Monday, August 11, 2014

HIVYO NDIVYO MWIGULU NA RIDHIWANI WALIVYOMALIZA KAZI UWANJA WA TAIFA: YAANI NI FULL MZUKA 100%.


KWELI raha jipe mwenyewe! Usemi huo ulidhihirika wikiendi iliyopita ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini (Night of Hope) ambapo wabunge mashabiki wa Yanga walikipiga na wabunge mashabiki wa Simba na kutia fora kwa kushangiliwa wakati wa mtanange huo.

Katika mchuano huo, wabunge wa Yanga waliwagaragaza wa Simba kwa mabao 3-2 hali iliyosababisha uwanja ulipuke kwa kelele za kushangilia kutoka kwa mashabiki na wapenzi halisi wa Yanga waliokuwepo  uwanjani hapo.


Mbunge za Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete (kulia) akiwa uwanjani.

Kama vile hiyo haitoshi, baada ya kipyenga cha mwisho, wabunge wa Yanga walipanda mzuka na kuanza kuuzunguka uwanja wakisherehekea ushindi wao.

Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba akiwa na mshabiki wao mkubwa kwa upande wa Yanga.

Wabunge waliotia fora zaidi kwa kushangilia huku wakionesha hisia kali ni Mbunge za Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete ambaye baada ya ushindi huo alikimbilia kwa mashabiki wa timu hiyo na kuvua jezi yake ya juu na kuwatupia, hali hiyo iliyomfanya kubaki tumbo wazi.

Ridhiwani Kikwete akirusha T-shirt yake kwa mashabiki wa timu yake.

Naye Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alikuwa sanjari na Ridhiwani ambapo yeye aliwarushia mashabiki wake ‘skafu’ aliyokuwa amejifunga shingoni, hali ambayo ilimfanya shabiki mmoja kuchomoka alikokuwa na kumfuata mheshimiwa huyo uwanjani na kuungana naye kushangilia.

Wakati huo, shabiki huyo alikuwa amevua shati na kuonekana kutoamini macho yake kwani kila wakati alikuwa akipiga magoti na kumshika miguu mheshimiwa huyo.

Baadhi ya wabunge wa Simba waliochezea kichapo kutoka kwa wabunge wa Yanga.

Matukio ya wabunge hao yaliwafurahisha mashabiki waliokuwa uwanjani hapo na shangwe kuwa kubwa kupindukia.

“Jamani sijui niseme nini, najiona kama naota hivi kwa sababu nampenda sana Mwigulu na leo nimemuona na nimemshika na kushangilia naye.

Mwanadada kutoka Nigeria, Yemi Alade alikonga nyoyo za mashabiki wake.

Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti kwa wabunge wa Simba ambao baada ya kipigo hicho, walianza kulalamika kuwa wamehujumiwa na refarii wa mchezo huo, Othman Kazi.

ANGALIA PICHA ZAIDI DIAMOND PLATINUMZ NA MADANSA WAKE WAKIFANYA KUFURU JIJINI MWANZA.

  Kwa upande wa muziki, mwanadada kutoka Nigeria, Yemi Alade aliwakonga nyoyo mashabiki na baadaye akakiri kwamba alifikiri itakuwa ni shoo ndogo, kumbe ni kubwa kiasi hicho, akaeleza jinsi alivyofurahi na kutamani kualikwa tena Tanzania.



Bonyeza Like HAPO JUU USHINDE ZAWADI YA BAHATI NASIBU WAWEZA SHINDA HADI MILLION MOJA. 

ISOME NA HII

DADA YAKE DIAMOND NAE AANZA KUUZA SURA MITANDAONI MCHEKI HAPA.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top