Tuesday, January 14, 2014

Mbaya SANA;Daktari aliyeiba watoto 7 na kuwauzia wafanyabiashara nchini China ahukumiwa Kifo.

Daktari mmoja katika mkoa wa Kaskazini wa Shanxi nchini Uchina amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuwaiba watoto saba kutoka hospitali aliyokuwa akihudumu na kuwauza watoto hao kwa wauzaji watoto.

Wakati mmoja daktari Zhang Shuxia alikuwa mtaalam mashuhuri lakini sasa ni nuhalifu mwenye hatia aliyejipatia faida kubwa kutokanana na uuzaji wa watoto.

Daktari huyo aliwadanganya wazazi wapya kwamba watoto wao walizaliwa wakiwa na ugonjwa mbaya.Aliwahadaa kwamba iwapo wazazi wangeliwachia serikali jukumu la kuwaangalia basi wangepewa matibabu ya hali ya juu waliohitaji.

Watoto hao wenye afya njema baadaye waliuzwa kwa bei ya maelfu ya madola kwa wauzaji watoto wanaohudumu katika mikoa ilio karibu.

Sita kati ya watoto walioibwa walipatikana na kurudishwa kwa wazazi wao huku mtoto mmoja aliyeuzwa kwa dola 165 pekee akipatikana ameaga dunia kandokando ya barabara ambapo alikuwa amewachwa na muuzaji mmoja wa watoto.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top