KOCHA Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, amemvaa kocha wa Simba Patrick Phiri na kumuomba urafiki huku akimtangazia vita hadharani.
Simba na Yanga zote zipo Zanzibar zikijiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na makocha hao wenye viwango vya hali ya juu, walikutana jana kwenye Uwanja Amaan, wakati Yanga ilipokuwa ikiivaa Shangani kwenye mechi ya kirafiki, kabla ya Simba nao kuvaana na KMKM saa 2:30 usiku.
“Habari bwana, mambo yanasemaje, naomba tuwe marafiki mimi na wewe. Lakini tukiwa uwanjani kwenye dakika tisini itakuwa vita kali na urafiki tutauweka pembeni,” alisema Maximo huku Phiri akimsikiliza kwa umakini wa hali ya juu.
Kuonyesha kuwa Phiri amekubaliana na kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars, alikuwa akitingisha kichwa kila kocha huyo alipokuwa akizungumza naye.
Hii ni mara ya kwanza makocha hao wanakutana baada ya wote kuingia mikataba na timu zao miezi michache iliyopita.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment