Friday, September 12, 2014

OKWI: YANGA WAENDE FIFA, CAS WATANISIKIA KWENYE BOMBA.


Mshambuliaji mpya wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi.

Na Hans Mloli

SIKU chache baada ya Yanga kutangaza kuwa na mpango wa kwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kumshitaki mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, mchezaji huyo ameibuka na kusema: “Hata Yanga waende kushitaki wapi, mimi sina wasiwasi hata kidogo.”

Yanga imeamua kuchukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF ya kumuidhinisha Okwi kuitumikia Simba huku ikidai kuwa bado ana mkataba na Wanajangwani hao.

Okwi aliulizwa swali juu ya sakata hilo katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Boko Veterani, juzi ambapo alisema kwa ufupi:

“Mimi sasa hivi sitaki tena kuwazungumzia hao Yanga, nipo Simba na nina furaha kuwa hapa, kama wanakwenda Fifa hata wafike mpaka Cas (Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo) watajua wenyewe lakini sidhani kama huko kunaweza kubadili chochote, waende tu watajua wenyewe.”


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

AIBU:DADA MREMBO MTOTO WA KIGOGO AANIKA PICHA ZAKE ZA UTAMU.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top