Wednesday, January 29, 2014

Kama ulimiss hii: Dalili kuu 2 za mwanamke kufika kileleni



ZIFUATAZO NI DALILI KUU ZA MWANAMKE ANAPOKARIBIA KUFIKA KILELENI:

1. Dalili ya kwanza inayomuashiria mwanamke anapotaka kufika kileleni ni ya kupiga mayowe/kelele, hii ni dalili kubwa kwa wanawake wengi napozungumzia dalili hii sina maana kwamba ya kupiga kelele za fujo ila kelele zinazopigwa ni zile za raha zilizoambatana na Miguno ya kimahaba kama alikuwa anatoa sauti ya chini ghafla utaanza kuona anapandisha na kuikuza sauti. Pia kuna wanawake wengine hujikuta wakiropokwa maneno pindi raha zinapozidi,

2. Dalili nyingine ya pili inayoweza kukusaidia kumtambua mwanamke anapotaka kufika kileleni ni hii wanawake wengi hubainika kufika kileleni pindi raha zinapo

wazidia na wanapo kojoa (Bao) huwakumbatia wapenzi wao kwanguvumpaka wanapomaliza kukidhi haja yao katika hili pia unaweza kumuona mwanamke mwingine anafikia mpaka hatua ya kukung'ata meno ila fahamu zote zinakuwa ni raha anajikuta anafanya vitu bila kutarajia.

Naamini somo limeeleweka na kwa hizi dalili chache sidhani kama ikitokea mwanamke wako akifanya moja wapo kati ya hili kwako itakuwa kama suprise ni vitu vya kawaida katika mapenzi na jinsia zote mbili zina haki ya kuridhika katika sehemu ya kusex. Ushauri wangu mkubwa ni kuzingatia maandalizi mazuri kabla ya tendo

kwani siku zote huwezi kuplan kujenga nyumba bila kuwa na msingi na kwenye mapenzi pia huwezi kufanikiwa kumridhisha mwenza wako bila kumuandaa.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Kanidanganya yeye ni Bikira na hayawai ku do KUMBE….Majanga.


Mambo niaje wakuu..sijui hata nianzie wapi?...hawa wanawake...!! basi tu!!basi bwana nmekua nikimdate dada mmoja mwenyeji wa iringa .sio siri kwa haraka haraka nlijua huyu ananipenda kwa dhati, mie kiukweli nlimpenda sana.

Tumedate kwa almost mwaka na nusu,kwa mda wote huo sharti ilikua ni hakuna kugegendana mpaka tufunge ndoa.Kidume nlijipa moyo nkajikaza kwani nilihusi namjua sana ni mlokole haswaa mpka watu uwa wananishangaa nlimpataje coz mie cnaga swaga za kilokole,aliku kesha nihakikishia kua yeye ni bikira na ajawai ku do.

Kwa mda wote wa mapenzi yetu nmekua nikijaribu kuomba mchezo ila ilishndkana.juzi kati ulizuka ugomvi mkubwa sana kati yangu na yeye kisa kikiwa ni hicho hicho kugegenda, Mimi nkiwanataka yeye ataki,tumekaa bila kuongeleshana kwa almost wiki nzima,jana ijumamosi ndo aliamua kuvunja ukimya na kuniita niende kwake ili tusort out ili tatizo.

Tuliongea mengi ila dada bado alikua kashikilia msimamo wake ila akaniomba nimpe mda kidogo afikilie jinsi ya kulifanya hilo, nlimkubalia, basi ile kuangana kwa hugs na kisses tukajikuta kitandani bahati nzuri ni kama she was 50/50 kufanya, na mie sikutaka kua ---- nikatoa dudu fasta nikijua leo ndo naifumua zawadi yngu ya chrsmas... mmmh.. nilichokikuta huko staki kuamini mpka sa hvi.. nahisi mie nlikua mwanaume wa 50 Kumuingilia.

Hata gori nlishdwa kupiga kwa sababu ya mawazo nlokua nayo, nilivaa suruali yangu taratibu. nikimwacha demu analia sana uku akiniomba msamaha daa wanawake siwatamani tena.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Msanii wa vichekesho KINYAMBE anusurika kulawitiwa na MABAUNSA...Soma hapa.


Na Mwandishi watu wa  Xdeejayz & Boss ngasa
Msanii aliyejichukulia umaarufu mkubwa kutokana na stairi yake ya uigizaji imesemekana ilikuwa alawitiwe endapo angenasa mtego huo wa fumanizi lakini kwa bahati mbaya 
fumanizi hilo lilidunda.


Habari za uhakika zilizofanywa na webesite hii baada ya wiki iliyopita kuzuka habari za kufuamaniwa kwa msanii huyo aliyefahamika kwa jina la Kinyambe. 


Paparazi wetu ambae alifika eneo la Kawe ambako ndiko inakodaiwa msanii huyo alifumaniwa wakiongea kwa sharti  ya kutotajwa majina yao walisema" Huyu jamaa Mungu alikuwa upande wake kwani huyo jamaa mwenye mke alikuwa ameshaandaa mabaunsa kwa ajili ya kumlawiti msanii huyo lakini kwa bahati mbaya fumanizi hilo lilidunda" Alisema mama mmoja ambae aliongeza kusema mabaunsa hao walikuwa wanne.
 


Mwandishi wetu alimtafuta Kinyambe kupitia simu yake ya mkononi aliendelea kusisitiza kuwa hakufumaniwa na wala hajawahi kufumaniwa huo  ni mpango wa kumchafua.


Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Video ya Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM akisema Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania wala Mwenyekiti wa CCM!


TAMKO LA JUMUIYA YA VIJANA KUUNGA MKONO KAZI YA SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CHINI YA KATIBU MKUU NDUGU ABDULRAHAMAN KINANA

“..Chama Cha Siasa chochote duniani hubomoka kutokana na migongano iliyokithiri ya muda mrefu. Uzoefu wa vyama vikubwa vilivyoporomoka umeonyesha hivyo! Chama lazima kidhibiti uchu wa madaraka wa baadhi ya viongozi wake na ndani ya serikali yake...” – Dr Eginald P. Mihanjo

“..Chama cha siasa ni itikadi. Chama cha siasa ni siasa kwa maana halisi ya neno lenyewe siasa –“siasa”. Ni mahali ambapo watu wenye madhumuni mamoja yaliyoainishwa waziwazi hukutana na kuwa kitu kimoja. Chama cha siasa sio mkusanyiko wa “majini dume yenye tamaa”, - majini ambayo yametanguliza mbele tamaa kufa na kupona-tamaa ya kutengeneza pesa au kupata vyeo kwa gharama yoyote! – Dr Bashir Ally

UTANGULIZI:

Hili ni tamko la vijana makini wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuunga mkono juhudi na utendaji wa sekretarieti ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi ikiongozwa na Katibu Mkuu Komredi Abdulrahaman Kinana.

Maneno ya utangulizi yamebeba dhima ya tamko hili, kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vikiwanukuu baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, wakiwatuhumu Viongozi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.

Sisi Vijana tunatambua kuwa tuhuma hizo na maneno hayo ya hovyo yametolewa kwa nia ovu yenye kulenga kuwakatisha tamaa Viongozi hao wa Chama. Tunafahamu kuwa upo mkakati wa kiuhaini ulioandaliwa na kuratibiwa na “mtandao” ndani ya Chama ambao umejipanga kuendesha uhaini huo.

Sisi vijana wa UVCCM tunatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga na kukiimarisha Chama kwa kuisimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake, katika umri wetu hatukuwahi kuona Chama kikiwa karibu na wananchi kwa kufuatilia, kusikiliza na kushiriki katika utatuzi wa kero, shida na changamoto zao kama ilivyo katika kipindi hiki chini ya Comrade Kinana na timu yake. Juhudi hizi ni za kuungwa mkono na kamwe si za kubezwa na mwanaCCM muadilifu, muaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Chama.

