
Konde Mbelwa akiwa chini baada ya kipigo kutoka kwa Karama Nyirawila hayupo pichani .
Na Richard Bukos
PAMBANO la ndondi kugombea mkanda wa ubingwa wa UBO, kati ya bondia Kalama Nyilawila na Said Mbelwa lililofanyika usiku wa kuamkia jana Jumapili kwenye Ukumbi wa Friends Corner Hotel, Manzese jijini Dar es Salaam, lilikatishwa kutokana na kuibuka varangati.

Karama Nyirawila (kushoto) akimpelekea konde Mbelwa.
Damu ndiyo lilikuwa gumzo baada ya Mbelwa kuchanika kwa madai Nyilawila alimpiga kichwa lakini Nyilawila naye akapigwa chupa na shabiki wa mpinzani wake.
Hali hiyo ilisababisha ngumi hizo ziendelee nje ya ulingo, hata hivyo wahusika wakiwemo wapambe wao, waliwahi na kuwaamua na ndiyo ukawa mwisho wa pambano katika raundi ya sita.
Katika raundi ya tatu, tano na sita, Nyilawila alimsukuma Mbelwa kwa makonde yaliyompeleka chini lakini bondia huyo alisimama na kuendelea.
Raundi la sita ilipoanza Mbelwa alimvurumishia Nyilawila masumbwi mazito mfululizo hali iliyomfanya bondia huyo ajisalimishe kwa kumkumbatia ili kujiokoa lakini katika tukio hilo alimgonga Mbelwa kwa kichwa juu ya jicho na kuanza kuvuja damu.
Mbelwa alilalamikia tukio hilo na kusema ni la makusudi hali ilisababisha waendelee kuzichapa kwa kukamiana zaidi na kuzisahau sheria za mchezo.

Baada ya vurugu.
Katika hali ya kukamiana, Mbelwa alimbana Nyilawila kwenye kamba na kumtupia makonde mazito mfululizo na kumtoa nje ya ulingo na kuamua kumfuata nje ya ulingo na kuendelea kuchapana naye.
Tukio hilo lilisababisha vurumai kubwa na kusababisha mwamuzi Ruta kuvunja pambano na kukimbia. Mwamuzi huyo na majaji wake wakikimbia hovyo kila mmoja njia yake, gazeti hili lilimkimbiza mwamuzi huyo na kumkamata akitaka kuvuka barabara ya Morogoro kusalimisha uhai wake.
“Hapa hapafai wataniua hawa, twende tukaongelee kule mbele, ona lile kundi kubwa nahisi linatufuata,” alisema Ruta.
“Nimelivunja raundi ya nane lakini tayari Nyilawila alikuwa akiongoza kwa pointi kwa mujibu wa majaji wangu,” alisema mwamuzi huyo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment