Friday, January 17, 2014

Picha na Stori nzima jinsi Baby Madaha alivyonasa Mtego wa Kujiuuza.



Kumekuwa na skendo kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo hujihusisha na biashara ya kujiuza ili kujipatia kipato na kufanya sanaa kuwa kama chambo cha kunasa wanaume.
OFM MZIGONI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, mwaka jana ilinasa mastaa wawili kwenye mtego wake, mke wa mtu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ na Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Mwaka huu, OFM imeanza kazi zake ambapo kwa kuanzia iliamua kumtega Baby Madaha aliyejaa kwenye kumi na nane zake.
Mmoja wa wadau wa OFM alijifanya mfanyabiashara kutoka Mwanza ambaye ni mgeni wa jiji a.k.a Ngosha akijipachika jina la Frank ambapo baadaye katika mazungumzo, Baby Madaha alimbana na kutaka ampatie majina matatu ndipo mwana-OFM Frank (feki) akajipatia jina Frank Michael Lugwisha.
 

ILIKUWAJE?
Mchezo mzima ulianza Januari 13, mwaka majira ya saa 11:52 jioni kwa kuchati kwenye simu ya kiganjani ambapo Baby Madaha aliingia kichwakichwa bila kujua anachati na ‘sumu’ wa OFM kama ifuatavyo;
Frank/OFM: Mambo vipi Baby Madaha? Nilikuwa naomba tuonane.
Baby Madaha: Kuhusu nini?
Frank/OFM: Niwe mkweli, Madaha nimekupenda, nilipofika hapa Dar ndo nikaona nikutafute.
Baby Madaha: Unampendaje mtu usiyemjua?
Frank/OFM: Jamani nakuonaga magazetini na video zako.
Baby Madaha: Safi, so unataka kuniambia nini ambacho sijakisikia?
 Frank/OFM:  Nataka tu-meet (kukutana) Madaha nimetokea kukupenda sana lakini Alhamisi (jana) narudi mkoani Mwanza.

Baby Madaha: Huwezi ku-manage kuwa na mimi, baki kuwa shabiki wangu tu.
Frank/OFM: N’take radhi Madaha, kwa nini nisiweze, kikubwa kipi?
Baby Madaha: Huh! Tuma vocha tuone how worth are you? (Tuma vocha tuone utajiri wako)
Frank/OFM: Acha utani bwana, vocha kitu gani, ongea mambo makubwa Madaha
Baby Madaha: Hahaha…yote ninayo-except vocha tajiri.
Frank/OFM: Acha bwana. Vocha ndo kikwazo kwako?
Baby Madaha: Yap! Kama hutaki acha au unadhani natumia wireless kuchati na wewe?
Frank/OFM: Madaha wewe ni mkatili kiasi hicho?
MAMBO YASIMAMA KWA MUDA
Masuala ya kuchati yalisimama kwa muda lakini ilipofika saa 2:22 usiku, mazungumzo yaliendelea ambapo siku iliyofuata Frank wa OFM aliamua kuendelea kumtengenezea mtego ili kujiridhisha kama ni kweli baadhi ya mastaa wa Bongo wanafanya biashara hiyo haramu.
Januari 14, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi, Frank wa OFM alianza tena kuchati na Baby Madaha kama ifuatavyo;
 
Frank/OFM: Mambo Madaha? Mi Frank
(akaamua kumpigia simu Frank wa OFM, ilikuwa mshtuko kwa Frank kwa sababu hakujipanga kuongea naye kwa hiyo hakupokea simu ya Baby Madaha ambayo ilipigwa saa 6: 30 mchana.
Dakika moja baadaye, Baby Madaha alituma meseji ya kumtoa hofu Frank wa OFM;
Baby Madaha: Frank ‘am calling you in vain uh afraiding of me (Frank nakupigia kwa nia njema unaniogopa?)
Frank/OFM: Sorry nilikuwa tight, naweza kupiga?
Baby Madaha: Yap!
Frank/OFM: Frank wa OFM aliongea na Baby Madaha na kuanza kumchomekea ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha na kuonesha nia ya kujenga uhusiano huku akimtaka staa huyo kuwa ‘siriaz’ akimuahidi kuwa atakuwa naye na kuwa ajenti wake wa muvi jijini Mwanza.
Baada ya maongezi ya kutongozana kwenye simu, Frank wa OFM alimtumia tena meseji Baby Madaha kama ifuatavyo;
 
Frank/OFM: Nimefurahi sana kuongea nawe, sijui itakuwaje tukionana?
Baby Madaha: Wait, you I’ll see.
Frank/OFM: Eti ee, nimetokea kukupenda sana.
Baby Madaha: Thanks.
Baada ya hapo Frank wa OFM alimaliza kumtumia ‘sms’ siku hiyo, ilikuwa saa 9:12 alasiri.
Hata hivyo, Frank wa OFM aliamua kumhoji zaidi kupitia sms akitaka kujua hasa akiwa naye hata kwa saa tatu atataka shilingi ngapi?
Frank/OFM: Sasa hivi nataka kutoka niende ATM kuchukua pesa, sasa hebu kuwa muwazi tu wangu, kuwa na wewe kwa kama saa tatu utakuwa poa nikupe Sh. ngapi? Mtu mzima nisije nikaumbuka si unajua tena kwa staa kama wewe?
Baby Madaha: Milioni 10!
Frank/OFM: Baby usinikomoe, mimi na wewe tuna safari ndefu, kila nikija Dar tutakuwa pamoja.
Baby Madaha: (...anapiga simu lakini Frank wa OFM hapokei).
Baada ya kuona hivyo, Baby Madaha alituma sms hii “Call” (piga).
 
MAONGEZI YA SIMU
Frank/OFM: Mambo vipi Baby, habari za muda tena?
Baby Madaha: Salama tu, kwani wewe ulikuwa unataka kutoa sh. ngapi ATM?
Frank/OFM: Mimi ndiyo nilikuwa njiani naelekea ATM natoka hapa hotelini nilipofikia nina Shilingi Mil.4 kwa usiku mmoja, hapo vipi?
Baby Madaha: Katoe 5 fresh, sasa benki gani utaenda kutoa wakati benki zote zimeshafungwa na ATM mwisho kutoa ni Mil.1, sasa hapo itakuwaje?
Frank/OFM: Nitatoa kwa ATM, hata hivyo, nina master-card, naweza kutoa Mil.1 hadi mara 5, usijali kwani pesa kitu gani, cha msingi mimi ni kuwa na wewe!
Baby Madaha: Okay, fine unaweza kuja Kijitonyama (Dar) hapa kwenye hoteli ya (anaitaja jina)?
Frank/OFM: Nimefikia hapa hotelini (jina kapuni), sasa kutoka ni vigumu.
Baby Madaha: Okay, poa nitakuja hapo hotelini saa 1:00 usiku.
Frank/OFM: Usijali karibu sana, nakupenda sana Baby Madaha yaani niko tayari kwa lolote, sema unataka nikupe nini?
Baby Madaha: Hahaha....(anachekaaa) nikija nitakwambia vyote ninavyotaka kwani unafanya biashara gani?
 
Frank/OFM: Nauza nguo, mara nyingi nafuata Jakarta, Indonesia mara kwa mara lakini natumia muda mwingi kufanya kazi zangu Mwanza.
Baby Madaha: Wee Msukuma eti? Mimi mwenyewe Msukuma kwani unadhani jina Madaha ni la nini hilo, mimi mwenyewe Msukuma.
Frank/OFM: Nimefurahi sana kusikia hivyo, unaweza kuongea Kisukuma?
Baby Madaha: Naweza, wewe nisemeshe tu!
Frank/OFM: Nakutogilwe gete Madaha (Frank anaongea Kisukuma kwamba anampenda sana Madaha)
Baby Madaha: Tukuhoya ntondo nduhu tabu (anajibu kwa Kisukuma kuwa hakuna tatizo tutaongea kesho).
Ulipofika muda waliokubaliana na Frank wa OFM, Madaha alisema kuna foleni kubwa hivyo kuna sababu ya kubadilisha hoteli hiyo iliyoko maeneo ya Ubungo alipopanga Frank wa OFM waonane, Baby Madaha akataka wakutane nyingine iliyoko Kijitonyama.
“Siwezi kuja huko, kwanza kuna mifoleni isitoshe ni vizuri ukafika mwenyewe maeneo haya ya hoteli ya… (anataja), ni sehemu nzuri kwangu hivyo kama huna nia mbaya na mimi ni vizuri ukaja maana kesho nasafiri kwenda Kenya kwenye shughuli zangu za muvi, kwa hiyo unaweza kuja wewe tu maeneo haya,” alisema Madaha.
 
Frank aliendelea kumbana kwamba tayari alikuwa ameshaandaa pesa shilingi Mil.5, kama walivyokubaliana lakini asingeweza kubeba mfuko wa fedha wote huo isitoshe ni hoteli ambayo ameizoea kwa muda mrefu.
“Ujue Dar mimi siyo mzoefu, achilia mbali kuogopa kutapeliwa hivyo nakuomba uje kwenye hii hoteli nitafurahi sana dear, nakuomba unielewe ujue nakupenda sana mpenzi wangu Baby Madaha, tulia tuyajenge maisha,” alisema Frank wa OFM.
Msanii huyo alimkomalia Frank wa OFM wakutane siku ya Jumanne usiku ambapo alimwambia pia kuwa amepata dharura anakwenda kumuona mfanyabiashara mwenzake kwenye hoteli moja iliyopo Masaki (jina tunalo) ambapo Baby Madaha alitaka waonane na Frank wa OFM kwenye hoteli hiyohiyo.
“Nimepata dharura sitaweza kuonana na wewe, naenda kumuona mfanyabiashara mwenzangu maeneo ya hoteli…(jina tunalo), tuonane kesho muda wa asubuhi,” alisema Frank.
Baadaye Frank alimjulisha mteja wake kuwa yuko njiani anafuata mzigo bandarini akitoka wataonana na Baby Madaha kesho yake asubuhi ya Jumatano iliyopita, alituma sms hii;
Baby Madaha: Kuna stage tano in anything, nakupa tatu, coz uko siku ya tatu, denying, bargaining, accepting..... tomorrow if you be still on game, i give you the remained good day, enjoy Mr Frank, ukitoka cargo call me, we meet!
Frank/OFM: Okay, siku njema nitakutafuta.

Baby Madaha: Matajiri wengine hawana maneno kama wewe kwa mfano…(anataja jina la pedeshee mmoja maarufu Dar). Wanatuma pesa na siyo maneno, wee tuma hela (-)-pesa ipo kila sehemu we tuma ndo nitaweza kujiongeza kama nakuja au laa.
Frank/OFM: Nakutumia muda siyo mrefu, usijali.
IJUMAA LAMBANA BABY MADAHA
Hata hivyo, Baby Madaha hakutumiwa pesa alizotaka ili kukamilisha zoezi badala yake, OFM walitua mzigo wa ushahidi kwenye dawati la Ijumaa ambalo lilikuwa na jukumu la kutafuta mzani wa ishu hiyo.
Ijumaa lilipomtafuta Baby Madaha alikiri kuwa kwenye mawasiliano na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Frank Michael Lugisha ambaye alisema alikuwa akifanya naye makubaliano ya kusambaza filamu yake ya The Gal Bladder.
Alipobanwa juu ya makubaliano ya kujiuza kwa mwanaume huyo kwa Sh. milioni 5 alikataa pamoja na kwamba alielezwa kuwa kuna ushahidi wa meseji na sauti.
Alipotakiwa kufika kwenye ofisi za gazeti hili ili kusikilizishwa sauti na kuoneshwa meseji zake, Baby Madaha alisema hawezi kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda nchini Kenya muda mfupi baadaye.
CREDIT:GPL.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper atambulisha bwana mpyaaaaa.

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Akizunhumza na ijumaa hivi karibuni amesema alikuwa kimya kwa mda kutafakari kwani asingeweza kukurupuka bila kuchunguza tabia ya mpenziwe.


Hayo yamekuja baada ya kuachana na mchumba ake wa zamani Dallas.

Amesema anafurahia sana mpenzi wake wa sasa na anaomba mungu awajalie waweze tambulishana kwa wazazi na hatimaye kufunga pingu za maisha.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Thursday, January 16, 2014

Masikini Dada Huyu amwagiwa tindikali na mumewe wakigombea mali.



MARIA Nkwabi [33] Mkazi wa Kijiji cha Kakola akiwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kumwagiwa Tindikali na Mumewe;Ray Chobe katika ugomvi unaodaiwa kugombea mali.
Jeshi la Polisi Wilayani Kahama limethibisha kutokea kwa tukio hilo na bado wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo.
MWONEKANO WA BI MARIA NKWABI BAADA YA KUPATA HUDUMA YA KWANZA.

Kweli hii sio Fair Kabisa kama huwezi kuishi na mwanamke acha usioe.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Cheki alichokisema Flora Mvungi 'MRS H.BABA' katika Instagram, kuhusu Penzi la Wema Na Diamond.

 Huyu Ndiye frora Mvungu aka Mme wa H.Baba ambaye hivi karibuni kasherekea Birthday yake .
Bila shaka zile taarifa za Wema kunyang’anywa vitu aliipata na kuandika haya


Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Happy Birthday TO YUUUUU! Ona jinsi H.Baba na mkeo Florah Mvungi walivyosherekea siku ya kuzaliwa.

 H.Baba na mke wake, Florah Mvungi wakilishana keki.


H.Baba akimlisha keki mama yake.

Florah Mvungi akiwa na mtoto wake Tanzanite. 


 Florah Mvungi  akiwa ameshika keki ya bethidei.

Jana tarehe mtu mzima H.Baba msanii kutoka kule Mwanza alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na familia yake nikimaanisha mke wake na mtoto wao mpya anaitwa Tanzanite pamoja na mama mzazi wa HBaba na wadogo zake wa mwisho.
 Hizi ni baadhi ya picha tu wakiwa pamoja wakila keki kwa pamoja.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Wapora maiti baada ya kuchoshwa na ibada ya kanisa TAG Uyole, Mbeya


Kundi la vijana 60, juzi walipora mwili wa marehemu Gabriel Ngalele ukiwa unaombewa kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) eneo la Uyole jijini baada ya kuchoshwa na ibada ndefu ya mchungaji.
 
