Saturday, September 20, 2014

YANGA SC YAPIGWA 2-0 JAJA AKOSA PENALTI MOROGORO.

Mchezaji wa timu ya Yanga, Mrisho Ngassa akimtoka mchezaji wa Mtibwa Sugar (Picha na maktaba).
YANGA SC imeanza kwa kipigo cha mabao 2-0 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro mshambuliaji Genilson Santana ‘Jaja’ akikosa penalti.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa, Dominick Nyamisana wa Dodoma, aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Milambo Tshikungu wa Mbeya, hadi mapumziko tayari Mtibwa Sugar walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Mussa Hassan Mgosi dakika ya 16 aliyemalizia pasi ya kichwa ya Ame Ali na kumuwahi kipa Deo Munishi ‘Dida’ aliyetokea vizuri kutaka kudaka.

Mfungaji wa bao la pili la Mtibwa Sugar ni Ame Ali dakika ya 82 kipindi cha pili.
Yanga SC: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46.

Matokeo mengine kwenye ligi hiyo ni kama ifuatavyo: Stand 1-4 Ndanda, Azam 3-1 Polisi Moro, Prisons 2-0 Ruvu Shooting, Mgambo 1-0 Kagera, Mbeya City 0-0 JKT Ruvu


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top