Bwana Sharon ni mtu muhimu kwenye historia ya taifa la Israel tangu akiwa jenerali wa jeshi na baadaye mwanasiasa.
Kifo ni kitu cha huzuni kwa wafiwa na jamii kwa vile aliyekufa hataonekana hivyo burasa na kila kitu cha ndo vimekwisha.
Alikuwa kiongozi shupavu lakini atasalia kukumbukwa kwa utata wake mkubwa hasa miongoni mwa wapalestina.
Mkuu wa kituo cha matibabu cha Sheba karibu na mji wa Tel Aviv alisema kuwa Sharon alifariki Jumamosi jioni.
Rais Shimon Peres alisema kuwa Sharon aliijenga Israel ingawa afisaa mmoja mkuu akaongeza kuwa safari ya Sharon ilikuwa ya vita na mashambuliika ili kuweza kufikia malengo yake ya kisiasa.
Cha ajabu baada ya taarifa kusambazwa Wapalestina wamefanya sherehe za haraka wakisema mtu huyo alikuwa mbaya sana kwao.
Katika majiji kadhaa keki zilinunuliwa haraka huku kukiwa na shamra shamra za kusherekea kifo hicho.
Tusichokijua ni kama Israel itabadilisha msimamo na siasa zake juu ya Palestina kutokana na kifo hicho.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment