Monday, January 27, 2014

Kijana apewa kichapo na mama mkwe kisa kashindwa kumpa bintiye mimba.


Thembelani Dube mkazi wa Nigeria alipokea kichapo kutoka kwa mama mke wake bi. Onzilina Mpala kwa kisa kilicho daiwa kuwa ni kushindwa kupata mjukuu wa pili kwa mke wake, Virginia Ndlovu.
Wanandoa hao wana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 3 na mke pamoja na mama mkwe wana mlaumu Dube kwa ukosefu wa mtoto mwingine.


Ingawa  inadaiwa kwamba Dube ana mtoto wa miaka mitatu mke alilalamika kwa mama yake kuwa mumewe huyo alishindwa kupata mtoto mwingine kwani alikuwa dhaifu katika kitanda na kwahiyo alishindwa kumtia mimba.

Ila Dube alilalamika kwa kusema kuwa mkewe Virginia alikuwa akitembea na wanaume wengine akidai kuwa wao ni bora kuliko yeye na hivyo kumnyima haki yake ya ndoa na ndiyo sababu ya yeye kushindwa kumpa mke wake mimba.

Na ndipo mama mkwe wake alipo kuja na kuanza kunitukana na kunipiga akisema sistaili kuwa na binti yake,Alimalizia kusema Dube.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top