
Staa wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa na vituko, Aunt Ezekiel (katikati) akiwa karibu na dansa wa Wasafi Classic, Moses Yobo.
Aunt alinaswa akiwa na mnenguaji wa Wasafi Classic, Moses Yobo anayepiga mzigo chini ya Nasib Abdul ‘Diamond’ katika shoo ya Fiesta iliyofanyika jijini hapa katika Uwanja wa CCM Kirumba, wikiendi iliyopita.
PICHA NA VIDEO ZA SHILOLE AKIWA MZIWANDA KITANDANI ZAVUJA MTANDAONI, JIONEE MWENYEWE HAPA.
Awali, katika gazeti hili, toleo la wiki iliyopita, tuliripoti habari ya Aunt kufanyiwa vurugu nyumbani kwa Wema na mke wa Yobo aliyekuwa na timu yake.
Moses Yobo akiongoza kikosi cha unenguaji cha Wasafi Classic jukwaani.
Baada ya habari hiyo kutoka, Aunt aliibuka na kusema kuwa, hana uhusiano wa kimapenzi na Yobo lakini kwa sababu amezushiwa, akaahidi kujiweka karibu na kumfanyia mitego ili atoke naye kweli ndipo afanyiwe vurugu ya halali.

Moses Yobo akiwa na familia yake.
Paparazi wetu baada ya kuona hali na ukaribu huo alimfuata Aunt ili kujua kama kweli ameamua kutekeleza azma aliyoitangaza, lakini akaruka kimanga.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment