe Magufuli 87%, Balozi Amina Ali 10% na Asha-Rose Migiro 3%.

Katika Mkutano Mkuu uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli amechaguliwa kwa kura 2104 sawa na asilimia 87.08, akifuatiwa na Balozi Amina Salum Ali aliyepata kura 253 sawa na asilimia 10.4 na Asha-Rose Migiro aliyepata kura 59 sawa na asilimia 2.44702.


Jumla ya kura zilizopigwa kwenye Mkutano Mkuu wa CCM kumchagua Mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa 2015 ni kura 2422, kura zilizoharibika ni sita, kura halali walizopigiwa wagombea ni 2416.
habari kamili :: read more...

Thursday, February 12, 2015

MHE. WASIRA AAMUA KUMWONA NGOWI ILI AMTENGENEZEE SUTI ZAKE.



Mhe. Stephen Wasira akichukuliwa vipmo vya suti na mbunifu wa mavazi, Sheria Ngowi.

BAADA ya kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kutofunga vizuri vifungo vya suti yake,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen Wasira ameamua kumuona mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ili aanze kumtengenezea suti zake.

Waziri Wasira akijaribu kurekebisha suti yake iliyokosewa kufungwa vifungo na kuzua mjadala mitandaoni.

Mhe. Wasira ameamua kukutana na mbunifu huyo aliyeanza mara moja kumchukua vipimo vyake ili amtengenezee mavazi yake ambayo atakuwa akiyatumia katika shughuli zake mbalimbali za kiserikali.

Picha za Waziri Wasira zilienea mitandaoni alipopiga picha ya pamoja akiwa na Viongozi wa Kanisa la Kisabato kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la suti yake likiwa limekosewa kufungwa vifungo.
Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walirusha picha mbalimbali zikimuonesha Mhe. Wasira huku mmoja wa watangazaji akisema kuwa iwapo akikubaliwa, atajitolea kuwa wabunifu wa suti zake za mitoko ili jambo hilo lisijitokeze tena.

Mhe. Wasiara akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kanisa la Kisabato kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la suti yake likiwa limekosewa kufungwa vifungo.

Kwa kuamua kumuona Sheria Ngowi, Mhe. Wasira atakuwa amepata mti shamba wa tatizo hilo lililotawala mitandao ya kijamii hivi karibuni.

U.S. Leads 12 Air Strikes Against Islamic State – U.S. Military.

UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Wednesday, February 11, 2015

Chibok girls have not yet released – Defence HQ.

Abuja (NAN) – The Defence Headquarters (DHQ) has said that “the story circulating in respect of the release of the Chibok girls is not true.”

The clarification is contained in a statement posted on the DHQ website on Tuesday.

According to the statement, the buses that drove into the barracks in Maiduguri purportedly carrying the girls were conveying other individuals.

The News Agency of Nigeria (NAN), however, learnt that the DHQ would soon address newsmen on some of the recent developments in the counter-insurgency campaign. Many terrorists were said to have died in the campaign, while many were captured by troops and some others willingly surrendered themselves.

EXCLUSIVE: TEVEZ AFUNGUKA ALIVYOTESWA.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Tanzania Yasikitishwa na Uamuzi wa Kenya wa kuzuia magari ya kitalii ya Tanzania.

Serikali imeelezea kusikitishwa na uamuzi wa Kenya wa kuzuia magari ya kitalii ya Tanzania kwenda kuchukua na kushusha watalii wanaotumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, kwa kusema kuwa hatua hiyo haijengi wala kuendana na dhamira njema ya mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe alisema jana kuwa,  dhamira ya kuanzishwa upya kwa jumuiya hiyo haiendani  na tukio la aina hiyo.

Hata hivyo alisema kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kuheshimu na kuzingatia amri iliyotolewa na Kenya ili kulinda undugu na urafiki uliopo kati ya nchi hizo huku wakitafakari hatua za kuchukua kuondoa bughudha iliyotokea kwa watalii na wasafiri wanaopitia uwanja huo.

Waziri Mwakyembe alieleza kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea na mchakato ulioanzishwa wa kuhusisha wadau wote wanaoguswa na tatizo hilo hadi kufikia  uamuzi ambao utauwasilisha kwa Serikali ya Kenya kupitia vikao rasmi vya Jumuiya.
Hata hivyo, alisema pamoja na kwamba amri hiyo ya Serikali ya Kenya inakwenda nje ya mkataba wa 1985 kwa kuvihusisha hata viwanja vya ndege kuwa sehemu ya vivutio vya utalii, Serikali ya Tanzania itaheshimu na kuzingatia amri hiyo ili kulinda undugu na urafiki uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Alisema pia kwamba Serikali itatafakari hatua za kuchukua ili kuondoa bughudha kubwa itakayotokea kwa watalii na wasafiri wanaokuja nchini wanaopitia uwanja huo wa Jomo Kenyatta.
Alizitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuwafahamisha watalii na wageni wote wenye nia ya kutembelea vivutio vya kitalii vya Tanzania kutumia viwanja vingine vya ndege ili kuepuka kadhia na gharama zisizo za lazima.

Waziri huyo alisisitiza kuwa viwanja vya ndege hasa vile vya kimataifa vitaendelea kuwa sehemu ya milango ya kuingilia na kutokea kwenda kokote ndani ya Jumuiya au nje ya Jumuiya na havitachukuliwa kama vivutio vya utalii.

"Tanzania haitazuia magari ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au nchi nyingine yoyote kuingia katika viwanja vyake vya ndege kuleta au kuchukua watalii wanaopitia katika viwanja hivyo na kwenda katika nchi zao," alisema.

Dk Mwakyembe ambaye ni Waziri mpya kwenye wizara hiyo alisema mkataba wa mwaka 1985 kati ya Tanzania na Kenya ulilenga kutoa mwongozo wa ushirikiano katika Sekta ya Utalii kati ya nchi hizo mbili.

Aliongeza kuwa makubaliano hayo yalielekeza maeneo muafaka kwa ajili ya kubadilishana watalii huku ikizingatiwa kuondoa bughudha kwa watalii.

Maeneo hayo ni pamoja na miji ya mipakani na miji rasmi iliyopendekezwa na kukubalika na pande zote mbili ikiwemo Nairobi ambako Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta kipo.

EXCLUSIVE: TEVEZ AFUNGUKA ALIVYOTESWA.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Tuesday, February 3, 2015

Afisa Elimu Mbinga avuliwa madaraka.

BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limemvua madaraka afisa elimu msingi wa wilaya hiyo Daniel Mkali baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa muda kwa tuhuma mbalimbali zilizotajwa na baadhi ya madiwani pamoja na viongozi wa idara hiyo ya elimu msingi na kuelekea kutishia kuibuka kwa mgogoro wilayani humo.
 
Akitangaza uamuzi huo wa kumvua wadhifa huo pamoja na kumshusha cheo na kutakiwa kupangiwa shule ya kufundisha mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Mbinga Alanus Ngahi, mbele ya madiwani pamoja na watumishi wengine wa halmashauri hiyo amesema uamuzi huo umefikiwa na kamati ya maadili iliyokutana kujadili suala hilo la kinidhamu na kiutumishi na baraza hilo kuridhia hatua zichukuliwe dhidi ya afisa elimu huyo.
 
Akizitaja tuhuma nne zilizokuwa zikimkabili afisa elimu huyo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Hussein Isa amesema ni pamoja na kusajili asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyojulikana kwa jina la (UWEKAMBI) umoja wa waratibu elimu kata ya Mbinga na kuwaagiza walimu wakuu wa shule za msingi wilayani humo kuhamishia fedha zote za capitation na michango ya Umitashumta jumla ya shilingi milioni 232 ambapo katika fedha hizo shilingi milioni 60 ni michango ya Umitashumta, milioni 10 ni michango ya wazazi na shilingi milioni 61 ni fedha kwa ajili ya capitation na mitihani zilipelekwa kwenye akaunti yenye namba 61714000405 iliyopo katika benki ya NMB tawi la Mbinga.
 
Ameitaja tuhuma nyingine kuwa ni kughushi nyaraka kwa lengo la kutoa fedha kupitia ununuzi wa mafuta ya diesel lita 5500 na petrol lita 5500 na kuwaagiza walimu wakuu wachangie fedha za kupiga picha wanafunzi wa darasa la saba pamoja na fedha kwa ajili ya TSM 9 kwa maelekezo hayo ni kosa kwa sababu alikuwa akijua kuwa gharama za TSM 9 hugharamiwa na serikali kwa asilimia mia moja.
 
Amesema kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 12.47 zilipelekwa kwenye akaunti hiyo ya UWEKAMBI na ameitaja tuhuma nyingine kuwa ni kumdanganya mwajiri kuwa hakujakusanywa fedha yoyote kutoka kwa wazazi na hakuna fedha ya capitation iliyopelekwa kwenye akaunti hiyo ya UWEKAMBI.
 
Aidha mkurugenzi mtendaji amesema baada ya maamuzi hayo yaliyotolewa na baraza la madiwani hatua nyingine zinazohusishwa na mamlaka nyingine zikiwemo za kinidhamu zitafuata ingawa kwa sasa anapaswa kuyatumikia maamuzi yaliyotolewa na baraza hilo la madiwani.

HATIMAYE JOTI WA ORIGINAL COMEDY AMVISHA PETE MCHUMBA WAAKE WA SIKU NYINGI.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Saturday, January 10, 2015

MBUNGE WA MBEYA MJINI APATA AJARI MILIMA KITONGA IRINGA.


Mbunge wa mbeya mjini mr sugu akiwa na rafiki yake kando ya gari lao baada ya kupinduka katika mteremko wa kitonga leo.


Ajari hiyo imetokea mchana wa leo wakati gari hilo likiwa na watu wanne likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es salaam,na hakuna aliyepoteza maisha katika ajari hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan\ Mungi amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo japo amesema taarifa kamili itatolewa na askari polisi waliokwenda katika tukio hilo la ajari
 


MIMBA YAMTIBUA AUNT EZEKIEL.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Wednesday, January 7, 2015

Ngumi, mabomu uapishaji wenyeviti wa mitaa.


ENEO la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam, jana liligeuka uwanja wa mapambano baada ya polisi kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi ili kunusuru hafla ya kuapishwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Wilaya ya Kinondoni.

Dalili za kuibuka kwa fujo zilianza kuonekana kwa wananchi waliokuwa wamekusanyika nje ya hoteli ya Land Mark ambako hafla hiyo ilipangwa kufanyika, waliokuwa wakipinga kuapishwa kwa waliokuwa wagombea uenyekiti kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliodai walishindwa katika uchaguzi huo.

Wananchi hao ambao wengi wao wanatoka mitaa ya Msisiri ‘A’, Kawe Ukwamani, Kata ya Saranga, Kimara King’ong’o na Mtaa wa Temboni, Kata ya Msigani, walidai katika maeneo yao, wagombea wa CCM walipewa ushindi kinyume na matokeo halali.

Walidai kuwa katika uchaguzi huo, wagombea halali walioshinda wanatoka Chama cha Wananchi (CUF), lakini matokeo yalibadilishwa siku ya pili baada ya kutangazwa.
MABOMU NA RISASI

Katika tukio hilo, polisi walilazimika kupiga mabomu ya machozi na kurusha juu risasi za moto, huku wakiwataka wananchi kuondoka eneo hilo baada ya kuona fujo zinaweza kuwa kubwa.
Wakati risasi zikirushwa, wananchi hao walikuwa wakiimba kwa kutaja neno “Ukawa, Ukawa…” na wengine walikuwa wakisikika wakisema “zipigwe risasi nyingine” ndipo polisi walipoanza kupiga mabomu ya machozi.
Pamoja na mabomu kupigwa, wananchi waliamua kuhamia upande wa pili wa hoteli hiyo.
Hali ilikuwa ngumu katika geti la kuingia hotelini hapo ambapo muda wote lilionekana limezingirwa.


NDANI YA MTARO
Mambo yalibadilika zaidi, baada ya aliyekuwa mgombea kutoka Mtaa wa Msisiri ‘A’, Juma Mbena (CCM) kushindwa kuingia ndani, baada ya kuzuiwa na wananchi.

Inadaiwa katika mtaa huo, matokeo halali yalibadilishwa, licha ya kuonyesha mgombea wa CUF, Gasper Chambembe ni mshindi kwa kupata kura 497 dhidi ya 450 za Mbena.
Muda wote wananchi walikuwa wakimtaka Mbena kuondoka eneo hilo, huku wakimvuta shati lake hadi kuchanika wakidai si kiongozi wao halali.

Baada ya kuona amezidiwa, Mbena alikimbia na kwenda kujificha ndani ya mtaro wa maji machafu.
“Huyu kiongozi aliyekuja kuapishwa hapa tutahakikisha haingii kwa kuwa si chaguo letu, eneo letu alishinda mgombea wa CUF, tuliamka asubuhi lakini ilipofika saa 4 matokeo yalibadilishwa na ofisa mtendaji kwa kufutwafutwa kwa kalamu ya wino na kumpa ushindi mgombea wa CCM ambaye alishindwa katika uchaguzi,” alisema mmoja wa wananchi hao aliyefahamika kwa jina moja la Nassoro.

Wananchi kutoka eneo la Kawe Ukwamani walifika kwenye hoteli hiyo wakiwa na aliyekuwa mgombea wao wa uenyekiti, Nasri Mohamed (CUF), lakini alizuiwa kuingia ndani kwa kile kichodaiwa hakuwa na barua ya mwaliko kutoka Manispaa ya Kinondoni.

“Mimi nimeingia ndani nikatolewa, amebaki mwenzangu wa CCM ambaye katika uchaguzi ule nilimshinda,” alisema Mohamed.
Alisema katika uchaguzi huo alishinda kwa kupata kura 568 dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Suleiman Jeta aliyepata kura 560.
 MKURUGENZI WA MANISPAA
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mussa Nati, alisema wenyeviti 154 waliapishwa kati ya 191.
“Tumeapisha wenyeviti 154 kati ya 191. Kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo ugonjwa na dharura nyingine wengine wameshindwa kufika,” alisema Nati.

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya wananchi na kuhusishwa kuvuruga uchaguzi huo, alisema hana jibu kwakuwa alikuwa akipata majina ya washindi kutoka kwa watendaji wa mitaa na kata.
Wenyeviti hao waliapishwa na Mwanasheria wa Manispaa hiyo, Burton Mahenge.

KAMANDA WA POLISI
Akizungumzia vurugu hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura, alikiri kutokea na kusema hadi jana walikuwa wanashikilia watu saba.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Kinyaiya Shiriri, Fadhili Ally, Wilfred Ngowi, Stanley Hurio, Prisan Clement, Joseph Samki na Zito Fabiani.

Alisema wanaendelea kuwahoji na uchunguzi utakapokamilika jalada lao litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili sheria ichukue mkondo wake.

VPL: Matokeo ya Yanga vs Azam FC haya hapa.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

BREAKING NEWS: Kashfa ya Escrow yamng’oa Chenge rasmi...atangaza kuachia nafasi ya uwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

WAKATI Watanzania wakisubiri hatima ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye Rais Jakaya Kikwete alisema anamuweka kiporo kutokana na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.

Bunge lililopita baada ya kujadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu miamala iliyofanyika kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, lilipitisha maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuazimia kuwajibishwa viongozi wa Serikali na wale wa kamati za Bunge walioonekana kuhusika katika kashfa hiyo.

Viongozi wa kamati ambao Bunge liliazimia wawajibishwe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco, Victor Mwambalaswa.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tulizipata jana, Chenge alitangaza kujiuzulu nafasi yake juzi baada ya kamati yake kukutana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
“Amejiuzulu jana (juzi), saa tano asubuhi wakati wa kikao cha Kamati ya Bajeti kilichokutana kwenye Ukumbi wa Mkwawa, ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam.
“Aliwaambia wajumbe kuwa hataki malumbano na wabunge na hataki msuguano wowote, nafasi yake kwa sasa inashikiliwa na Dk. Festus Limbu, ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa kamati,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel, alipotakiwa kuthibitisha suala hilo, alisema hayuko ofisini, hivyo hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya suala hilo.
Alisema kama Chenge mwenyewe amefikia uamuzi huo, atakuwa amempunguzia kazi Spika.

Joel alisema kujiuzulu kwake kutakuwa ni kutimiza maazimio ya Bunge jambo ambalo ni lazima litekelezwe.
Akifafanua juu ya kumpata mwenyekiti mpya wa kamati hiyo, Joel alisema mara baada ya wajumbe hao kukutana kama viongozi hawapo, jambo la kwanza ni kufanya uchaguzi.

Alisema Chenge alichaguliwa na Spika kuongoza kamati hiyo kwa kuwa ilikuwa ni kamati mpya na ambayo ni nyeti sana.
“Wajumbe wake ukiangalia wengi walitoka kwenye Kamati ya Kushauri Vyanzo Vipya vya Mapato, Spika aliomba kumchagua mtu ili apate mtu makini anayejua vyanzo vya mapato,” alisema.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alipoulizwa kama ofisi yake ina taarifa za kujiuzulu kwa Chenge, alisema yupo jimboni na hana taarifa hizo ila anachojua suala la kuwajibika kwa wenyeviti waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) juu ya kashfa ya Escrow ni la lazima na halihitaji mtu kuandika barua ya kujiuzulu.

“Hakuna kuandika barua ya kujiuzulu, yale ni maamuzi ya Bunge, kinachotakiwa ni kamati kukaa na kuchagua viongozi wengine,” alisema.
Ndugai akizungumza na gazeti hili mwanzoni mwa juma lililopita, alisema kamati ambazo viongozi wake walihusishwa na kashfa ya Tegeta Escrow, zitakapokutana jukumu la kwanza litakuwa ni kuchagua viongozi wapya kwani tayari chombo hicho kilishaazimia kuwawajibisha.

Katika kashfa ya Escrow, Chenge anadaiwa kupokea Sh bilioni 1.6, kutoka kwa James Rugamalira ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering iliyokuwa na asilimia 30 kwenye Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), inayodaiwa kuuzwa kinyemela kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP).

VPL: Matokeo ya Yanga vs Azam FC haya hapa.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Monday, December 22, 2014

ALICHO POST ZITTO KABWE, BAADA YA RAIS KUMWAJIBISHA WAZIRI ANNA TIBAIJUKA NA KUBAKIZA KIPORO.

Nimemsikiliza Mhe Rais. Ninachoweza kusema ni kwamba maazimio yale hayakuwa ya Zitto Kabwe, PAC, CAG au PCCB. Yalikuwa ni maamuzi ya Bunge zima. Bunge la vyama vyote kikiwamo chama cha Rais Kikwete yaani CCM. Sisi kama Bunge tulitoa maazimio yale kwa maridhiano, uzalendo na bila kutaka kumuonea mtu yeyote. Suala hili sasa naliacha kwa wananchi. Bunge limefanya kazi yake na Serikali ambayo ndiyo tulikuwa tunasubiri maamuzi yake imeamua hivyo. Wananchi wataamua wenyewe.

MDAHALO WA KATIBA WAFANYIKA LEO MWANZA.



UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

HAWA Ndo MAPROF BWANA!!!! PROF. TIBAIJUKA AOMBWA KUPISHA NAFASI, PROF MUHONGO AWEKWA KIPORO.

 Rais Dk. Jakaya Kikwete.

--Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Tibaijuka.

--Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Tibaijuka, tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.

--Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Fredreck Werema ameshajiuzulu na amesema amebeba dhamana hiyo pia kwa niaba ya waliojiuzulu.

--Kuhusu watu kuwawajibisha, bodi ya TANESCO bahati nzuri imemaliza muda wake na tumeanza mchakato wa bodi, na tutaipata siku chache zijazo. Katibu mkuu wa wizara ni mtumishi wa umma, hivyo kuna taratibu na nimeshaagiza zianze.

----Serikali iandae muswada wa sheria ulioleta TAKUKURU, ni wazo zuri, Mchakato wa kufanya mageuzi TAKUKURU tumeuanza tangu 2008. Sheria ya kwanza ya PCCB ilikua na makosa manne tu ya rushwa tukayaongeza mpaka 24.

--Kuhusu mabenki kuwekwa kama zinatakatisha fedha, pendekezo uchunguzi ufanyike ni pendekezo zuri na intelligence unit ndio watakaofatilia

--Rais aunde tume ya kijaji kuwachunguza majaji(Mujulizi na Luangisa), nimelipokea lakini utaratibu wa kisheria kushughulikia linatakiwa lianzie kwenye mahakama na sio linaanzia kwa rais au bunge. Mahakama inaporidhika amepoteza sifa, inaletwa kwa rais maana ndie anaeteua majaji. Lazima kushirikiana na muhumili wenyewe. Nilichosema tumwachie jaji mkuu na wakiridhika watakuja kwa raisi endapo wataridhika wahusika wamekosa sifa.

--Kamati za bunge kuwavua nyadhifa wenyeviti wa kamati za bunge tunaliachia bunge lenyewe

--TAKUKURU na jeshi la usalama vichukue hatua, nimeshaeleza hatua zinaendelea.

--Kuhusu uwazi wa mikataba na mapitio, tutafanya na lipo moja tutafanya kuhusu usiri wao wa biashara, kuweka wazi zinaweza kutumiwa na wapinzani wa kibiashara, hivyo tutaangalia namna ya kulifanya.

--Niwahakikishie mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira katika kutimiza maazimio ya bunge.
Kutaifisha mitambo ya IPTL, tunahimiza sekta binafsi kuwekeza, tunapotaifisha habari tunayopeleka si nzuri, sisi tuliotaifisha mwanzo siku hizi tunasema hatuna sera ya ujamaa hivyo waje kuwekeza. Watasema wale jamaa wamerudia tena wanataifisha. Mahakama imefanya maamuzi kwa IPTL, kwanza waibadili mitambo yao ibadili itumie gas badala ya mafuta, tukiyafatilia yanaweza kutufikisha mahali. Haya ya kutaifisha yananipa wasiwasi

--Maazimio ya bunge
Kwanza niseme serikali imayakubali na niwapongeze waheshimiwa wabunge. Nashukuru kamati ya bunge chini ya Zitto na Filikunjombe, watu wa upinzani kufanya yale maamuzi yao, kwamba CCM ni mafisadi. Ni kweli watu hawa wanatoka CCM ila sio kwamba CCM inaridhia. Ntashangaa mbunge kulipinga hili eti kisa tu yuko CCM, bunge wengi ni CCM, kama ni kweli walikuwa hawataki hakuna azimio lingepita? Na kuna baadhi ya wabunge wa CCM waliudhika na maovu haya, wenzetu wanatafuta sifa laini kwa jambo ambalo ni letu sote.

--VIP walipouza na kupata dola milioni 78, wamelipa kodi bilioni 38. Kulikua na tuhuma za rushwa katika mchakato mzima. Yamesemwa mengi na bado hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa walizozipata wazipeleke PCCB. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato wao. Kwa miamala, serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa mujibu wa taratibu, maaskofu na masheikh kupewa kitu hawatuhusu, mtumishi wa umma ana masharti ya kupokea fedha. Watahojiwa na PCCB. Hushtuki asubuhi akaunti ina bilioni 1.6, milioni 80 etc. Zimeanguka kutoka juu ya mti. Huo ndo utangulizi.

--Tulitaka kufanya uchunguzi sisi wenyewe na mamlaka zetu na taarifa zimeshakuja, tunazifanyia kazi. Kuna vitu vimetokea, kuna vilivyofanyika nje na taarifa hazikuja na sasa tunalaumiana, hivyo tunafanya uchunguzi na wote waliohusuka tunawahoji na mahakama kuu ipo kesi ya PAP kumiliki hisa za IPTL, ipo kesi ya uhalali wa PAP kupokea pesa za IPTL. Hatutaki kuwaingilia ila sisi tutafanya uchunguzi wetu kwa ajili ya taarifa zetu. Tuwe na uhakika hizi hisa zimeuzwa kwa bei gani, tunataka kujiridhisha kwa sababu ipo kodi ya serikali(capital gain) na inalipwa na alieuza na sio alieuziwa. Kodi hulipwa na aliepata na sio aliepoteza (Alienunua).

--Fedha zilizotoka imelipwa PAP, akitokea mtu ana madai, serikali mnaikinga vipi. Ingetokea mtu ana madai yoyote angepelekwa PAP kulingana na makubaliano. Kukawa kuna hoja kuwa hata PAP umiliki wake wa hisa 70% unatia mashaka kutoka Mechmar, lakini waliziuza kwanza kwa kampuni ya Uingereza ambayo yenyewe ndo ikaziuza PAP. Kampuni ilikua chini ya ufilisi na kwa mujibu wa taratibu huwezi kuuza ukiwa chini ya ufilisi, kwa mujibu wa taarifa sio kweli.

--Kwa upande wa kodi ya serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa alisema hakuna kodi iliyochelewa kulipwa. Mgogoro ni baina ya IPTL na TANESCO havyo uamuzi wa standard charted haukuweza kuingia, kwa vile haikuhusishwa, ilienda kuzuia maamuzi hayo.

--Kabla ya mzozo wa ukokotoaji TANESCO ilikuwa inailipa ITPL Moja kwa moja. Lakini hata ulipotokea mzozo bado IPTL haikuacha kupeleka madai na Tanesco haikuacha kulipa. Kuwepo kwa akaunti ya escrow haibadili mwenye fedha yake.

--Nilipokutana na mwanasheria mkuu, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala mahakama haikufanya makosa, na kuhusu ile hasara amesema hakuna hasara yyte iliyopatikana kwa sababu pesa imelipwa kwa mtu halali.

--Jambo moja ambalo ni bahati mbaya, ilijengeka dhana kuwa akaunti kufungwa ni jambo lililoanzishwa na maafisa wa serikali kwa manufaa yao binafsi.

--Na hata TANESCO alipewa ushauri huo huo, uamuzi ule umetiliwa shaka na kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni kwa sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu kunufaika binafsi. Mara kuna watu wameenda benki na kubeba pesa kwenye sandarusi, lumbesa na mengineyo.

--Mfilisi aliagizwa kuhamisha kwa PAP kutoka IPTL ikiwemo Akaunti ya Escrow, ilizua mjadala mkali. Wizara ya nishati ilimwandikia mwanasheria mkuu kuomba ushauri, Mwanasheria akasema lipeni, uamuzi uko sawa na hauna matatizo na benki kuu wakauliza maswali hayo hayo na majibu yakawa yaleyale. Kuzingatia ushauri huo akaunti ikafungwa na pesa kukabidhiwa PAP. Mjadala ukaendelea bunguni na kwenye mablogu.

--CAG aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu pesa walizolipa kwenye akaunti ya escrow kama pesa zao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya TANESCO(Asset). Mahakama kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na mahakama ikakubali.

--Kama katika fedha hizo ipo kodi ya serikali, kwa mujibu kulikua na kodi ya ongezeko la thamani ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini ulikua bilioni 21 na ushee, TRA imepeleka madai yake kwa PAP.

--Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya TANESCO yakakubali ya tozo kupunguzwa, kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za TANESCO ambazo lazima zirudi kwa kiasi kilichopunguzwa. Bahati mbaya miaka saba baadae halikuwa limefanyika.

--Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, mdhibiti wa hesabu alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL, Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikua wanalipa moja kwa moja lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke BoT.

--Akaunti ikafunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka tozo ya uwekezaji, zinahifadhiwa ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao lakini kabla ya hapo TANESCO walikua wanalipa moja kwa moja.

--Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.

--Kwa mujibu wa mkataba, TANESCO isipolipa inatozwa riba ya 2%, kwa mujibu wa taarifa akaunti ilikua na 202.9 bilioni na sio 309.7, hizi zilipaswa kuwepo endapo TANESCO ingelipa zote kwa wakati.

--Masharti ilikuwa kampuni ya IPTL itaendelea kupeleka madai yake TANESCO ya tozo ya uwekezaji na TANESCO itaendelea kulipa lakini yataenda escrow akaunti badala ya IPTL lakini ya umeme yaliendelea kwenda IPTL na ilifunguliwa 2006 na mpaka kesi kuamuliwa 2013 wakati IPTL inachukuliwa na PAP walikua hawajamalizana. (They decided to manage the crisis rather than resolve it)

--TANESCO na IPTL walikubaliana kuanzisha Akaunti ya Tegeta Escrow benki kuu na kuingia mkataba, wizara ya madini kwa niaba ya TANESCO na IPTL na benki kuu kama wakala.

--Rais Kikwete anaelezea kuhusu mgogoro kati ya Tanesco na IPTL mpaka kupelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya Escrow

--Aeleza kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa naye aliagizwa na serikali kufuatilia mihamala ya Escrow na kuchukua hatua stahiki.

--Aaanza kuelezea uamuzi wa Serikali kumtaka CAG kufanya uchunguzi kuhusu akaunti ya Escrow na taarifa kupelekwa bungeni.

--Asema amelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa wale wote waliochangia vurugu katika uchaguzi huo.

--Aelezea furaha yake kuhusu uamuzi wa Mhe. Wassira kuwachukulia hatua wote waliochangia kasoro za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwemo baadhi ya watendaji kufukuzwa kazi huku wengine wakishushwa vyeo.

--Aongelea kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

--Mhe Kikwete aanza kwa kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa zawadi ya ujenzi wa maabara pamoja na kumtakia heri kuhusu afya yake.

--Rais Kikwete ameanza kuongea na wazee wa Mkoa wa Dar katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo Watanzania wanataraji atoe mwongozo kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

MDAHALO WA KATIBA WAFANYIKA LEO MWANZA.



UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Saturday, December 20, 2014

MDAHALO WA KATIBA WAFANYIKA LEO MWANZA.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiwasili jioni ya leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini mwanza.

Umati wa watu waliojitokeza katika mdahalo wa Katiba katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini mwanza.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji msitaafu Joseph Sinde warioba amewahutubia wananchi jijini Mwanza kuhusiana na katiba inayopendekezwa na kuwashauri wananchi hao kuisoma kwa umakini kwanza kabla ya kuipigia kura kwani kuna baadhi ya vipengele vimentofolewa katika katiba hiyo.

Akizungumza  katika mdahalo maalum ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hotel ya Gold Crest Warioba amesema kuwa watanzania kwa pamoja wapige kura ya ndiyo kama yale waliyoyapendekeza yamo kwenye katiba na wapige kura ya hapana kutokana na kuwa yale waliyoya pendekeza hayapo katika katiba hiyo.

OFFICIAL VIDEO: ALIKIBA - MWANA.



UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Tuesday, December 16, 2014

Breaking news!! MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, JAJI WEREMA AJIUZULU.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema (pichani) leo amejiuzulu nafasi yake na tayari amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Kikwete.

Rais Kikwete asema amepokea barua yake na kumshukuru kwa ushirikiano aliouonyesha katika kipindi cha utumishi wake.

Sababu ya kujiuzulu ni kwamba ushauri alioutoa kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka vizuri.

UPDATES ZA MATOKEO MIKOA MBALIMBALI YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA YALIYOKWISHA TANGAZWA HADI SASA.



UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

UPDATES ZA MATOKEO MIKOA MBALIMBALI YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA YALIYOKWISHA TANGAZWA HADI SASA.

 Mbozi; Mtaa Masaki: CHADEMA 99, CCM 44

Kigoma Mjini; Mtaa wa Gezaulole: CHADEMA 240, CCM 198

Ukonga- Mtaa wa Kivule Majohe: CHADEMA 231, CCM 77

Musoma Vijijini- Kijiji cha Muhoji: CHADEMA 197, CCM 464

Ubungo- Mtaa wa Msewe: CHADEMA 683, CCM 356

Kinondoni- Mwenge Nzasa: CHADEMA 344, CCM 318

Tarime Forodhani boda (kitongoji): CHADEMA 289, CCM 90

Tarime Forodhani Kijiji: CHADEMA 312, CCM 99

Monduli Mto wa Mbu Kijiji Jangwani: CHADEMA 147, CCM 124

Mwanga Kitongoji Mgagao: CHADEMA 56, CCM 32

Rorya- Mtaa Ngasaro: CHADEMA 480, CCM 360

Arumeru Mash. Mtaa wa Manyata: CHADEMA 168, CCM 91

Ubungo- Mbezi Yusuph: CHADEMA 190, CCM 163

Mwanga- Mtaa Mtahang’a: CHADEMA 116, CCM 73

Ilemela- Mtaa wa Pasiansi: CHADEMA 689, CCM 247

Karatu- Mtaa Mazingira: CHADEMA 290, CCM 130

Karatu Mtaa wa Maliasili: CHADEMA 240, CCM 77

Karatu- Mtaa wa Manyara: CHADEMA 220, CCM 170

Tarime Mtaa wa Bugosi: CHADEMA 438, CCM 138

Tarime Mtaa wa Regoryo: CHADEMA 191, CCM 75

Segerea Mtaa wa Migombani: CHADEMA 547, CCM 225

Mamlaka ya Mji mdogo Shirati-Rorya ina mitaa 9: CHADEMA mitaa 7, CCM mitaa 2

Mererani mitaa 8: CHADEMA mitaa 7, CCM mtaa 1

Magu Mjini: CHADEMA mitaa 10, CCM mitaa 7

Manispaa ya Bukoba: Mitaa 66 ndani ya Manispaa ya Bukoba, CCM wamepata mitaa 35 huku upinzani ukijinyakulia mitaa 31.

Jumla ya Wajumbe 330 walitakiwa ambapo wapinzani wamepata WAJUMBE 205 dhidi ya CCM waliopata WAJUMBE 125.

Wilayani Karagwe: Wilaya ina jumla ya mitaa/vijiji 18, Upinzani wamejinyakulia vijiji/mitaa 12 huku CCM wakipata vijiji/mitaa 6

Wilaya ya Nachingwea: Kitongoji cha Raha Leo, CCM 60 na Chadema 59.
Kitongoji cha Amani: CCM 35 na CDM 9.

Kijiji cha Mnyune: CCM 207 na CDM 20.

Monduli Magharibi: CDM 76, CCM 199.

Monduli Mjini Mashariki: CDM 57, CCM 88 na Mtaa wa Sabasaba CDM 84, CCM 172.

Kitongoji cha Mandela, Kata ya Mkalama: CCM imeshinda kwa kura 240 na CDM 196.

Kitongoji cha Kichangani Kata ya Gairo Mjini: CCM 260, CDM 115 zilozoharibika 2.

Wilaya ya Kyela: Orodha ya Vitongoji na chama kilichoshinda
Butiama- CHADEMA
Kyela kati -CHADEMA
Roma -CHADEMA
Mikoroshoni -CCM
Mbugani -CHADEMA
Nazareti -CHADEMA
Unyakyusa -CCM
Kapwil- CCM
Itunge mashariki -CCM
KEIFO -CCM
OROFEA -CHADEMA
SAMA B -CCM
Mikumi -CHADEMA
Mwaikambo -CHADEMA
Kilasil- CCM
Mkombozi -CHADEMA
Bondeni A-CCM
Bondeni B-CHADEMA
Itunge-Mundekesye CHADEMA

Tarime; Mtaa wa Bhughucha: CHADEMA 135, CCM 123

Tarime; Mtaa wa Buhemba: CHADEMA 104, CCM 50

Tarime; Nyarusahi: CHADEMA 197, CCM 54

Tarime; National: CHADEMA 170, CCM 130

Tarime; Kijiji Nyabitocho: CHADEMA 899, CCM 315

Segerea; Migombani: CHADEMA 547, CCM 225

Huko Mvomero hadi sasa kati ya Vijiji 20 vya awali

CHADEMA Vijiji 15
CCM Vijiji 5

Vijiji hivyo 15 ni; Sarawe, Lungo, Kidudwe (nyumbani kwao mbunge wa Mvomero), Mndelwa, Masili, Ndugutu, Lukunguni, Mwalavi, Mvomero, Bumu, Madizini, Doma, Mlali, Tchenzema na Nanyinga (nyumbani kwa Mwenyekiti wa Halmashauri- CCM).

VURUGU SIMIYU: Watu 600 wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Chadema wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Simiyu wakihusishwa na vurugu za uchaguzi wa serikali za mitaa jana.

Kabla ya kukamatwa hapo jana kati ya saa 2 – 3 asubuhi, polisi walilazimika kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema kwa mabomu ya machozi walipokuwa wakipinga uchaguzi kufanyika leo badala ya kufanyika jana kama ilivyopangwa.

Kutokana na kulipuliwa mabomu ya machozi, huduma za usafiri wa mabasi kutoka na kuelekea Mwanza, Musoma, Bunda, Tarime, Simiyu zilisimama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alipopigiwa simu kutoa kauli kuhusu sakata hilo, hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu.

Takwimu uchaguzi: Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa ya Takwimu ya mambo yaliyotokea wakati wa kampeni za Uchaguzi Serilali za Mitaa.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Mkoa wa Tabora unaongoza kwa ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi ukifuatiwa na Kagera wakati Shinyanga na Mbeya wakifanya vizuri.

Kwa upande mwingine takwimu zinaonyesha kuwa kukosekana kwa mwamko wa kisiasa 19%, kampeni kuisha baada ya muda 18%, ratiba za kampeni kuwa wazi 12%, rushwa kwa wapiga kura10%, huku kampeni kuzuiwa na mamlaka 1% na vitisho kutoka kwa watu wasio vyombo vya dola 1%.

Mgombea Chadema atumbukia shimoni, afariki: Aliyekuwa mgombea ujumbe katika Kituo cha Msalala Road, Geita kupitia Chadema, Bethar Nchimani Ngosha amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo lililokuwa limejaa maji.

Baada ya kutangaziwa kuwa ameshinda, marehemu alikuwa anaelekea uani, karibu na choo kulikuwa na shimo la choo lililokuwa wazi ndipo alipodumbukia na mauti kumpata.

Akataa kusaini: Mtaa wa Katoma Geita Mjini wananchi wamekesha kusubiri matokeo.Mgombea wa CCM ameshindwa na amekataa kusaini matokeo.

Mabomu yatumika: Jeshi la Polisi limeamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi mkoani Mwanza katika maeneo ya Pasians, Mji Mwema, Kirumba, Ibungiro na Kitangiri baada ya vurugu wakati wa kusubiri kutangazwa matokeo.

Kijiji cha Muungano Kata ya Chahwa mkoani Dodoma: CHADEMA 196, ADC 38

Mbozi; Mtaa wa Masaki: CHADEMA 99, CCM 44

Kigoma Mjini; Mtaa wa Gezaulole: CHADEMA 240, CCM 198

Ukonga; Mtaa wa Kivule Majohe: CHADEMA 231, CCM 77

Musoma Vijijini; Kijiji cha Muhoji: CHADEMA 197, CCM 464

Ubungo; Mtaa wa Msewe: CHADEMA 683, CCM 356

Kinondoni; Mwenge Nzasa: CHADEMA 344, CCM 318

Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35

Mererani: CHADEMA imeshinda mitaa 7 kati ya 8

Kitongoji cha Endulele: CHADEMA 170, CCM 130

Monduli; Kitongoji Kambi ya Mkaa: CHADEMA 27, CCM 13

Mwanga Mtaa wa Lwami: CHADEMA 55, CCM 35

Arumeru Magharibi, Kitongoji Endulele: CHADEMA 170, CCM 130

Ushirombo Mjini: CHADEMA inaongoza vitongoji 10, CCM inaongoza vitongoji 4

Moshi Manispaa, Kitongoji Longuo A: CHADEMA 206, CCM 66

Mbozi Mtaa wa Mbugani: CHADEMA 227, CCM 160

Kata ya Mji Mpya, Morogoro yenye mitaa 12, CCM imeshinda mitaa 9, CHADEMA wakishinda mtaa 1 huku mitaa miwili mpaka sasa bado vurugu zimetanda baada ya kura kudaiwa kuzidi huku watu kadhaa wakituhumiwa kupiga kura mara mbili.

Kagondo, Kata ya Muhutwe, Kagera: CHADEMA imeshinda mitaa 4 kati ya 5

Kufungwa Vituo: Katika maeneo mengi vituo vya upigaji kura tayari vimefungwa huku wananchi wakisubiri kwa hamu kujua matokeo.

Uchaguzi Migombani: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa eneo la Migombani, Segerea jijini Dar umeingia dosari baada ya Afisa Mtendaji Kata ya Segerea kutangaza kusitisha uchaguzi huo kimyakimya bila sababu za msingi ambapo wananchi waliamua kumweka mtu kati mpaka akaruhusu uchaguzi huo kuendelea kwa maandishi. Akijitetea afisa huyo alidai kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala kufanya hivyo.

Mazimbu, Morogoro: Eneo la Mazimbu, Moro kimenuka mpaka wanajeshi wamelazimika kuingilia kati kutuliza ghasia wakati wa zoezi la upigaji kura.

Kawe, Dar: Uchaguzi wadaiwa kuingia dosari baada ya mgombea wa CCM kutoa amri ya vitabu kufungwa kabla ya muda ulipangwa.

Kigogo, Dar: Mgogoro umezuka katika Kituo cha uchaguzi Kigogo jijini Dar baada ya wananchi kudai kuwa baadhi ya watu wamepelekwa kama mamluki eneo hilo kwa ajili ya kugipa kura.

Sokoine-Kibaoni, Morogoro: Wananchi eneo la Sokoine-Kibaoni, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mpaka sasa bado hawajaanza kupiga kura mbali na wengi wao kujitokeza huku wengine wakiwa wamekodi magari kutoka Bwawa la Kihonda umbali wa kilomita 20 kwenda kupiga kura lakini mpaka sasa bado hawajapiga kura.

Amana, Ilala: Baadhi ya wananchi wameamua kususia zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Amana, Ilala jijini Dar baada ya mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Amama aitwaye Mathias Ijumba kuondolewa katika uchaguzi dakika za mwisho kwa kile kinachodaiwa kuwa si mkazi wa eneo hilo lakini jambo la ajabu jina like liko katika orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura na mgombea huyo ameruhusiwa kupiga kura yake.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai jamaa huyo anakubalika sana na huenda ndiyo chanzo cha jina lake kuondolewa.

Dar es Salaam: Wananchi katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.

Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.

Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.

MCHINA AMLA MATE DADA WA KIBONGO MBELE ZA WATU.



UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Thursday, December 11, 2014

UNAAMBIWA VIP ya Rugemalira Yadai Maamuzi ya Bunge Kuhusu Sakata la Escrow ni ya Kipuuzi.

Wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajia kutoa maamuzi juu ya kashfa ya uchotaji wa fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo, Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, imedai maamuzi ya Bunge yaliyopendekezwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ni ya kipuuzi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana yenye kurasa 19 na orodha ya vielelezo 17, Katibu wa kampuni hiyo, Respicius Didace, alisema VIP inatuhumiwa kimakosa kwamba imefanya vitendo vya uvunjifu wa sheria kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.

“Tuhuma hizi ni upuuzi kwa sababu VIP ililipwa kwa msingi wa Mkataba wa Uuzaji wa Hisa uliotangazwa na kuridhiwa kwa amri ya Mahakama ya Septemba 5, 2013; na kufuatiwa na amri ya mahakama ya Januari 17, 2014 iliyotolewa katika shauri la wazi; na baada ya kuwa imefanya malipo ya Sh. za Tanzania bilioni 38 (sawa na dola za Marekani milioni 23.6) katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kugharimia malipo yote ya kodi ya VIP,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ambayo pia imeishambulia Benki ya Standard Chartered (SCB) kama chimbuko la vurugu zote kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow.

Didace alisema VIP si mshirika katika mkataba wa akaunti ya Tegeta Escrow na haikuwa na jukumu lolote lile katika uanzishwaji wake na ulipwaji wa fedha kutoka katika akaunti hiyo na siyo mwanahisa tena wa IPTL.

Didace alisema hoja zilizotolewa na PAC wakati wa mjadala bungeni kwamba fedha zilizopo katika akaunti ya Escrow ni za Serikali siyo sahihi kwani haikusema wazi ni sehemu gani ya fedha hizo ni mali ya umma na kwa misingi gani.

“ Huo si msingi wenye mashiko wa kuwatuhumu watu kwamba wameiba fedha za umma, VIP ina uelewa mpana na wa kina wa historia ya IPTL na msingi wake wa kisheria na imegundua kwamba taarifa nyingi na tuhuma kuhusu VIP, IPTL na Akaunti ya Escrow   zinafanana kwa kutokuwa sahihi,” alisema.

Alisema VIP inaamini kwamba umma na Bunge la Tanzania wamedanganywa kwa kuaminishwa tuhuma zisizokuwa za kweli ambazo zitafaidisha malengo ya kigeni na kuwafakarisha Watanzania.

Aliongeza kuwa Bunge na PAC zimedharau masuala ya msingi na kushupalia masuala yasiyokuwa na tija kwa taifa na kwamba mapambano haya yamekuwa na mafanikio na hii ndiyo sababu SCB imesababisha mkanganyiko kwa kuwalisha Watanzania taarifa za uongo.

Didace alisema PAC imetoa tuhuma nzito za uvunjifu wa taratibu au jinai dhidi ya watu kadhaa bila ya kutoa ushahidi au sababu: “Hiki ni kiwango cha juu cha kutokuwajibika na ambalo limefanyika kwa maslahi ya muda mfupi ya kisiasa.”

“Ni kiwango cha juu cha kukosa uwajibikaji kwa sababu PAC haiwezi kutoa haki ambazo mahakama ya kisheria lazima itoe kwa watu binafsi wakati wakitoa maamuzi kuhusu migogoro yao,” imeeleza taaifa hiyo.

Alisema hakuna mahitimisho yoyote ya kisiasa yanayoweza kupewa fursa ya kuathiri mwenendo wa utoaji wa haki na mwenendo mzima wa kisheria wa pande zote za ndani ya Tanzania na nchi za nchi ikiwa ni pamoja na kwa VIP.

“Mihimili ya mahakama na watendaji wa serikali wasikimbilie katika kuhukumu na badala yake waheshimu uhuru, mamlaka ya kisheria na madaraka ya muhimili wa mahakama, ambao ndio nguzo za utawala wa sheria katika nchi yoyote ile ya kidemokrasia kama Tanzania,”imeeleza taarifa hiyo.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, wabunge walitoa maazimio manane kuhusu sakata la Escrow likiwamo la kutenguliwa kwa nyadhifa za Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema.

Wengine waliopendekezwa kuvuliwa yadhifa zao ni wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge hilo, William Ngeleja (Sheria, Katiba na Utawala), Andrew Chenge (Bajeti) na Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini).

Pia wamo  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Viongozi wa umma na maofisa wa ngazi za juu serikalini wanapaswa kuwajibika kwa sababu wamehusishwa na vitendo vya kijinai katika sakata hilo linalohusisha kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL).

Kadhalika, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, vimetakiwa kufanya uchunguzi dhidi ya wote waliotajwa kuhusika na sakata hilo na kupendekeza  watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua.

Maazimio mengine ni kumtaka Rais kuunda Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya majaji kuhusishwa  kwenye kashfa hiyo.

Majaji waliotakiwa kuchunguzwa ni Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Prof. Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Aidha, Bunge lilitaka mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi kuitaja Stanbic Bank Tanzania Ltd na benki nyingine yoyote itakayogundulika baada ya uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika akaunti ya Escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu.

Pia, Serikali iandae na kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria iliyounda Takukuru kwa lengo la kuanzisha taasisi mahususi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi  na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo.

Serikali imetakiwa kutekeleza azimio la Bunge kuhusu mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya Tanesco na kampuni binafsi ya kufua umeme na hivyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapitio ya mikataba ya umeme kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti.

BILIONEA NIGERIA AMZAWADIA TAYO $ 350,000 BAADA YA KUKOSA ZA BIG BROTHER HOTSHOTS.


UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

habari kamili :: read more...

Thursday, December 4, 2014

Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth Singh atema Cheche.

 Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth Singh.

Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth Singh amesema anafikiria mara mbilimbili iwapo aendelee kuwekeza nchini au la, baada ya kuwapo kwa tuhuma kwamba alihusika na uchotaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Nimeongelewa sana kiasi kwamba naona kama hakuna hata amani ya kuwekeza Tanzania, nitajifikiria mara mbili mbili. Wananchi wanaelewa vingine kabisa kuhusu suala hili kwa sababu ya upotoshwaji,” alisema Singh alipozungumza na gazeti hili jana.
Singh ambaye alituhumiwa kujipatia asilimia 70 ya hisa katika Kampuni ya IPTL isivyo halali, alisema hafikirii kuwekeza zaidi nchini kwa sababu yamekuwapo maneno mengi na shutuma zisizo na ukweli zilizoelekezwa kwake kuhusu sakata hilo.

Kauli ya bosi huyo wa IPTL imekuja wakati Taifa likisubiri utekelezaji wa maazimio ya Bunge na akiwa mmojawapo wa watu wanaotakiwa kuchunguzwa na vyombo vya dola ili akibainika kufanya makosa, afikishwe mahakamani.

Jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza haraka maazimio manane yaliyotolewa na Bunge dhidi ya ufisadi wa sakata la escrow.
“Rais hatakiwi kukaa kimya, atoe tamko la haraka ili kuwaondoa viongozi hao. Hata Waziri Mkuu anatakiwa kuwajibishwa kwa sababu ni chanzo cha udhaifu huo,” alisema Profesa Lipumba alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CUF (JUKECUF).
Jana, Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema alisema: “Kwangu ni kama hukumu imetangulia mashtaka kwa sababu sikuwahi kuitwa kuhojiwa mahali popote, ila ninauheshimu uamuzi wa Bunge.”
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema hayuko tayari kuzungumzia masuala ya kashfa ya Akaunti ya Escrow pamoja na mwingiliano wa mihimili miwili, Bunge na Mahakama kwa kuwa siyo wakati wake.
Wakati hayo yakiendelea, uongozi wa Benki ya Stanbic Tanzania nao ulitoa taarifa ya kukana kuhusika katika utakatishaji fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya Bunge kupitisha azimio la kuitaka mamlaka husika za kifedha kuichunguza.
Malamiko ya Singh
Singh alisema kampuni yake imekuwa ikiuza umeme kwa bei nafuu; senti nane kuliko kampuni nyingine, lakini bado anaonekana kuwa na makosa.

“Kuuza umeme kwa senti nane kwa megawati ni bei nafuu sana lakini mbona naonekana kama nina makosa? Ndiyo maana ninasema nitafikiria mara mbili kuwauzia umeme,” alisema.
Alisema kampuni nyingine za kufua umeme zinauza umeme mara mbili ya bei kuliko yake, lakini bado anaonekana si mwekezaji mzuri huku mazuri yote aliyoyafanya nchini yakisahauliwa.
Alisema anashangazwa na kauli za wabunge na baadhi ya wanasiasa kuwa anatakiwa kukamatwa kwa kukwepa kodi na kujipatia fedha isivyo halali na kusema haoni kosa alilolifanya mpaka sasa.
“Wanikamate kwa lipi? Hata kutaifisha mali zangu au mitambo hawawezi kabisa hiyo ni kazi ya Mahakama,” alisema.
Alisema wanaomtuhumu kuwa kaiba fedha za umma hawana hoja na kwamba kama ingekuwa kweli, waliotakiwa kulalamika ni mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira na raia wa Malaysia, aliyemtaja kwa jina moja la Barbin... “Wenyewe wahusika hawajasema kama wameibiwa lakini leo naambiwa na Bunge nimeiba na wanataka kutaifisha mali zangu inashangaza sana.”

Alisema ameshangazwa na jinsi Bunge lilivyomhukumu bila kupewa nafasi ya kujitetea... “Wao wanajadili bungeni, Mahakama haijatoa hukumu lakini wanamhukumu mtu ambaye hayupo hapo, hawajasikia utetezi wake. Inashangaza sana, kwa nini Mahakama isifanyie kazi suala hili na kutoa hukumu?”
Kuhusu utata wa uraia wake, Singh alisema hakuna ukweli wowote kuwa yeye ni Mkenya au wa Afrika Kusini na kusisitiza kuwa ni Mtanzania, mzaliwa wa Iringa. “Mimi ni Mtanzania, unafikiri mimi Mhindi?” alihoji Singh.
Kauli ya Ngeleja
Kwa upande wake, Ngeleja naye alilalamikia kutohojiwa na kusema: “Siwezi kufahamu kwa nini sikuitwa kuhojiwa maana hata maaskofu nimesikia kwenye vyombo vya habari kwamba nao wanalalamika hawakuhojiwa, pengine inawezekana muda ulikuwa mfupi, hilo sifahamu.”
Ngeleja ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini kabla ya kung’olewa katika nafasi hiyo alisema katika mazingira ya sasa hawezi kuzungumzia fedha zinazodaiwa kuingizwa katika akaunti yake, hadi pale wenye mamlaka zitakapotekeleza maazimio ya Bunge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko alisema anasubiri uchunguzi ufanyike ili kubaini ukweli juu ya kuhusishwa na mgawo wa Sh40.4 milioni zilizochotwa kutoka akaunti hiyo.

“Unataka nizungumze nini sasa? Taarifa zimesomwa na kutangazwa, tusubiri huo uchunguzi unaotakiwa kufanyika,” alisema.

Jaji Mkuu agoma
Akizungumza baada ya mkutano wa viongozi wa Mahakama na vyombo vya habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Jaji Mkuu Chande alisema: “Mambo hayo yameshajadiliwa na hapa tulipo si mahala pake.”

Aliombwa kutoa kauli yake kuhusu baadhi ya majaji kuhusishwa na kashfa ya hiyo na kile kilichoelezwa kuwa kuingiliana kwa mihimili ya Bunge na Mahakama katika kushughulikia suala hilo.

Hata hivyo, mmoja wa maofisa wa Mahakama aliyekuwapo eneo hilo, alisema suala majaji wanaotuhumiwa linanasubiri kuundwa kwa tume ya kijaji kama ilivyoelekezwa na Bunge.

Majaji hao waliotajwa ni Aloysius Mujulizi na Profesa Eudes Ruhangisa ambao wanadaiwa kuhamishiwa fedha kutoka kwa akaunti ya mmojawapo wa watuhumiwa iliyopo Benki ya Mkombozi. Hadi sasa majaji hao hawajatoa maelezo yoyote kuhusu suala hilo.
Stanbic yakana
Benki ya Stanbic jana ilitoa taarifa kwa umma ikisema haihusiki na sakata hilo na kwamba imekuwa ikifuata sheria na kanuni za kifedha katika utendaji wake.

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba Benki ya Stanbic siku zote inafuata masharti yote na pamoja na sheria za maadili zilizowekwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” ilisema taarifa hiyo.

Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki ilishatoa taarifa ikikanusha kuhusika kutakatisha fedha chafu.
“Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kutoyumbishwa na tuhuma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu,” ilisema taarifa hiyo.

Msemaji wa BoT, Lwaga Mwambane alisema tuhuma dhidi ya benki hizo zinafanyiwa kazi na Kitengo cha Intelijensia ya Fedha (FIU) kilichopo chini ya Wizara ya Fedha.
Masele ajigamba

Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele amejigamba kuwa tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwake kuhusu sakata hilo ni kama kumpiga chura teke na kumwongezea mwendo.
Akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Serikali za Mitaa mjini Shinyanga juzi, Masele alisema aliokolewa kutoka kwenye mto uliojaa mamba na kusema wabaya wake walijua tayari wamemwangamiza na kwamba kupona kwake kumempa nguvu ya kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko katika jimbo lake la Msalala.
chanzo:gazeti la mwananchi

LAVEDA ARUDI BIG BROTHER AFRICA -BBA.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Tuesday, December 2, 2014

Rais Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi waziri wa usalama Joseph Ole Lenku mara moja na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Nkaiseri.

Rais Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi waziri wa usalama Joseph Ole Lenku na kumpendekeza waziri mpya wa usalama Joseph Nkaiseri kuchukua nafasi hio.

Wakati huohuo mkuu wa polisi nchini Kenya inspekta generali David Kimaiyo amejiuzulu kutokana na shinikizo dhidi yake afanye hivyo kwa kushindwa kukabiliana na utovu wa usalama nchini.
Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bwana Kimaiyo alikubali 'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
 Rais alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.

Aliyekuwa mkuu wa polisi David Kimaiyo
Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake.
Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.

Hatua ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini.

Uteuzi wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.

Alipokuwa anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza mda wa vikao vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili wamuidhinishe.

Ferguson Shooting: Officer Wilson Quits Police Force after receiving Death Threats.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

PICHA MBALIMBALI ZA RAIS KIKWETE AKIMWAPISHA CAG MPYA, PROF MUSA JUMA ASSAD IKULU JIJINI DAR.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitia sahihi yake kwenye nyaraka baada ya kumuapisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad nyaraka baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaa  Novemba 02, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuangalia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad akiweka sahihi yake kwenye nyaraka baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na CAG Mstaafu Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 02, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Spika Anne makinda na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 02, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na wafanyakazi wa ofisi ya CAG  Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na familia ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 02, 2014.

JISOMEE MWENYEWE HAPA VIZURI NA TARATIBU RIPOT YA TEGETA ESCROW....YOU CAN'T BELIEVE ON Y's EYE HUYU NAE KAPEWA MGAO.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top