MWENYEKITI wa zamani wa Yanga ambaye yupo kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Imani Madega, amefunguka juu ya kilichotokea kuhusu kesi ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Madega ambaye anajulikana kwa kuwa na misimamo mikali, amefunguka kuwa maamuzi yaliyotolewa na kamati yake ambapo na yeye alikuwemo siku ya hukumu ya kesi hiyo, ni sahihi na kusisitiza kuwa hakuna tatizo kisheria kwa Okwi kuichezea Simba baada ya kuonekana Yanga ilikiuka mkataba wake na Mganda huyo.
OKWI: YANGA WAENDE FIFA, CAS WATANISIKIA KWENYE BOMBA.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo jana ofisini kwake, Posta jijini Dar es Salaam, baada ya kuwepo malalamiko ya chini kwa chini kuwa aliihujumu Yanga kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.Madega ameliambia gazeti hili kuwa, licha ya kuwa yeye ni mwanachama halali wa Yanga, lakini kutokana na dhamana kubwa aliyopewa katika taifa, aliuweka pembeni uanachama wake na kufanya kazi aliyopewa katika kutoa maamuzi sahihi juu ya sakata hilo la Okwi.
“Mimi nilishangaa Yanga kuandika barua na kuipeleka TFF kudai eti hawana imani na mimi kwa kuwa nina kesi na Manji. Najua wanataka kunigombanisha na wanachama wa Yanga.
“Sitaki kuzungumzia sana suala hilo kiundani kwa sababu limeshamalizika na maamuzi yameshatolewa, kikubwa ni kwamba sitapinga maamuzi yaliyotolewa na kamati yangu kwa sababu ni maamuzi sahihi na kila kitu kipo wazi.
“Niliweka pembeni uanachama wangu wa Yanga na kufanya kazi niliyopewa kwa manufaa ya taifa zima, lengo ni kuendeleza soka nchini.“Ukiisoma barua waliyoandika kutokuwa na imani na mimi ni wazi ililenga ugomvi binafsi kati ya Manji na mimi na siyo klabu, ndiyo maana TFF iliamua kutupilia mbali pingamizi hilo baada ya kuonekana hoja zao hazina mashiko.
“Ninaomba kuwaambia Wanayanga wote kuwa niliondoka Yanga nikiwa sina kinyongo na ugomvi na mtu yeyote, waelewa na walijue hilo,” alisema Madega ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment