Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anapanga kumchukulia hatua za kisheria Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutokana na kile alichodai kuwa ni kuzusha tuhuma zenye lengo la kumchafua yeye binafsi na chama hicho.
Tuhuma dhidi ya Mbowe ziliibuka baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu Zitto kuwa amehongwa magari mawili na Mkono.
Taarifa ya kusudio la Mbowe kumburuza Zitto mahakamani ilitolewa jana na Ofisa Mwandamizi wa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, huku ikikanusha tuhuma zote zilizotolewa dhidi ya Mbowe.
“Mbowe ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria. Mwenyekiti wa chama hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ambayo hata hivyo haikumtaja Zitto moja kwa moja.
Taarifa hiyo imesema tuhuma zinazoshughulikiwa ni zile zinazodai
kwamba Mbowe alichukua Sh40 milioni mwaka 2005 kutoka kwa Mkono ili
asifanye kampeni katika Jimbo la Musoma Vijijini.
Tuhuma nyingine ni kuwa 2008 Mkono alimpatia Mbowe
Sh20 milioni kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime, kwamba
Mbowe alizitoa fedha hizo kwenye chama kama mkopo na akalipwa.
Mvutano kati ya Zitto na Chadema ulishika kasi baada ya Mbunge
huyo kufungua kesi Mahakama Kuu kuomba mahakama hiyo kuizua Kamati Kuu
(CC) ya Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama
wake hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Zitto alishinda katika shauri hilo.Chanzo:Mwananchi;
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment