Thursday, May 29, 2014

Huyu ndie jamaa aliyekodi Ngoma wakati wa TUKIO la KUMFUMANIA MKE wake!

AMA kweli dunia ina mambo na mambo yenyewe ndiyo haya! Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ramadhan Ally, mkazi wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amewashangaza wengi kufuatia uamuzi wake wa kukodi ngoma ya asili kwa lengo la kwenda kumfumania mkewe aliyejulikana kwa jina moja la Asha.

Mwanadada aliyetambulika kwa jina la Asha baada ya kufumaniwa akisindikizwa na ngoma.

Tukio hilo lililofunga mtaa lilijiri asubuhi ya saa 3:14  Jumatatu iliyopita eneo maarufu kwa jina la Sultani baada ya mwanaume huyo kutonywa kuwa, mke wake alikuwa amelala kwa rafiki yake kipenzi, Abdallah Elias.

Baadhi ya wananchi waliobahatika kuwasili katika eneo la tukio walishuhudia mwenye mali akiwashushia kichapo kikali ‘wasaliti’ hao ambapo vurugu zikapamba moto.

Kufuatia hali hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa huo waliamua kutoa taarifa kwa Kamanda Mkuu wa Ulinzi wa Jadi Kata ya Mbuyuni, Aidan Mtimbo ambaye alifika eneo la tukio na vijana wake na kuwasomba watuhumiwa hao msobemsobe huku wakisindikizwa na ngoma hiyo hadi Kituo cha Polisi Kata ya Mbuyuni.

Vijana wakipiga ngoma wakati wa fumanizi la Asha.

Katika hali ya kushangza, nje ya kituo hicho cha polisi baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira walishinikiza watuhumiwa watolewe nje wawafanyie kitumbaya huku baadhi yao wakikipopoa mawe kituo hicho kilichokuwa na askari mmoja aliyevaa nguo za kiraia.

Baada ya vurugu hizo, afande huyo alipiga simu kituo kikuu cha polisi kuomba msaada ambapo askari wa pikipiki walifika na kuwakodia teksi watuhumiwa hadi kituoni.

Mwandishi wetu alifanikiwa kuwahoji wahusika wote watatu ambapo mume wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kama ifuatavyo:

“Huyu mwanamke ni malaya sana, kwanza  nimemtoa kwao Matombo (Morogoro) akiwa na watoto wawili na kila mmoja na baba yake.

“Mimi sikujali hilo, ukipenda bonga penda na ua lake. Miezi mitatu iliyopita aliniambia ana ujauzito wangu, taarifa hizo zilinifurahisha sana. Cha ajabu juzi akaniambia ametoa mimba yangu, nilipomuuliza kwa nini, akasema kwa ujeuri eti hayupo tayari kuzaa na mimi kwa sasa.

“Nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao, jana usiku napokea taarifa kuwa yuko nyumbani kwa rafiki yangu kipenzi, Abdallah Elias.

Polisi baada ya kutinga eneo la tukio kuwanusuru watuhumiwa.

“Ndiyo asubuhi nikakodi ngoma na kwenda, niliwakuta wamelala kitandani.”
Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema:
“Huyu mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia  amefukuzwa na mumewe hivyo anaomba alale kwangu kesho  yaani leo aende kwao Matombo kumbe alisharudishwa kwao toka juzi.”

Naye mwanamke huyo alipohojiwa na paparazi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Huyu mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi wangu ananipiga danadana. Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”

Mume wa Asha, Ramadhan Ally.

Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya amethibitisha kutokea kwa fumanizi hilo kwenye mtaa wake lakini aliwatupia lawama polisi wa pikipiki kwa kupuuza uongozi wa juu wa kata hiyo ambao kwa kushirikiana na walinzi wa jadi walifanikiwa kuwalinda watuhumiwa wao na kufika salama kwenye kituo cha polisi.
habari kamili :: read more...

Wednesday, May 28, 2014

Mkuu wa jeshi aponea chupu chupu ya kifo huko Somalia.

Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuchupu kuuawa mjini Mogadishu.

Hili ndilo shambulio la punde zaidi katika msururu wa mashambulio dhidi ya viongozi wa serikali na rasilimali za serikali nchini humo.Gari lake Jenerali Dahir Aden Elmim lilirushiwa bomu katika barabara kuu karibu na afisi za wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.

Aliponea kwa sababu yeye huendesha mojawepo ya magari machache yaliyo na uwezo wa kudhibiti shambulio la risasi, ambayo yametengewa viongozi wakuu wa serikali hiyo.

Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa japo inafahamika kuwa kundi la Al shabaab limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu.

Mwishoni mwa juma, watu 15 waliuawa katika shambulio lililolenga jengo la bunge la Somalia. Wengine wengi walijeruhiwa wakiwemo wabunge 3.
habari kamili :: read more...

INASEMEKANA MUME WA FLORA MBASHA AMEMBAKA SHEMEJI YAKE MWENYEWE UMRI WA MIAKA 17.

Dar es Salaam.

Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili,  anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo 17.
Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.

Binti huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.
Akizungumza na blog hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani ya gari.

Alisema mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.

Polisi katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na askari wa kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi jana mtuhumiwa huyo alikuwa hajakamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana hakupatikana kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati ya saa nane mchana na saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake akisema bosi wake ana kazi nyingine.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.

Mwimbaji anena
Alipoulizwa jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.

“Of course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused (nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia,” alisema.

Kadhalika, jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa ambaye baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema: “Samahani sana ujue sikusikii kabisa,” kisha alikata simu.
habari kamili :: read more...

MSANII WA BONGO MOVIE RECHO ATAZIKWA KESHO DAR.

Marehemu Rachel Haule 'Recho' enzi za uhai wake.
MSANII wa filamu Rachel Haule 'Recho'  aliyefariki dunia siku ya jana atazikwa jijini Dar es Salamm siku ya kesho badala ya  Songea kama ilivyopangwa hapo awali.
Ratiba ya kuuaga mwili wa marehemu inabaki pale pale siku ya kesho Leaders Club na baadae kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinonondoni.
habari kamili :: read more...

Baada ya Ndikumana kutoeleweka haya Ndio ayafanyayo Irene Uwoya na mijanaume.

Siku kadhaa zilizopita kuliwahi kulipotiwa na kuonesha picha Irene Uwoya akimtomasa sehemu nyeti Msanii mwenzake wa maigizo Haji Adam na kuzua mambo mengi hasa katika mitandao ya kijamii, lakini haikuishia hapo wawili hawa wamekuwa wakionekana pamoja mara kwa mara tena nyakati za usiku na pozi zao zinaonyesha ishara ya mahaba,ndipo swahilitz iliamua kumtafuta Haji Adam lakini hatukuweza kumpata vilevile ilitokea kwa irene uwoya kwani namba yake ilikuwa haipatikani ndipo tulibahatika kupata mawasiliano ya rafiki wa karibu na Irene ndipo akafunguka "Mbona hao wapenzi kitambo sema nyiye mmechelewa kufahamu ukweli tu" alimaliza rafiki huyo
Chanzo:williammalecela.com 

Msami ambae ni staa wa single ya ‘sound track’ amehusishwa na uhusiano wa kimapenzi na Irene Uwoya.

uuuHaya ni majibu ya Msami alipoulizwa juu ya uhusiano na Irene Uwoya>>’Nipo na uwoya kivipi? hizi stori sijui nani kakupa bwana’

Majibu ya mpenzi wa Msami anaitwa Rehema>>’Maswali gani hayo mpigie mwenyewe muulize kifupi yeye ana mambo yake mwenyewe hamna lolote tamaa za vijana wanapotoka wanashawishika na tamaa ya hela, sijui wanajifanya wao meneja,yule mimi kuniacha ni ngumu sana yaani hata apite nani na nani kuniacha mimi hawezi yaani nina uhakika huo na najua mpaka jana nawasiliana nae yaani yule chapa ilale sisikii wivu’

‘Mimi najiamini na najikubali kwamba hata nikitokea hawezi kuongea chochote Msami, hata Uwoya simuogopi kwa sababu staa? maana hata mie staa, hawezi kuwa anammiliki maana kama angekua anammiliki asingekua na ruksa Msami akamwambia nina mwanamke wangu ana hivi na hivi maana hata uwoya mwenyewe ananijua’

‘Yeye mwenyewe anatakiwa kujiheshimu kwanza ajitazame yeye mkubwa halafu lazima ajihesabie katembea na watu wangapi na nasikia taarifa yake kuwa yeye kawaida yake yaani kila mtu mtaani analalamika, anajishusha sana tofauti na wenzake wanaojiheshimu, kwa sababu sio rika lake kwa mtu anayejiheshimu hawezi kufanya hivyo’.

picha: www.makorokocho.co
habari kamili :: read more...

Hii ndo video ya House Girl aliyelazimishwa kufanya mapenzi na Mbwa na Bosi wake Mzungu.

habari kamili :: read more...

Tuesday, May 27, 2014

Majina ya walioitwa katika usaili UHAMIAJI NAFASI ZA KONSTEBO WA UHAMIAJI NA KOPLO haya hapa katika pdf.

Kuona majina hayo bofya hapa
habari kamili :: read more...

Mamen igeni staili Hii kuwafikisha kileleni haraka mashii zenu.

Mimi sio mwigizaji, zaidi ya hapo nilikuwa mtu wa mwisho kwenye maigizo kipindi cha shule ya msingi, ila nina uwezo mkubwa wa kusema "Oooh, hapo hapo.. unanifikishaaa!", mpaka mwanaume akahisi kweli amenifikisha, hata hivyo siko peke yangu wanawake wengi tu wanaigiza wakati wapo wanafanya mapenzi.
Utafiti wa kitaifa wa ngono uliofanywa na chuo cha indiana, ulionyesha asilimia 85% ya wanaume wakisema mara ya mwisho kufanya ngono waliwafikisha kileleni wenza wao, hata hivyo asilimia 64% tu ya wanawake walisema walifika kileleni mara ya mwisho walipofanya ngono, hii inamaanisha ni hesabu ya ajabu hata mtoto wa darasa la pili anajua imekosewa, na inamaanisha asilimia 21% ya wanaume walidanganywa na milio ya kimahaba ya wenza wao na wakaamini kuwa waliwafikisha.
Iwapo tukichukulia na wewe utaki kuwa mmoja wa hao waliodanganywa na mbaya zaidi hawakua na ufahamu wowote kuwa wamedanganywa, waulize wanaume wamekuandalia dalili zinazoonyesha na zitakazokuwa zinakuonyesha iwapo unadanganywa.

        #1; Unamwelewa

Tuweke hivi, "Ooooh, hapo hapo usiitoe... ooh, naisikia mpaka kichwani!", mwanamke huwa anasema hivi akiwa anakandwa miguu yake na maji ya moto baada ya safari ya miguu ya mwendo mrefu, "OH... USI...., JAMA... UNA.... NDIO...., HAPO HA...", hivi ndomwanamke anavyosema ukiwa unashughurika vizuri kitandani, akiweza kuunganisha sentensi nzima na ikaeleweka ujue anakuzuga, maana akifikia mshindo akili yote inakua kama haifanyi kazi vizuri na ikitokea akiwa analia kama kwenye video za ngono wanavyolia, ujue anakusubiri umalize mambo yako aanze kukuelezea shida zake alizonazo, wale wa kwenye video za ngono huwa wana igiza, mwanamke wa kihalisia wa kawaida huwa hawafiki kileleni iwapo mwanaume anatumia nguvu ovyo ovyo bila ya mpangilio na msuguano wowote unaohusisha kinembe.

         #2; Anakubusu bila kuacha

Kwa mwanamke ili afike mshindo, inabidi awe na umakini mkubwa na kuweka hisia zake zote kwenye msuguano na msisimko anaoupata mwilini mwake ili afike mshindo, kubusu na kutekenya hawezi kuvifanya kwa wakati huo ambao anaweka mawazo yote mahala hapo, ukiona unataka kumpiga denda akageukia pembeni ujue mambo ndoyamemkolea vizuri na sio vinginevyo.

        #3; Uso wake unakuwa mzuri

Ulishawahi kujiangalia kwenye kioo wakati uume wako unagombana na mikono yako, najua ulishawahi kujisugua, nani ambae hajawai..., hakuna!, na unaelekea yale mambo kumwagika, unajua usowako unakuwaje?, uso wako unakuwa kama vile unataka kutolewa maisha au kama unataka kulia vile, binadamu wote wako sawa upande wa kihisia, hata wanawake pia!, akiwa na sura nzuri wakati ndo anafika mshindo ujue hapo hakuna!, anatakiwa kuwa na sura ambayo haina mvuto kama anataka kulia na sio awe bado anapendeza kama ndo anaingia harusini.

      #4; Unafanya mapenzi na mpenzi wako kwa stairi ya kimbwa mbwa

Mwanamke kufika kileleni kwa stairi ya kutoka kwa nyuma ni sawa na wewe kufika mshindo huku mwanamke akiwa anakuchzea kwa mikono.
Sijasema haiwezekani, ila inahitaji ufundi mkubwa na dereva inabidi awe anaijua kwa umakini mkubwa njia yake anayopita, ili manbo hayo yaweze kutokea, kwa hio nitakua na wasiwasi kama mwanamke akisema kafika kileleni kwa kutumia hio stairi, mwanamke anauwezo mkubwa wa kufika kileleni iwapo anafanya mapenzi ila yeye ndo yuko juu ya mwanaume kashika msukani, au kwa stairi ya missionary inayoitwa Coital Alignment Technique kwa kifupi The Cat, najua huijui... i gugo(google) na utaiona.

     #5; Ngozi yake inakuwa nyororo na kavu

Mwanamke akiwa amefika kileleni, moyo, presha ya damu na mdundo vyote vinakuja juu ambavyo inamaanisha lazima jasho limtoke kwa aina yeyote ile na mwili unakua na majimaji kwenye ngozi, hii ni moja ya dalili amekwea mlima na kufika kileleni kwa furaha.
habari kamili :: read more...

Jeshi la nchini Nigeria limesema linajua mahali walikofichwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa.

Jeshi la nchini Nigeria limesema linajua mahali walikofichwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa wakiwa shuleni lakini hawawezi kuitaja sehemu hiyo hadharani.

Wasichana hao walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo linadai haliwezi kuwaachia hadi watakapobadilishana wafungwa wao na serikali ya nchi hiyo.
Kwenye kituo cha TV cha Nigeria, imetangazwa kwamba japo imefahamika walipo Wasichana hao ambao bado wanashikiliwa mateka….. majeshi ya Nigeria na mengine yanayoendesha opareshen hiyo hayatotumia nguvu za kijeshi kwenye uokoaji wa wasichana hawa.

Kitendo cha kutekwa kwa wasichana hao kimeibua majonzi makubwa miongoni mwa wazazi na kufanya kuibuka kwa kampeni iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari yenye jina la Bring Back Our Girls ikimaanisha “Rudisheni wasichana wetu”

habari kamili :: read more...

BREAKING NEWS!! MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho,’ amefariki dunia asubuhi hii.

Rachel Haule ‘Recho' enzi za uhai wake.
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho,’ amefariki dunia asubuhi hii. Marehemu amepoteza maisha mara baada ya kujifungua. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
habari kamili :: read more...

Picha chafu za Mke wa kigogo Dodoma hizi hapa.

Picha zake zasambaza baada ya kuchepuka na dent wa udom


habari kamili :: read more...

BINTI ALIYEZIKWA AIBUKIA NYUMBANI KWAO AKIWA MZIMA.


 HOFU ya ushirikina imetikisa Mkoa wa Arusha kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo mwanafunzi wa Chuo cha Kompyuta jiji hapa, Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12, mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, Kata ya Moshono wilayani Arumeru, Arusha kuibuka akiwa hai.

Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12 mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, mkoani Arusha na kuibuka akiwa hai tena.

Binti huyo aliibuka kwao hivi karibuni akiwa mpole na kuwafanya baadhi ya watu, wakiwemo wazazi wake kutimua mbio kwa hofu.
Watu kutoka maeneo

mbalimbali jijini hapa  wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa wazazi wa binti huyo kwa lengo la kumshuhudia kwa vile ndugu walishaamini kuwa, mpendwa wao huyo alishakufa na alizikwa.

Umati wa watu ukiwa katika hali ya mshangao kutokana na tukio hilo.

UWAZI LATIA TIMU NYUMBANI
Baada ya kusikia taarifa hizo, Uwazi lilifunga safari mpaka eneo la tukio na kumshuhudia binti huyo kisha likaenda kwenye kaburi alilozikwa.

Kwenye kaburi hilo, msalaba wenye kuonesha siku yake ya kuzaliwa (1992) na kufa (12, Aprili, 2014) ulikuwa bado umesimama imara huku kaburi lenyewe likionesha dalili ya kutitia kidogo.

BABA MZAZI ASIMULIA
Akisimulia mkasa huo kwa mshangao mkubwa, baba mzazi wa binti huyo, Obed Leiyo alisema:
“Ilikuwa Aprili mwanzoni, binti yangu alitoweka nyumbani  baada ya kurudi kutoka chuoni majira ya saa 2 usiku akiwa amechelewa.

Hili ni kaburi alipozikwa Witness Obeid Leiyo.

Mimi kama mzazi nilimfokea kwa kuchelewa kwake kurudi nyumbani.
“Yeye kwa hasira zake alizunguka nyumba akaondoka muda huohuo na hakurudi kabisa hapa nyumbani.

“Siku iliyofuata tulianza kumtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio, tukatoa matangazo kwenye vyombo vya habari lakini binti yangu hakuonekana.”

TAARIFA ZAFIKA, KAFA
Mzazi huyo aliendelea kusema: “Siku moja tulipata taarifa kwamba kuna mwili wa msichana umeonekana  katika Kijiji cha Bwawani hapahapa Arumeru.
“Mimi pamoja na ndugu wengine tuliamua kwenda katika kile kijiji. Tulipofika tuliambiwa ni kweli mwili wa msichana uliokotwa lakini wananchi wakauzika.”

WAFUKUA KABURI
Baba huyo anaendelea: “Niliamua kwenda Kituo cha Polisi cha Usa River ambako niliomba kibali kwa ajili ya kufukua kaburi na kuutoa mwili ili kuutambua kama ni binti yangu au la!

“Nilipewa kibali, tukafukua kaburi na kutoa mwili. Nilimtambua kuwa ni binti yangu kutokana na alama mbalimbali alizokuwa nazo, ikiwemo rangi kwenye kucha na sehemu ya kushoto ya uso ilikuwa nyeusi kwa sababu aliwahi kupooza.

Witness akiwa na baba yake mzazi, Bw. Obeid Leiyo Mara baada ya kurudi nyumbani akiwa hai.

MWILI WASAFIRISHWA, WAZIKWA
Baba huyo wa Witness alizidi kueleza kuwa waliusafirisha mwili huo hadi nyumbani kwake Moshono na kuandaa taratibu za mazishi ambapo Aprili 23, mwaka huu mwili ulizikwa.

AIBUKA GHAFLA
Hata hivyo, Obed anasema alishangaa siku ya tukio kumwona binti yake huyo akiibuka nyumbani hapo akiwa hai jambo ambalo lilimshangaza na kumfanya akimbie kwanza na baadaye kufanya mawasiliano naye.

BINTI ASIMULIA
Akizungumza na Uwazi, binti huyo alikiri kutoweka nyumbani kwao Aprili 15, mwaka huu na kwenda kusikojulikana.

Alisema hakujua kilichoendelea baada ya kuondoka nyumbani lakini baadaye alibaini kuwa alikuwa katika Kijiji cha Olkokola wilayani Arumeru na alikwenda kwenye nyumba ya mwanamke mmoja asiyefahamiana naye akamuomba maji ya kunywa.

“Nilifika kwenye nyumba moja nikamkuta mama mmoja, nikamwomba maji ya kunywa akaenda kuniletea. Nilikunywa huku amenisimamia, lakini maji yalikuwa machungu sana, nikamrudishia, akanilazimisha ninywe kwa kunisukumia kikombe kinywani. Nilipomaliza nilipoteza fahamu.

“Baadaye nilizinduka, nikaendelea kuishi palepale nyumbani kwa yule mama  lakini sifahamu nilikuwa nafanya nini.

“Juzi ndiyo nikashangaa
kujikuta nimerudi nyumbani, mimi sijui nini kilikuwa kikiendelea,” alisema binti huyo.

MAJIRANI NAO
Majirani kadhaa waliokuwepo nyumbani kwa Obed walilielezea tukio hilo kwamba ni la ushirikina huku wakisema ni jambo la kuogofya ambalo halikuwahi kutokea kijijini hapo kabla.

Wengine walisema kuwa binti huyo alifufuka na wengine walisema alichukuliwa msukule.
“Hili si suala la kawaida lazima kuna ushirikina kwani huyu binti tulishamzika na wazazi wake walimtambua kabisa kuwa ni yeye baada ya

kuambiwa alikutwa amekufa, sasa hebu fikiria tangu tumezika mbona hakuna mtu aliyekuja na kusema na yeye alipotelewa na binti yake halafu cha ajabu hilo kaburi mbona limebonyea? Atakuwa amefufuka,’ alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Amina Liwa.

Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Usa River, Benedict Mpujila amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi unafanyika.

KUMBUKUMBU
Mapema mwaka jana tukio la kishirikina liliibuka katika wilayani Arumeru eneo la Kwa Mrefu ambapo mtu mmoja alidaiwa kudondoka na ungo, muda mfupi baadaye alitoweka na kwenye ungo kubaki mayai na kuku mweupe.
habari kamili :: read more...

Monday, May 26, 2014

HAYA NDIO MAMBO SABABISHA HAMU YA KUFANYA MAPENZ KILA MARA , SOMA HAPA

 Kuna mambo mengi sana ambayo husabisha kuhisi hamu ya kuwa na mwanaume au mwanamke kila mara hapa nitaorodhesha machache yale ya muhimu.

1) Upweke mara nyingi hupelekea sana akili ya mtu kuhama na kutafuta kitu mbadala cha kuweza kujiliwaza na mara nyingi huchagua raha za kimwili kama kufanya mapenzi au kuwa na mwenza karibu.
2) Story za Mapenzi kama vile kusoma vitabu vya mapenzi kuangalia picha zenye mvuto wa kimahaba pia kusikia habari hizo vyote hivi vinaweza kukusababishia hamu kubwa sana ya kufanya mapenzi.
3) Kuzoea sana kufanya tendo hilo na mtu ambaye uko karbu nae, na kisha mtu huyo kuondoka au kutenga nae, hii hali inaweza kukupa shida sana kwani huduma ya karibu tena hauna hivyo utaishia tu kuwa na hamu sana ya tendo hilo na kuanza kuhangaika kutafuta njia mbadala. 4) Pombe na vilevi vingine pia huleta sana hamu ya tendo la ndoa wakati mwengine watu hufikia hata kubaka kwa kushindwa kujizuia.
Haya ndio machache makubwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na hamu ya tendo a ndoa mara. Unaweza kuyaepuka...!!? 
habari kamili :: read more...

Hivi ndivyo bondia Nyilawila alivyomtoa damu Bondia Mbelwa, ulingoni katika Pambano.


Konde Mbelwa akiwa chini baada ya kipigo kutoka kwa Karama Nyirawila hayupo pichani .

Na Richard Bukos
PAMBANO la ndondi kugombea mkanda wa ubingwa wa UBO, kati ya bondia Kalama Nyilawila na Said Mbelwa lililofanyika usiku wa kuamkia jana Jumapili kwenye Ukumbi wa Friends Corner Hotel, Manzese jijini Dar es Salaam, lilikatishwa kutokana na kuibuka varangati.

Karama Nyirawila (kushoto) akimpelekea konde Mbelwa.

Damu ndiyo lilikuwa gumzo baada ya Mbelwa kuchanika kwa madai Nyilawila alimpiga kichwa lakini Nyilawila naye akapigwa chupa na shabiki wa mpinzani wake.

Hali hiyo ilisababisha ngumi hizo ziendelee nje ya ulingo, hata hivyo wahusika wakiwemo wapambe wao, waliwahi na kuwaamua na ndiyo ukawa mwisho wa pambano katika raundi ya sita.
Katika raundi ya tatu, tano na sita, Nyilawila alimsukuma Mbelwa kwa makonde yaliyompeleka chini lakini bondia huyo alisimama na kuendelea.

Raundi la sita ilipoanza Mbelwa alimvurumishia Nyilawila masumbwi mazito mfululizo hali iliyomfanya bondia huyo ajisalimishe kwa kumkumbatia ili kujiokoa lakini katika tukio hilo alimgonga Mbelwa kwa kichwa juu ya jicho na kuanza kuvuja damu.

Mbelwa alilalamikia tukio hilo na kusema ni la makusudi hali ilisababisha waendelee kuzichapa kwa kukamiana zaidi na kuzisahau sheria za mchezo.

Baada ya vurugu.

Katika hali ya kukamiana, Mbelwa alimbana Nyilawila kwenye kamba na kumtupia makonde mazito mfululizo na kumtoa nje ya ulingo na kuamua kumfuata nje ya ulingo na kuendelea kuchapana naye.
 Tukio hilo lilisababisha vurumai kubwa na kusababisha mwamuzi Ruta kuvunja pambano na kukimbia. Mwamuzi huyo na majaji wake wakikimbia hovyo kila mmoja njia yake, gazeti hili lilimkimbiza mwamuzi huyo na kumkamata akitaka kuvuka barabara ya Morogoro kusalimisha uhai wake.

“Hapa hapafai wataniua hawa, twende tukaongelee kule mbele, ona lile kundi kubwa nahisi linatufuata,” alisema Ruta.
“Nimelivunja raundi ya nane lakini tayari Nyilawila alikuwa akiongoza kwa pointi kwa mujibu wa majaji wangu,” alisema mwamuzi huyo.






habari kamili :: read more...

TSHIRT MOKO NDEMBE NDEMBE...STAILI MPYA BAADA YA KANGA MOKO KUEXPIRE...LAANA HII.

 KWA muda mrefu, zilisikika sauti za kupiga vita makundi ya wanawake yaliyosifika kwa kucheza utupu kwa kulowanisha khanga maji maarufu kama Khanga Moko Ndembendembe lakini sasa imeibuka nyingine, inayoitwa Fulana au Tisheti Ndembendembe
 
Uchunguzi wetu wa miezi kadhaa tangu mwaka jana ulibaini kwamba tayari staili hiyo ya uchezaji wa muziki wa mwambao kwa kulowanisha tisheti laini nyeupe kwa maji na kusababisha chuchu kuonekana sawia, inazidi kushika kasi kama moto wa kifuu Bongo.


Ilibainika kuwa staili hiyo ambayo ilianzia Pwani ya Kenya, sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini hasa kwenye ngoma maarufu za ‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana.

Habari zilisema kuwa katika uchezaji huo, sharti ‘nido’ ya mrembo iwe saa sita ili kuwavutia na kuwaridhisha wanaume kimahaba ambao kazi yao huwa ni kuwatuza fedha baada ya kufurahishwa kwa kutazama uchezaji huo na wengine kuondoka nao kwenda kuvunja amri ya sita.

Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa.

Mamlaka na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa nguvu zote kwani huo ni mwanzo mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania na ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU)
habari kamili :: read more...

Bingwa wa michezo ya Olympiki mbio za mita mia nane David Rudisha wa Kenya ametangaza rasmi anarudi uwanjani.

Bingwa wa michezo ya Olympiki mbio za mita mia nane David Rudisha wa Kenya ametangaza rasmi anarudi uwanjani Mei tarehe 31 mwezi huu katika mbio za Golden League huko Oregon, Marekani, baada ya kutokimbia kwa muda wa mwaka mmoja akiuguza jeraha la goti la kulia.

Rudisha, ambaye pia anashikilia rekodi ya dunia, amezungumza na John Nene huko Iten eneo la bonde la ufa wakiwa mazoezini pamoja na kusema sasa yuko sawa na tayari kukimbia tena.
habari kamili :: read more...

JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA.


1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.


2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.

3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation.

Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.

4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.

5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.

6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu ‘enjoyable’ na sio tendo ‘mechanical’ kwa ajili ya kutafuta mtoto.

Kama hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu. Natumaini uzi huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto.
habari kamili :: read more...

ISIKUPITE : shuhudia shindano la kunyonyana denda la wanawake na vituko vyake..!!


 Lucy, Salama na Amina wakishindana kunyonyana ndimi ilikuwa kama movie vile
 
Raheri na Suzy wakiwa kwenye hisia kali za kunyonyana ndimi hadi mshindi apatikane.

Hawa Xdeejayz haikupata majina yao nao pia wakiwa kwenye kwenye shindano hilo.


Jackline na Neema kama wanavyoonekana


 
Angel na Monalisa kulia wakiwa kwenye bize kuhakikisha mshindi anapatikana bila upendeleo
Na Mwandishi wa Xdeejayz- Iringa

Hakika ni ukweli kwamba taifa letu la tanzania linakwenda kuangamia kwa kwani vijana wengi tunaowategemea kuwa viongozi wa kesho na tegemeo kwa tafia hili wameendelea kuonesha tabia za ajabu kiasi cha kuogopesha.
Wasichana kadhaa wanaosoma kwenye chuo kimoja maarufu mkoani Iringa jina linahifadhiwa wamenaswa na kamera za Xdeejayz wakifanya part ya kushindana kunyonyana mate hadi mshindi kupatikana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopenya hadi kwenye part hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi mmoja wa Hotel maarufu Mkoani humo inayomilikiwa na mfanyabishara aliyefahamika kwa jina la Pongezi Sanga iitwayo Vavene Hotel wasichana hao walikuwa zaidi ya kumi.
Hata kwa kweli hatari kubwa sana kwa matukio ya wakina wanafunzi hao wa vyuo kwani kiukweli taifa letu liko hatarini kukosa viongozi baadae kwani kwa vitendo hivi hakika hapo hakuna kiongozi mtarajiwa.
Msomaji mmoja wa Blog hii aliyejitambulisha kwa jina la Nyakulinga alisema " Yani hii ni hatari upuuzi huu kweli tutategemea kupata mawaziri hapa au rais wa nchi? Hawa viongozi tuliokuwa nao sasa hawakuwa hivi ndiyo maana wanatuongoza lakini kama wangekuwa hivi na wao leo hii tusingepata viongozi bora" Alisema mzee huyo hadi machozi kumtoka kwa uchungu.
Katika shindano hilo msindi alikuwa Salama na Suzy ambao ambao walijinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili na nusu.
CREDIT: XDEEJAYZ TANZANI.
habari kamili :: read more...

HAYA NDIO MATUSI ALIYOMWAGIWA NISHA KISA, MWANAUME

Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’
Matusi! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutukanwa matusi ya nguoni na mwanadada anayejulikana kwa jina la Muna Alphonce kisa, kikidaiwa ni mwanaume.
Habari ya mjini ilieleza kwamba Muna ambaye ni mke wa mtu aliporomosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini huku akimtoa kasoro mbalimbali Nisha na kumweleza kuwa hakuwahi kufikiria wala kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake wa sasa kwani ana mume na familia.
“Sina uhusiano na mwanaume wa Nisha ila kuna siku moja alinipigia simu na kujitambulisha kwangu kwamba anahitaji tufanye biashara kwani anafanya biashara ya magari lakini nikampotezea, akarudia tena mara ya pili pia nikampotezea lakini sasa nashangaa Nisha kudai ninamtaka mwanaume wake. Wewe nisha nikome kabisa,” alisema Muna.
Baada ya kuzinyaka habari hizo na matusi hayo ya nguoni, gazeti hili lilimtafuta Nisha na kumuuliza kulikoni ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi sigombei mwanaume na mtu. Mwanaume wangu ninampenda na yeye ananipenda japokuwa watu wanazungumza mengi,” alisema Nisha.
habari kamili :: read more...

Picha kali za mama majanga Snura hizi hapa; kweli Dunia imekwisha.







habari kamili :: read more...

'Usife moyo mpendwa na mimi pia ni mkimbizi' ni maneno ya wakimbizi wa kisomali.


 Vijana wakimbizi wanaoishi katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, nchini Kenya, Dadaab wamewatumia barua za kuwapa matumaini watoto wanaokumbwa na vita nchini Syria, ambao wamelazimika kutoroka vita na kukimbilia nchi jirani.

Wakimbizi hao wanaishi Dadaab Kaskazini mwa Kenya. Ni makao kwa wakimbizi 400,000 wengi wao waliotoroka vita, njaa na ukame nchini Somalia.
Shirika la misaada la kimataifa la Care International, ambalo hutoa misaada kwa wakimbizi hao, liliandaa mpango wa kuandikiana barua kati ya watoto hao na wale wa Syria wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Amman nchini Jordan.

Barua zao ni za ujumbe wa matumaini , kuwapa moyo na ushauri wenzao wanaoishi katika mazingira sawa na wao. Wanawaita dada na ndugu zao.

Wengi wanawaasa kuhusu muhimu wa kusoma na kupata elimu wakiwa kambini.

''Mimi ni mkimbizi tu kama wewe''

Hibo Mahamed Dubow

''Nina uhakika kuwa ukisoma na kujitahidi maishani , utafanikiwa,'' ndio ujumbe wake Hibo Mahamed Dubow. "Cha mwisho ninakushauri kuwa usipoteze matumaini kwa sababu umekuwa mkimbizi kwa miaka mitatu pekee. Nini maoni yako kuhusu watu ambao wamekuwa wakimbizi kwa miaka 20?''

Ujumbe wake Hibo

''Kuweni mashujaa na marais wa sasa''

Dahir Mohamed aliandika barua ya matumaini

"Wapendwa dada zetu na kaka zetu, someni kwa bidii shuleni na muwe marais wapya wa Syria,'' alisema Dahir Mohamed.

Ujumbe wake Dahir Mohammed

''Tunahisi kama nyinyi tu''

Abshir Hussein aliandika ujumbe wa matumaini kwa wakimbizi wenzake

"Tunawaombea Mungu awape maisha mema na kwa msaada wake mtaweza kupata amani katika nchi yenu kwa sababu tunahisi tu kama nyinyi,'' ndivyo aliandika Abshir Hussein.
Watoto wa Syria nao pia walijibu.

Watoto wa Syria walipokea barua zao na picha. Picha hii ni ya Zakariye Mohamed akipokea barua yake pamoja na picha


Barua hizo zilipokewa vyema kwa mujibu wa shirika la Care International, na sasa wanaandika majibu yao kuwatumia watoto wa kambi ya Dadaab.
habari kamili :: read more...

Thursday, May 1, 2014

The Specia one aambuliwa na Atletico Madrid uwanjani kwake sasa kakosa vyote yaani uefa na EPL.


Tabia ya kocha wa Chelsea kucheza mpira wa Kupaki na kufanya mashambulizi ya kushitukiza yaani "Anti' football"imeshindwa kufua dafu Jana baada ya vijana wa Atletico Madrid kulishambulia lango la Chelsea kama Mbwa mwitu na kufanikiwa kuzamishwa magoli 3 kwa 1.

Ilikuwa katika dakika ya  36′ Fernando Torres alipachika bao la kwanza kwa Chelsea na kumfanya kocha wao Jose Mourinho kuanza kuwaamasisha wachezaji wapaki benk akizani mambo yatakuwa kama kwa Liverpool.

Baada ya Atletico kumgundua kaanza mchezo huo usiokubalika hata na Sepp Blatter basi hawakuwa na la kupoteza il kucheza kwa mashambulizi ya haraka na kasi kubwa kama mbwa mwitu aliye na njaa kali wanavyoshambulia jambo lililowazesha kupata mabao matatu kupitia kwa  Adrián 44'
 Diego Costa 60' (PG),Arda Turan 72' .

Kwa matokeo hayo Chelsea watakosa Makombe yote msimu huu yaani UEFA na lile la ligi kuu England EPL licha ya kumwaribia Liverpool harakati hizo.
Kucheki Video za magoli  Bofya hapa

Fainali UEFA sasa ni kati Atletico Madrid VS Real Madrid.
habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top