Ibada hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Mchungaji, Edward Mtweve wa kanisa hilo ambaye alijikuta kwenye mazingira magumu baada ya vijana hao wanaodaiwa kuwa ni madereva wa pikipiki kuvamia madhabahu na kubeba sanduku lililokuwa na mwili wa marehemu.
Marehemu Ngatele alikuwa dereva wa pikipiki na alifariki kwenye ajali iliyotokea eneo la Sae baada ya pikipiki yake kuligonga lori lililoharibika katikati ya barabara. Katika ajali hiyo, abiria pia alifariki.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika kanisa hilo, na wakati mchungaji akiendesha ibada kulijitokeza kelele za hapa na pale na kusababisha mchungaji kuomba utulivu mara kadhaa.
Lakini kelele nyingi zililipuka ghafla zikiwamo za kulalamika kwamba ibada ilikuwa ndefu na hatimaye vijana wengi walionekana wakiingia kwenye mlango na kuvamia madhabahu na kutoka na mwili wa marehemu.
 
 Kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole
Baada ya kuuchukua mwili, vijana hao walikwenda kwenye makaburi kuuzika wakati naye mchungaji akiendelea kuhubiri waumini waliobaki ndani ya kanisa.
Mchungaji Mtweve alilazimika kwenda nyumbani baada ya kumaliza ibada badala ya makaburini, huku vijana nao wakiendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa waendesha pikipiki Mbeya, Vicent Mwashoma.

 
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani
Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.

Mwendesha pikipiki aliyetajwa kwa jina la Bahati Mwasote alilazimika kuendesha ibada ya mazishi.
Mchungaji Edward Mtweve alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema alisikitishwa na kitendo cha kuvurugwa kwa ibada.
Chanzo:Mwananchi.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Mapenzi Nomaaaa WEMA SEPETU.ANYANG'ANYWA KILA KITU KISA KURUDIANA na DIAMOND.


Msanii wa filamu Bongo, Wema Isaac  Sepetu, amenyang’anywa samani za ofisi yake ya Endless Fame Film Production na aliyekuwa mpenzi wake, Clement ‘kigogo wa ikulu’ na sasa amebaki mweupeeheeeeeeeeeeeeeeeee,  Amani limepakuliwa ikiwa imeiva.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la aibu lilijiri hivi karibuni kwenye ofisi hiyo ya Wema iliyopo Mwananyamala-Komakoma jijini Dar.

KIGOGO WA IKULU AVAMIA NA MABAUNSA
Habari za uhakika zinadai kuwa, siku ya tukio, Clement akiwa ameongozana na watu waliosadikiwa kuwa ni mabaunsa, walivamia ofisi hiyo aliyomfungulia mlimbwende huyo na kukomba vitu vyote vya thamani alivyomnunulia wakati wa mapenzi motomoto (hakuna lenye mwanzo lisilo na ncha).

KUMBE ALIKODI CANTER
Kama njiwa apelekaye ujumbe muhimu wa huba, mtoa taarifa huyo alizidi kumwaga ‘upupu’ kuwa, siku hiyo Clement mbali na gari lake la kifahari, pia alitinga akiwa na gari aina ya Canter ambapo bila maswali wala maelezo achilia mbali ufafanuzi, alikusanya vifaa vyote na kuvirundika kwenye gari.
 

Wema akiwa katika ofisi yake kabla ya kunyang'anywa samani zilizomo.

IDADI YA VITU VILIVYOBEBWA
Vifaa hivyo ni tarakishi (computer), kamera ya kurekodi sinema (video camera), vifaa vya kurekebisha hali ya hewa (air conditioner), vifaa vya kuhifadhia umeme wa ziada, uninterruptible power supply  (ups) pamoja na vifaa vingine zikiwemo nyaya za umeme na kuiacha ofisi nyeupe kama uwanja wa mpira.

“Hali ni mbaya sana, jamaa (Clement) alichukua kila kitu ndani ya ofisi hiyo kuanzia kompyuta, kamera hata nyaya! Hivi tunavyoongea, ofisi haina kitu kabisa,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.

CHANZO NI DIAMOND
Mpashaji huyo alizidi kuyapa utulivu masikio ya mwandishi wetu kuwa, chanzo cha kigogo huyo kufanya ‘umafia’ huo ni kitendo cha Wema kurejesha penzi lake kwa ‘mtemea maiki’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.


Geti la kuingia katika ofisi hiyo.

“Ni kweli kabisa Clement amefanya hivyo, lakini nashangaa na ni mara yangu ya kwanza kuona wapenzi wakiachana mwanaume anaamua kuchukua vitu vyote alivyowahi kumnunulia au kumpa.
“Huo ni ushamba na unyanyasaji, akumbuke kwamba alipokuwa na mimi alinitumia pia,” alisema Wema na kuongeza:

“Hata hivyo, namshukuru Mungu, vitu vyote alivyochukuwa Clement, baby (Diamond) kasema ataninunulia, wiki mbili hazitapita.”
Wema alikwenda mblele zaidi kwa kuonesha machungu yake kwa kigogo huyo pale aliposema: “Kwanza nasikia vitu vyenyewe alipofika nyumbani kavimwaga nje maana ndani hakuna nafasi.”

KAANZA MWAKA VIBAYA
Mwanzoni mwa mwaka huu, Wema alikumbwa na mkasa wa kunyang’anywa lile gari la kifahari alilodai ni lake, Audi Q7 baada ya kusemekana kuwa halikuwa lake.
Kumbe gari hilo alipewa na Clement ambaye naye alilikopa kwa thamani ya shilingi milioni 90 kutoka kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Shadrack Tweve.

Tweve, baada ya kuzungushwa sana kulipwa fedha hizo, alikimbilia Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo hakimu aliamuru gari hilo likamatwe na kurejeshewa mlalalamikaji huyo.

PENZI LA WEMA, NA KIGOGO WA IKULU
Uhakika ni kwamba, penzi kati ya Wema na kigogo huyo halipo tena na kwa sasa jamaa ana demu mwingine (jina tunalo) ambapo mapaparazi wetu wanaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuwanasa katika mazingira yoyote yale.
CREDIT:GPL

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Wednesday, January 15, 2014

Watangazaji wa CLOUDS FM:: DIVA LOVENESS, B12 NA ADAMU MCHOMVU,WAMEFUKUZWA.

WATANGAZAJI maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na kituo hicho... 

Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.
Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikiri.

“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.
“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.

Alipoulizwa ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Baikoko la TANGA cha mtoto Cheki hili la Mombasa hapa ,NI ZAIDI YA LAAANAA ..!!!!



Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

NILIMFUMA MKE WANGU AKINYATIA KUINGIA KWENYE CHUMBA CHA MDOGO WANGU WA KIUME..

Kumbe ilikuwa ni tabia yake kwenda kwa mdogo wangu huyo wa kiume ambaye ni mtoto wa shangazi yangu, na kula uroda wakati mimi sipo, nilipata tetesi hizo kutoka kwa housegirl wetu lakini sikuweza kuamini. siku hiyo nilirudi kimya kimya na kujifungia chumba kimoja ambacho kilikuwa hakitumiki, na wote hawakujua kama nilikuwa nipo.

Mara ilipofika ,majira ya saa nne hivi usiku, nilimuona mke wangu ananyata huku akiwa amevaa nguo za ajabu sana, alipita chumba cha house girl na kisha kuzama kwenye chumba cha ndugu yangu huyo wa kiume. nilitoa simu yangu niliyokuwa nayo na kumpiga picha kwa ushahidi zaidi, alipoingia tu na mimi nikaingia alishindwa kuamini na gafla alianza kuomba msamaha, nilimuuliza mke wangu kwani umefanya nini alishindwa kunijibu huku akiendelea kulia na kuomba msamha, nilitoka na kwenda chumbani kwangu kulala, yule mdogo wangu wa kiume alifungasha usiku ule ule na kuondoka na mke wangu hakuweza kulala, iliniuma sana sikuweza kuamini kwani nilimuamini sana mke wangu.

Kesho yake sikuweza kuvumilia nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao , kwani ningeweza kumfanya kitu kibaya sana kama ningeendelea kumuona. 

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Tuesday, January 14, 2014

Mbaya SANA;Daktari aliyeiba watoto 7 na kuwauzia wafanyabiashara nchini China ahukumiwa Kifo.

Daktari mmoja katika mkoa wa Kaskazini wa Shanxi nchini Uchina amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuwaiba watoto saba kutoka hospitali aliyokuwa akihudumu na kuwauza watoto hao kwa wauzaji watoto.

Wakati mmoja daktari Zhang Shuxia alikuwa mtaalam mashuhuri lakini sasa ni nuhalifu mwenye hatia aliyejipatia faida kubwa kutokanana na uuzaji wa watoto.

Daktari huyo aliwadanganya wazazi wapya kwamba watoto wao walizaliwa wakiwa na ugonjwa mbaya.Aliwahadaa kwamba iwapo wazazi wangeliwachia serikali jukumu la kuwaangalia basi wangepewa matibabu ya hali ya juu waliohitaji.

Watoto hao wenye afya njema baadaye waliuzwa kwa bei ya maelfu ya madola kwa wauzaji watoto wanaohudumu katika mikoa ilio karibu.

Sita kati ya watoto walioibwa walipatikana na kurudishwa kwa wazazi wao huku mtoto mmoja aliyeuzwa kwa dola 165 pekee akipatikana ameaga dunia kandokando ya barabara ambapo alikuwa amewachwa na muuzaji mmoja wa watoto.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Video na maelezo ya Boyfriend wa Cliff akihojiwa juu ya nn waliongea na Jackie Cliff aliyenasa china .


Ndani ya wiki moja iliyopita Balozi wa Tanzania nchini China aliongea Exclusive na millardayo.com na kuthibitisha kwamba hajawahi kupokea taarifa kutoka gereza lolote la China juu ya kukamatwa na dawa za kulevya kwa Mtanzania, mrembo ambae amekua akitokea kwenye video kadhaa za bongofleva “Jackie Patrick Cliff’
Maelezo yake yalifanya kuwe na maswali zaidi manake kila mmoja alikua anajiuliza atakua wapi Mtanzania huyu baada ya taarifa kusambaa kwenye vyombo vya habari Tanzania kwamba kakamatwa huko Macao?


Boyfriend wake ambae ni msanii wa bongofleva Jux ameongea kwenye Exclusive interview na millardayo.com Jan 13 2014 saa kadhaa baada ya kuweka post ambayo ilionyesha wamewasiliana muda mfupi uliopita.

Baadhi ya maswali aliyoyajibu kwenye video hapa chini ni pamoja na Wameongea lini mara ya mwisho? Jack anasemaje? Jack alikua wapi wakati wanaongea? yuko nchi gani? anarudi lini bongo? na mengine.
Video yenyewe hii hapa:

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

kagame atoa onyo kali kwa Wasaliti wa Rwanda;Watatafutwa kokote duniani watakakokimbilia.


Rais Paul Kagame wa Rwanda ameonya kwamba atakayethubutu kulisaliti taifa hilo atakiona cha moto.Rais Kagame alikuwa akielezea hisia zake wakati wa sala za kuombea taifa hilo kwa awamu ya kumi na nne.Hayo yamejiri siku chache baada ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha kwa aliyekuwa kiongozi wa ujasusi nchini humo Patrick Karegeya katika hoteli moja nchini Afrika Kusini.

Pia siku za karibuni kulikuwa na taarifa za  uongo za eti kagame kafa.
Tetesi za kifo cha Kagame zilitoka Wapi?Jibu hili hapa
Wakazi wa Goma walibeba jeneza bandia likiwa na Msalaba baada ya kupata taarifa hizo

Kwa masaa kadhaa Ijumaa iliyopita yaani tarehe 10/01/2013 nyakati za asubuhi, kulikuwa na fununu kuwa Rais wa Rwanda,Paul Kagame ameaga dunia na taarifa hizo zilienea hadi mji wa Goma Mashariki mwa Congo. Wengi walisherehekea baada ya kupata habari hizo.

Lakini taarifa hiyo inasemekana kutokana na ujumbe bandia kwenye Facebook.
Hapana shaka kuwa kuna uhasama kati ya DR Congo na Rwanda hasa katika eneo la Mashariki mwa DRC ambako Rwanda imekuwa ikituhumiwa kwa kuchochea ghasia zinazoendelea huko.

Kwa hivyo fununu zilipoanza kuenezwa kuwa Kagame amefariki, walikuwa na furaha sana.
Mamia ya watu waliandamana kwenye barabara za mji wa Goma kuelekea katika mpaka wa Rwanda kusherehekea kile ambacho baadaye kilijuliakana kuwa tu tetesi na fununu za uongo kuwa Kagame kafariki.Hata walibeba jeneza bandia na msalaba .Madereva barabarani walishaniglia kwa kupiga honi.

Tetetsi hizo zilipingwa vikali na serikali ya Rwanda kupitia Twitter.Waziri mkuu wa Rwanda alijibu kwa kusema , kuwa taarifa hizo ni za kipuuzi sana huku mshauri mkuu wa Kagame pia akisema ni mambo ya kipuuzi.Punde baada ya fununu hizo, maafisa wa serikali walichapisha picha ya Kagame kwenye Tiwtter akiamkuana na wanafunzi wageni waliotembelea nchi hiyo kutoka Marekani, ishara ya kuwa Kagame yuko hai.Chuo hicho kimethibitishia BBC kuwa picha hiyo ni ya kweli na kuwa Kagame kweli alikutana na wanafunzi hao.

Sasa kwa kuwa Kagame yuko hai na anaendelea na kazi zake za kawaida, fununu hizo zilitoka wapi na zilianza vipi?

Wakazi wa Goma wanasema kuwa zilitokana na ujumbe kwenye facebook ambao ulitolewa kwenye mtandao bandia kuhusu taarifa za vifo. Ujumbe huo ulichapishwa na kuanza kusambaziwa watu wa Goma.Christoph Vogel, mtaalamu wa maswala ya Goma, anasema kuwa alianza kusikia kelele za watu asubuhi na kisha kuona baadhi ya ujumbe wa Facebook ukichapishwa katika mkahawa mmoja.Na hapo ndipo maji yalizidi unga kwani watu walianza kukusanyika wakishangiliaNa hivyo ndivyo taarifa huibuka na kuenea ziwe na kweli au za uongo .

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Vieleele vya wanawake Mmoja kati ya hawa nusura alie jana baada ya mpenziwe kutoswa.

Tuzo za Ballon d'Or 2013 zilitangazwa jana huko Zurich na kuhudhuriwa na watu wengi wakiwemowachezajiwa zamani akama pele na Delima. lakini pia tuzo hizo zilihudhuriwa na wanawake maarufu duniani yaani yule sh wa Ronaldo ambaye ni mwanamitindo na Sh wa Messi.

Baada ya raikisho la soka ulimwenguni Sepp Blatter kumtangaza  CR7 kuwa ndiye mshindi sh wa Mesii alikuwa katika wakati mgum kwani hakuamini machoni mwake kuwa hayo yametokea yaani mpenziwe kukosa tuzo hizo ambaye yy binafsi alidhani kuwa Lionel Messi angeshindinda tuzo hiyo ya  Ballon d'Or.

Hata ronaldo mwenyewe pindi anaenda pokea tuzo hiyo machozi yalimjaa machoni sijui ni kwa vile aliona miujiza au ni nn lakini ukweli ni kwamba majeraha ya Messi ndo yamefanya CR7 kunyakua tuzo hiyo kwani upinzani aliotegemea ni kutoka kwa Messi na sio Ribbery.

Picha nyingine na video  hizi hapa.
Picha zingine :




Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Monday, January 13, 2014

ANASWA CHINI YA UVUNGU AKIWALIA CHABO WANANDOA WAKI NANINILI.......


NI aibu kubwa! Mpigachabo maarufu nchini, Andrea Masangu (29) amenaswa akiwa kwenye uvungu wa kitanda akiwapiga chabo wanandoa, Ijumaa Wikienda lina mkasa wote mkononi.

Tukio hilo lilitokea Januari 10, mwaka huu, ndani ya Gesti ya Riverside, Stendi ya Nyegezi jijini hapa ambapo kijana huyo aliingia kwa kuruhusiwa na mhudumu wa gesti hiyo katika mtego makini uliotegwa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na mwishowe kujikuta akiumbuka.

KWA WATU WAZIMA TU; CORAZON AMEACHIA VIDEO NYINGINE AKIKATIKA AKIWA NUSU UTUPU ICHEKI HAPA.

OFM WAPOKEA MASHTAKA
Wiki moja nyuma, mtu mmoja alipiga simu kwa OFM jijini Dar akidai yeye ni msomaji wa MagazeMPIGti Pendwa ya Global. Akasema ameamua kupiga simu ili kumshtakia Andrea akidai amekuwa na tabia iliyoota sugu ya kupiga chabo wapenzi wanapokuwa gesti.
“Mimi naitwa…(akataja jina lake), napiga simu kutoka jijini Mwanza. Kuna bwana mmoja anaitwa Andrea, amekuwa na tabia ya kuwachungulia (kuwapiga chabo) wapendanao wanapokuwa gesti.
“Mbaya zaidi, huyu jamaa nasikia huu mtindo anao siku nyingi sana. Amekuwa akienda hata nje ya Mkoa wa Mwanza kwa ajili hiyo,” alisema mtoa habari huyo.
Akaongeza: “Kuna watu wanasema kuwa hata Tabora, Dodoma wanamjua kwa tabia hiyo. Hebu

PICHA NA VIDEO ZA SHILOLE AKIWA MZIWANDA KITANDANI ZAVUJA MTANDAONI, JIONEE MWENYEWE HAPA.

OFM njooni Mwanza.
Ijumaa Wikienda: Usipate tabu, hukohuko Mwanza kuna OFM wametokea hapa makao makuu. Nawapa namba yako ili mshirikiane.
Mtoa Habari: Mtakuwa mmefanya jambo la maana sana.

KAZI YAANZA
Ndani ya dakika tano tu, OFM waliopo Mwanza wakapewa namba za mnyetishaji wetu, kazi ikaanza.
OFM Mwanza, walimtafuta mtoa habari huyo na kukaa naye meza moja ambapo walipanga mipango.
Miongoni mwa mipango hiyo ilikuwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi jijini Mwanza ambapo maafande walijipanga.

SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio, Andrea alikwenda kwenye gesti hiyo na kumuuliza mhudumu kama kuna wateja wa ‘shot’ taimu’ wataingia, akajibiwa wapo njiani.
Akaomba alipe shilingi elfu mbili (2,000) ili atangulie kuingia yeye kwenye chumba ambacho mhudumu huyo atahakikisha anawaingiza wapendanao hao.

OFM WAJULISHWA, WAINGIA
OFM walijulishwa kuwa mpiga chabo huyo amewasili na tayari ameingia chini ya kitanda kwenye gesti hiyo, nao wakamchukua OFM mwanamke na kutinga naye sanjari na Polisi wa Dawati la Jinsia Jiji la Mwanza.

OFM WAMCHEZEA MCHEZO
Ndani ya chumba hicho, wapendanao (mke na mume) hao walifikia kitandani. Lakini ili kujiridhisha kama kweli Andrea alikuwa uvunguni, OFM mwanaume alijifanya ameangusha pesa chini, alipoinama kuiokota akamuona kiaina lakini hakuonesha kushtuka.
Ndipo OFM hao ‘wapendanao’ walianza kuchojoa nguo za juu na kuzitupa chini kana kwamba walikuwa tayari ‘mchezoni’ ili kumshawishi Andrea aendelee kuamini na kufurahia dhamira yake chafu.

OFM NJE YA GESTI
Nini kilibaki hapo kama si OFM waliokuwa chumbani kuwajulisha kwa simu wenzao waliokuwa nje na polisi?
Chumba kilivamiwa, Andrea akajikuta yuko chini ya mikono ya sheria akionekana ameingilia faragha.

ETI AKAJITETEA!
Baada ya kutolewa chini ya kitanda, Andrea aliwekwa mtu kati na kuhojiwa kulikoni kuwa mpiga chabo wa kiwango kile?
Andrea alianza kwa kuomba msamaha na kuahidi kuacha kabisa tabia hiyo. Alikiri amekuwa akichungulia watu wengi sana wanaofika katika gesti za jijini Mwanza.
“Jamani nimekoma, ni shetani tu, naacha kabisa mambo haya ‘haki  ya Mungu’ kuanzia leo sifanyi tena.

BABY MADAHA APONEA CHUPU CHUPU KUBAKWA.

“Kweli nimewachungulia watu wengi sana na sijapata faida yoyote, sijui shetani gani aliniingia,” alilalama Andrea na kuongeza kuwa hayupo peke yake bali ana marafiki zake wengi ambao hufanya kama anavyofanya yeyeSoo hilo liliisha kwa Mshauri Nasaha wa Taasisi ya Farijika, Aisha Mtumwa kumrekebisha kisaikolojia Andrea sambamba na kumpa onyo kwamba akirudia tena atatupwa rumande kwa kosa la kuingilia faragha ya watu

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Zitto mahakamani tena: Safari hii ataburuzwa na Freeman Mbowe sio CHADEMA tena.

 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anapanga kumchukulia hatua za kisheria Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutokana na kile alichodai kuwa ni kuzusha tuhuma zenye lengo la kumchafua yeye binafsi na chama hicho.

Tuhuma dhidi ya Mbowe ziliibuka baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu Zitto kuwa amehongwa magari mawili na Mkono.

Taarifa ya kusudio la Mbowe kumburuza Zitto mahakamani ilitolewa jana na Ofisa Mwandamizi wa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, huku ikikanusha tuhuma zote zilizotolewa dhidi ya Mbowe.

“Mbowe ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria. Mwenyekiti wa chama hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ambayo hata hivyo haikumtaja Zitto moja kwa moja.
 
Taarifa hiyo imesema tuhuma zinazoshughulikiwa ni zile zinazodai kwamba Mbowe alichukua Sh40 milioni mwaka 2005  kutoka kwa Mkono ili asifanye kampeni katika Jimbo la Musoma Vijijini.
Tuhuma nyingine ni kuwa 2008 Mkono alimpatia Mbowe Sh20 milioni kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime, kwamba Mbowe alizitoa fedha hizo kwenye chama kama mkopo na akalipwa.
 
Mvutano kati ya Zitto na Chadema ulishika kasi baada ya Mbunge huyo kufungua kesi Mahakama Kuu kuomba mahakama hiyo kuizua Kamati Kuu (CC) ya Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Zitto alishinda katika shauri hilo.
Chanzo:Mwananchi;

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Sunday, January 12, 2014

Wakati Israeli ina majonzi, Wapalestina washerekea kifo cha Ariel Sharon.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua kiharusi toka mwaka 2006 wakati akiwa kwenye zama za juu za maisha yake ya kisiasa.
Bwana Sharon ni mtu muhimu kwenye historia ya taifa la Israel tangu akiwa jenerali wa jeshi na baadaye mwanasiasa.
Kifo ni kitu cha huzuni kwa wafiwa na jamii kwa vile aliyekufa hataonekana hivyo burasa na kila kitu cha ndo vimekwisha.

Alikuwa kiongozi shupavu lakini atasalia kukumbukwa kwa utata wake mkubwa hasa miongoni mwa wapalestina.

Mkuu wa kituo cha matibabu cha Sheba karibu na mji wa Tel Aviv alisema kuwa Sharon alifariki Jumamosi jioni.


Rais Shimon Peres alisema kuwa Sharon aliijenga Israel ingawa afisaa mmoja mkuu akaongeza kuwa safari ya Sharon ilikuwa ya vita na mashambuliika ili kuweza kufikia malengo yake ya kisiasa.

Cha ajabu baada ya taarifa kusambazwa Wapalestina wamefanya sherehe za haraka wakisema mtu huyo alikuwa mbaya sana kwao.
Katika majiji kadhaa keki zilinunuliwa haraka huku kukiwa na shamra shamra za kusherekea kifo hicho.
Tusichokijua ni kama Israel itabadilisha msimamo na siasa zake juu ya Palestina kutokana na kifo hicho.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top