Monday, August 25, 2014

Mh.Mwigulu Nchemba AVUA SUTI NA KUTOA HUDUMA YA KWANZA KWA MAJERUHI .



 Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.

Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.
 
Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo.Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.

Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Roli Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.

Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.

JOHARI ATOA SOMO LA UZAZI.


Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo

Nchemba alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.

Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongea sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi zao.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

ISSUE ZA MADAWA YA KULEVYA: DIAMOND KIMENUKA MBAYA; NZOWA ASEMA AMA ZAKE AMA ZAO.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top