Juhudi za kukiimarisha Chama kutoka ngazi za chini, kwa mabalozi ni mkakati bora kuwahi kutekelezwa na Chama, kukirudisha Chama kwa wanachama ni kutimiza lengo la kuundwa kwa Chama hiki, Chama hiki ni cha wanyonge, masikini wa Taifa hili, HAIWEZEKANI matajiri watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema tutakilinda Chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu.

Ni hawa ambao wanabezwa leo ndio wameweza kurudisha Imani ya wananchi kwa Chama, Imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na Chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wan chi hii.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliozunguka kwenda kukutana na wakulima wa Pamba kule mikoa ya Kanda ya ziwa na kumpeleka balozi wa China na kumshawishi kujenga viwanda ili kuboresha manufaa kwa wakulima.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliokwenda Kusini kukutana na wakulima wa Korosho na kushirikiana nao pamoja na bodi kutatua tatizo la Korosho.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio walioibua hoja na kero za wafugaji, walimu na wananchi kwa ujumla, na kuwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanawajibika kwa wananchi walipa kodi wa Taifa hili.

Kupinga mafanikio ya Ziara hizo ni kupinga utetezi wa wanyonge.

Mtu anayebeza ziara hizo na kuwaita Viongozi waliozifanya waropokaji na wahuni wahuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo,hana maadili, asiyekipenda Chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

TAMKO hili limezingatia wosia wa Baba wa Taifa, muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Julius Kambarage Nyerere katika kitabu Chake TUJISAHIHISHE.

“Inapofikia wasimamizi wa Kanuni za Chama wanapigwa vita ya wazi kwa uamuzi wao wa kukisimamia Chama, tafsir yake ni moja tu watu wanaowapiga vita hawakitakii mema chama chetu.”

Imetolewa na Paul Christian Makonda.

Katibu wa Hamasa na Chipukizi.
SOURCE:Jamii forum.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Dahaaa! Wanaume Nchni Zimbabwe waomba msaada polisi kukabili genge la wanawake wababaji.

Imeripotiwa kuwa Idadi ya wanaume wanaobakwa na wanawake huko zimbabwe imekua ikiongezeka kwa kasi kila kukicha na sasa wanaume wanahofia kutembea usiku na vichochoroni.

Mwanaume mmoja anaefahamika kwa jina la Al Bayan amewashtaki wanawake watatu kwa kosa la kumkaba kumpiga na kumbaka kwa zamu hukuwakiondoka na sperm zake katika mji wa Bulawayo.

 Polisi wanasema hiyo ni kesi ya sita ya ubakaji wa wanaume tangu mwaka huu uanze.

mwanaume mwingine anadai kupewa lift na wanawake wawili ambao badae walimpulizia chemiko na alposhutuka ndipo alipogundua kuwa alikua amebakwa na wanawake hao pia wlimwiba simu pamoja na pesa kiasi cha dola 20. 

Pia nchini Zimbabwe kuna imani kuwa sperm za mwanaume zinatumika kufanya mwanamke awe tajiri hatujui ni kwa namn gani.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Tuesday, January 28, 2014

Msanii wa BONGO MOVIE Akutwa amejinyonga Gesti baada ya kuigiza Muvie ya kujinyonga.


MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie afariki dunia kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR  ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.
 
Hapo pichani ni mwili wa marehemu ulivyokuwa ukipakiwa katika gari kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,
 

Chanzo cha habari kiliieleza kuwa msanii huyo alikuwa katika harakati zake za kushoot filamu yake mpya ambayo alicheza kama muhusika mkuu katika filamu hiyo.
Kilichowashangaza wenzake ni kwamba filamu iliisha jana Jumatatu 27/01/2014 na story ilimalizikia Vicktor kufa kwakujinyonga matokeo yake leo alfajiri Victor akakutwa amejinyonga kweli na kuiaga dunia, Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijatambulika.

Ndugu msomaji taarifa kamili na picha za tukio zima la kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka Hospitali na mengineyo fatilia hapa utayapata hivi punde

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Happy Birthday TO YUUUUU! Mhe. January Makamba leo ametimiza umri wa miaka 40


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba leo ametimiza umri wa miaka 40. Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), alizaliwa Januari 28, 1974. GPL inamtakia kila la kheri Mhe. Makamba katika siku yake ya kuzaliwa leo.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Eti Freemason wanadai chao kwenye kanisa la mzee wa Upako:Habari yote hapa chini;

ULE uvumi kwamba baadhi ya wachungaji na maaskofu wa makanisa ya kiroho  nchini wanajihusisha na imani ya Freemason unazidi kushika kasi huku awamu hii ‘rungu’ likimwangukia Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar, Lusekelo Antony ‘Mzee wa Upako’ na kutikisika, Uwazi lina cha kusema.
MINONG’ONO ILIVYOANZA
Madai ya mtumishi huyo kujihusisha na imani ya Freemason yalianza kuenea kwa kasi mithili ya moto nyikani huku baadhi ya watu, wakiwemo watumishi wa makanisa ya Kikristo, wakionesha shaka juu ya uponyaji wa mtumishi huyo kufuatia miujiza ya ajabu ambayo amekuwa akiionesha kwa watu wenye uhitaji wa kiimani.
MATENDO YA SHAKA
Baadhi ya matendo ambayo yamekuwa yakiwatia shaka baadhi ya watu ni pamoja na kitendo cha mchungaji huyo kuwaombea watu wakiwa hawana kitu kabisa lakini baada ya miezi michache hurudi kanisani hapo wakiwa na magari ya kifahari na wakionesha kila dalili ya ukwasi (utajiri).
“Eti unakuta mtu amekwenda kuombewa akiwa hana kitu kabisa (fukara) lakini bada ya miezi michache anarudi akiwa na gari la kifahari, kweli?
“Tena anaonesha kila dalili ya ukwasi, huenda ni kweli kuna nguvu za ziada zaidi ya ile ya kiroho,” walisema baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali ya Kikristo walipozungumza na gazeti hili hivi karibuni.
ALAMA NA VIASHIRIA  TATA
Wakifafanua kwa kina zaidi juu ya wasiwasi wao kwa Mzee wa Upako na miujiza yake, waumini hao walitolea mfano wa baadhi ya dalili na viashiria tata vinavyoshukiwa kuwa ni moja ya utambulisho wa Taasisi ya Freemason.
Wakitaja baadhi ya alama hizo, waumini hao walisema mara nyingi mtumishi huyo akiwa madhabahuni amekuwa akitumia kitambaa kikubwa.
“Kila akiwa  jukwaani au madhabahuni hutumia kitambaa kikubwa kujifutia na kuwagusia anaowaombea hali ambayo huwafanya kuanguka na kupiga kelele hovyo,” walisema.
Mbali na kitambaa, pia walisema Mzee wa Upako amekuwa akionekana na pete zenye picha za ajabu akiwa anahubiri au kutenda miujiza.
MADAI ZAIDI
Baadhi ya waumini hao walisema viashiria vingine ni kitendo cha mchungaji huyo kutotaja neno Mbinguni katika mahubiri yake zaidi ya kusema, ‘Mungu wangu awabariki sana’.
“Mapete yake yana  mapicha ya ajabu sana, yale maalama ya Freemason yapo, pia huwa hawezi kusema Mungu wa Mbinguni, badala yake husema ‘Mungu wangu awatangulie’ au ‘kwa uwezo wa Mungu ninaye mwabudu’ jambo ambalo hututia shaka sana,” walisema Wakristo hao.
WAUMINI WAMBANA
Katika kufuatilia kwa kina sakata hilo, habari zikadai kuwa baada ya mambo kupamba moto waumini wa kanisa lake walianza kumbana mtumishi wao huyo kuhusu uvumi huo huku baadhi yao wakianza kutimkia kwingine.
“Ni kweli zahama hiyo iliwahi kutokea, lakini mambo yalikaa sawa baada ya baba (Lusekelo) kutufafanulia zaidi juu ya madai hayo,” alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
LUSEKELO KIZIMBANI
Baada ya ‘viranja’ wetu kupata taarifa hizo nzito, hivi karibuni  waliamua ‘kukanyaga  lami’ hadi kanisani kwa mchungaji huyo, Ubungo -Kibangu  ambapo licha ya kukumbana na vikwazo mbalimbali walibahatika kukutana naye na kumbana kwa maswali juu ya tuhuma hizo ambapo kwa ‘jasho jembamba’ aliweza kueleza kwa kina:
“Hizo tuhuma zilianza kusikika zamani sana, watu walianza kunituhumu kwenye matumizi ya bendera ya taifa kanisani, nikatoa, wakahamia kwenye kitambaa.
“Jamani natumia muda mwingi sana kusimama madhabahuni. Sasa nikitumia kitambaa (hendkachifu) cha shilingi mia tano itawezekana kweli, natumia kitaulo kidogo kujifutia jasho, sasa inaonekana nongwa.
“Baadaye wakahamia kwenye pete! Mimi ni mtu smart sana (msafi) nimezaliwa mjini (born town) sasa kuvaa pete ni sehemu ya maisha ya mjini sioni tabu, lakini baada ya manenomaneno nilivua na sasa sina,” alisema Mzee wa Upako.
KUHUSU WAUMINI KUTIMKA
“Ni kweli, baadhi waliniuliza nikawajibu, wengine wakaamua kutimka. Unajua mimi nimeanza kumtumikia Mungu kwa miaka thelathini sasa, muumini kuhama kanisa na kwenda kwingine sishangai.
“Lakini wajue kwamba hapa kwangu ni moto mkubwa, super charge, cartapillar, siteteleki, nitazidi kuwaombea na kuwaponya wenye taabu na magonjwa,” aliongeza.
KUHUSU FREEMASON?
“Sijawahi kufikiria hata siku moja kuwa Freemason, kwanza sifahamu hata wanavyopatikana, nimeanza kumtumikia Mungu nikiwa kijana mdogo, mimi si muumini wa dini wala imani yoyote ya kishetani.
“Shetani mwenyewe ananiogopa, sasa hao wanaosema kuwa huwa sisemi Mungu wa Mbinguni, nashangaa, ni lazima kuweka neno Mbinguni? Jamani hao Freemason siwajui, wala siwazuii watu kuniita hivyo, naendelea kulihuburi Neno la Mungu aliye hai,” alisema Lusekelo na kufunga ‘faili’ la mazungumzo na waandishi wetu.

CREDIT:GPL

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Inasikitisha sana!! MESENJA WA DC AMBAKA MTOTO WA DARSA LA KWANZA.!SOMA ZAIDI HAPA


DUNIA inaelekea ukingoni. Mesenja katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani, Mud Yusuph yu matatani kwa madai ya ubakaji wa denti wa darasa la kwanza,10,  (jina linahifadhiwa). 
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya ofisi hiyo, mtuhumiwa huyo (55) alidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwake Kisarawe, Januari 20 mwaka huu.

Siku ya tukio inadaiwa mtoto huyo alikwenda nyumbani kwa mtumishi huyo ambaye ni shemeji yake. Mtuhumiwa ameoa dada wa binti.
 

Mtoto huyo alipofika kwa mtuhumiwa hakumkuta dada yake. Ikadaiwa mtuhumiwa aliitumia nafasi hiyo kumrubuni binti huyo kabla ya kumkamata, kisha akamvutia ndani na baadaye ikadaiwa alimbaka huku sebuleni kwake televisheni ikiwa inafanya kazi. 

Akizungumza na gazeti la GPL hivi karibuni juu ya tukio hilo, binti huyo alisema wakati akifanyiwa kitendo hicho alisikia maumivu makali na kulia, lakini mtuhumiwa alimtishia kumchinja endapo atapiga kelele.

“Baada ya kuniambia atanichinja nilinyamaza, lakini nilikuwa ninasikia maumivu, alipomaliza aliniambia nichukue maji nikanawe, baada ya hapo alinipa shilingi  elfu moja (1,000), nikaenda nyumbani.” 

Mama mzazi wa mtoto huyo, Rehema Shukuru alipozungumza na gazeti hili alisema:

“Siku hiyo mwanangu alikuja nyumbani analia.  Nilipomuuliza analia nini, alinijibu shemeji yake amemfanyia kitu kibaya. Nilipomwangalia sehemu za siri nilikuta uchafu wa manii, ndipo nilipokwenda Kituo cha Polisi Kisarawe kutoa taarifa,” alisema. 

Kwa mujibu wa mama huyo, mtuhumiwa huyo alitafutwa na kupatikana ambapo aliomba msamaha kwa kitendo alichokifanya lakini hata hivyo, polisi walimwweka mahabusu. 

Wakati mtuhumiwa huyo akiwa selo, mtoto huyo alilazwa katika Hospitali ya Wilaya  Kisarawe kwa ajili ya matibabu, lakini katika hali ya kushangaza, siku mbili baadaye mtuhumiwa aliachiwa kwa dhamana na kuiacha familia katika mshangao. 

Jitihada za gazeti hili kumfikia mtuhumiwa huyo ziligonga mwamba baada ya kutompata nyumbani kwake huku ikisemekana hayupo wilayani humo. 

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kisarawe, Happy Ndosi alikiri kupokea taarifa ya mtoto huyo na kusema walimpima Ukimwi na kumpa dawa kama kutakuwa na maambukizi. 

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, SACP Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema taratibu zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa mazingira ya tukio lenyewe.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Mwinjilisti amchinja mkewe mjamzito na mwenyewe kujinyonga huko Bagamoyo.


Bagamoyo
YULE Mwinjilisti wa Kanisa la Angilikana lililopo Kijiji cha Gama Makaani wilayani Bagamoyo, Pwani, Elikia Daniel (35) aliyemuua mkewe Mboni Patrick (28) kwa kumchinja  kikatili naye kujinyonga, simulizi yake inashangaza.


Baada ya mauaji hayo, waandishi wa Uwazi walikwenda kwenye kijiji hicho kilichopo kilomita 100 kutoka jijini Dar es Salaam na kukutana na ndugu, jamaa, marafiki wa marehemu wote sanjari na uongozi wa kijiji.
MWANZO WA MKASA
Wakisimulia kwa masikitiko, wakazi wa kijiji hicho walisema siku ya tukio, Mwinjilisti Elikia na mkewe, Mboni walikwenda msituni kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa wa biashara. Walikuwa wameongozana na mtoto wao wa miaka (12) ambaye jina halikupatikana mara moja.

Baada ya kufika msituni, simulizi inasema, majira ya saa tatu asubuhi, mwinjilisti huyo alimtaka mwanaye huyo kurudi nyumbani kupika.
“Yule mtoto alipika chakula na kukiweka kwenye ‘hotipoti’ kwa ajili ya kuwapelekea wazazi. Alikwenda msituni akiwa ameambatana na mtoto wa jirani ambaye ni rafiki yake.

WAZAZI HAWAPO
“Alipofika msituni, mahali alipowaacha wazazi wake hakuwakuta, akawaita kwa muda mrefu, baba, mama lakini ukimya ulitawala eneo lile.

“Katika juhudi za kuwasaka huku na kule, mtoto alishangaa kuona damu nyingi imetapakaa eneo lile na aliposogea akashangaa kuuona mkono wa mama yake ukiwa umetokeza nje huku mwili wake umefunikwa na magogo kwenye tanuri walilokuwa wakitumia kuchomea mkaa,” alisema ndugu mmoja wa marehemu  Mboni aliyeomba hifadhi ya jina lake.
WATOTO WAKIMBIA KIJIJINI KUSEMA
Simulizi inazidi kuweka wazi kwamba, baada ya kuona hali hiyo, watoto hao huku wakilia walikimbilia kijijini ambapo waliwaambia watu walichokutana nacho msituni.
Wanakijiji walikukusanyika na kwenda eneo la tukio kushuhudia mwili wa mwanamke huyo.

MSAKO WAANZA
Kwa vile wawili hao waliachwa msituni na mtoto wao, wanakijiji waliamini kwamba, Elikia ndiye aliyefanya mauaji hayo, wakaanza kumsaka.
Walitembea umbali mrefu, wakafika mahali na kukuta nguo za mwinjilisti barabarani, waliposogea sehemu yenye miti iliyoshonana ndipo walipouona mwili wa Elikia ukining’inia mtini. Hakuacha ujumbe wowote.

NINI CHANZO?
Akizungumza kuhusu mauaji hayo, mwenyekiti wa eneo hilo, Ali Thabiti alisema kwa jinsi alivyopata taarifa kutoka kwa majirani, chanzo cha mauaji hayo ni fedha za mkaa. Mwinjilisti alikuwa akidaiwa fedha na mkewe lakini alikuwa akimzungusha kumlipa.

Alisema mgogoro wa marehemu hao ulikuwa wa muda mrefu, walishapelekwa mpaka kanisani kusuluhishwa, mwinjilisti alikubali ana makosa na kuahidi kwamba atangemlipa mkewe fedha za mkaa wake wa magunia mia moja alizokuwa akimdai.
“Usiku wa kuamkia siku ya tukio, mtoto alisema alimsikia baba yake akimwambia mama yake kuwa atamuua na kweli akamuua asubuhi iliyofuata,” alisema jirani mmoja.
UNAWEZA KUAMINI HII?
Vyanzo mbalimbali kijijini hapo vilieleza kuwa, mwinjilisti huyo aliwahi kudaiwa kumuua mtu (jina halikupatikana) huko Kigoma kwa kutumia nondo ambayo alimpiga nayo kichwani.

KUMBE MKE ALIKUWA MJAMZITO?
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wakati daktari alipofika kuupima mwili wa marehemu Mboni, taarifa ilitoka kwamba mwanamke huyo alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu wakati anauawa.

NI MAUAJI YA KUTISHA
Mwili wa marehemu Mboni ulikutwa ukiwa na majeraha mengi, kubwa zaidi ni la shingoni kwani mumewe alimchinja kama kuku.

MWINJILISTI AZIKWA NA SANDA YA KIROBA
Baada ya polisi kufika eneo la tukio na daktari kufanya uchunguzi, wanakijiji walifikia uamuzi kwamba mwanamke azikwe eneo hilohilo ulipokutwa mwili wake, mwinjilisti alizikwa chini ya mti aliojinyongea, tena mwili wake ukiviringishwa kwenye kiroba. Wote walizikwa bila majeneza na miili yao iliharibika.

ASKOFU MOKIWA AMKANA MWINJILISTI
Uwazi lilizungumza na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentine Mokiwa (zamani alikuwa askofu mkuu Tanzania) ambaye alikana marehemu Elikia kuwa mwinjilisti wa 



Si kweli. Anglikana hatuna mwinjilisti huyo. Nimesoma kwenye vyombo vya habari kuhusu madai hayo, waandishi hawakuchunguza vizuri,” alisema Askofu Mokiwa.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

M4C jana walikuwa Uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa.

 
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Iringa, katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa jana.


 
Wafuasi wakisikiliza jambo katika mkutano huo.
 

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Monday, January 27, 2014

Habari ya kuudhunisha : Mzee DUDE WA FUTUHI AFARIKI DUNIA


Msanii wa kundi la Futuhi Mzee Dude amefariki dunia Leo mida ya saa kumi na moja jion.
Habari zinasema kuwa alizidiwa jana Jumapili na kukimbizwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Tunatoa pole kwa wote wanaohusika na msiba huu.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

video +picha; Dunia imekwisha , Mtumishi bandia abambwa akizini na mke wa mtu kichakani.


Tafadhali video hii hairuhusiwi chini ya umri chini ya miaka 20.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Raisi Kikwete atua Magole-Dumila, akagua daraja na kuongea na wananchi.

 Helkopta iliyokuja na Rais Kikwete ikitua eneo la daraja la Dumila mkoani Morogoro leo
 
Rais Kikwete akishuka katika helkopta aliyokuja nayo.
 
Rais Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Magole mkoani Morogoro waliokumbwa na mafuriko ambao kwa sasa wanaishi katika mahema yaliyopo Shule ya Sekondari Magole


Rais Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi.
RAIS Dk. Jakaya Kikwete leo ametua kwa helikopta kijijini Magole, Dumila ili kukagua daraja lililoharibiwa na mvua pamoja na kuongea na wananchi wa eneo hilo waliokumbwa na mafuriko yaliyotokea Januari 22, mwaka huu wilayani Mvomero, Morogoro.

CREDIT: GPL

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Mtikisiko mkubwa wazua taharudi jengo la tigo kijitonyama;


Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, akiongea na wanahabari baada ya mtikisiko kutokea katika jengo la Derm lenye ofisi za kampuni ya simu za mkononi ya Tigo lililopo Makumbusho jijini Dar es Salaam leo.
Mtikisiko huo uliwafanya wafanyakazi wa tigo wote wakimbilie nje ya jengo haraka.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Kijana apewa kichapo na mama mkwe kisa kashindwa kumpa bintiye mimba.


Thembelani Dube mkazi wa Nigeria alipokea kichapo kutoka kwa mama mke wake bi. Onzilina Mpala kwa kisa kilicho daiwa kuwa ni kushindwa kupata mjukuu wa pili kwa mke wake, Virginia Ndlovu.
Wanandoa hao wana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 3 na mke pamoja na mama mkwe wana mlaumu Dube kwa ukosefu wa mtoto mwingine.


Ingawa  inadaiwa kwamba Dube ana mtoto wa miaka mitatu mke alilalamika kwa mama yake kuwa mumewe huyo alishindwa kupata mtoto mwingine kwani alikuwa dhaifu katika kitanda na kwahiyo alishindwa kumtia mimba.

Ila Dube alilalamika kwa kusema kuwa mkewe Virginia alikuwa akitembea na wanaume wengine akidai kuwa wao ni bora kuliko yeye na hivyo kumnyima haki yake ya ndoa na ndiyo sababu ya yeye kushindwa kumpa mke wake mimba.

Na ndipo mama mkwe wake alipo kuja na kuanza kunitukana na kunipiga akisema sistaili kuwa na binti yake,Alimalizia kusema Dube.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Aiubuuuu! Mchumba wa mtu anaswa LIVE akijiuza, aliaga anaenda kumsalimia bibi. Duuu



Za mwizi 40: Mchumba wa mtu baada ya kunaswa na OFM akijiuza licha ya kuaga kuwa anakwenda kwa bibi yake. Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya mji kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu ya ngono.

Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni mgonjwa.
Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.

 
Mshangao: Mchumba wa mtu akishangaa baada ya kubambwa na OFM. Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alieleza kuwa kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika viunga vya Kaumba.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.


 
Twendeni: Mchumba wa mtu akiongoza wenzake wanaoshuka kutoka kwenye difenda kuelekea kituoni. “Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za advance ya ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.

 

 
Chini ya ulinzi: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa chini ya ulinzi kituoni. OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
 

Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake. 
 

 

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Kigogo aliyemtosa Wema sepetu amnasa shorti wake wa karibu.Malove nje nje.

 
 Naima Shaa.

NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).
“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement  kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.
 
Wema Sepetu.
NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.
“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.
“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.
“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.
WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.

Tatoo ya Clement mgongoni mwa Naima.
“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.
UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.
Alipoulizwa kuhusu  tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).
“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.
WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.
Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.
“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.
NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.
“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.
“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top