TEDDY Omary John (22), mkazi wa Tegeta jijini Dar amejikuta akihenyeshwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumchoma na kumjeruhi mtoto Magdalena Elisha (10) na kitu chenye ncha kali mapajani na kumsababishia maumivu makali.
Teddy Omary John (22), mkazi wa Tegeta jijini Dar anayetuhumiwa kumsulubu mtoto, Magdalena Elisha.
Imedaiwa kuwa, mtuhumiwa ambaye alikuwa akiishi na binti huyo kama mfanyakazi wake wa ndani (hausigeli), kwa sababu ambazo hazikufahamika alimchoma na kitu chenye ncha kali Magdalena pamoja na kumchoma na mshumaa.
Katika kesi hiyo, Teddy alipokuwa akihojiwa, aliyakana mashtaka ya msingi ambapo mahojiano baina ya hakimu na mtuhumiwa yalikuwa hivi:
Teddy Omary John akiwa mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.
Hakimu: Wewe ni mkazi wa Tegeta?
Teddy: Ndiyo.
Hakimu: Mnamo tarehe 30, Julai ulikuwa Mbezi Beach jijini Dar?
Teddy: Ndiyo.
Hakimu: Bila uhalali ulimchoma na kumkwaruza Magdalena Elisha na kitu chenye ncha kali?
Teddy: Si kweli.
Mtuhumiwa Teddy akirudishwa kizimbani chini ya ulinzi mkali.
Hakimu: Kwa mara ya kwanza ulipokamatwa na kuhojiwa na polisi ulikiri kosa lako?
Teddy: Si kweli.
Is Agatha Atiti A Hottest TV Personality In EAST AFRICA? ……..Check Out Some Of Her Sexy Photos.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 22, mwaka huu itakaposikilizwa tena katika mahakama hiyo na mtuhumiwa alirudishwa kizimbani kusubiri taratibu za dhamana ambayo ilikuwa wazi.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment