Saturday, September 20, 2014

DIAMOND AZINGUA TENA; ASHINDWA KUTOKEA KWENYE SHOW LONDON.

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.

Kwa mara nyingine tena, mashabiki wa Diamond Platnumz wameshindwa kumuona akitumbuiza licha ya kumsubiria hadi saa 10 Alfajiri.

Awamu hii imetokea jijini London, Uingereza katika show aliyoitangaza kwa kiasi kikubwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Tofauti na Stuttgurt, Ujerumani ambako mashabiki walifanya uharibifu mkubwa, mashabiki wa London waliamua kuwa wapole tu na kurejea majumbani mwao na hasira walizozimeza vifuani.

Chanzo cha Diamond kutotumbuiza kwenye show hiyo kinaonekana kuwa ni kile kile kama cha Ujerumani wiki kadhaa zilizopita yaani promota kushindwa kumlipa fedha yake.

Staa huyo hakuchelewa kumtupia lawama promota wa show hiyo, DJ Rule.
 Akiweka picha ya promota huyo kwenye Instagram, Diamond ameandika: Tafadhali ndugu zangu wa UK!!!….kuweni makini sana na promoter huyu (Victor – Dj Rule) mnaposikia kaandaa show, party au hafla yoyote…ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwa sababu ni tapeli…. si unajua aisifiae mvua imemnyeshea… basi miye nimeloa kabisa.”


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top