Tuesday, August 19, 2014

CHADEMA YAKANUSHA KATU KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANGOSI.


Mkurugenzi  wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari.

Baadhi ya viongozi wa Chadema kutoka kushoto ni Ofisa Habari, Tumaini Makene, Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika, Ofisa Mwandamizi Mafunzo na Uendeshaji, Mohamed Mtoi, na mwenye gwanda ni Katibu Mtendaji, Ofisi ya Katibu Mkuu, Victor Kimesera.


Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Chadema.

Jengo la makao makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni, Dar.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekana shutuma zilizoelekezewa kwao kuwa wanahusika na kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Mhe. John Mnyika, ameeleza kuwa hawahusiki na mauaji hayo bali ni propaganda zinazoenezwa ili kuwasahaulisha wananchi juu ya suala la katiba linaloendelea.

Mnyika alieleza kuwa wanaoeneza habari hizo ni wale ambao wanataka kuizuia Chadema na Ukawa kwa ujumla kuendelea na harakati za kupigania katiba ya wananchi ikiwemo kufanyika maandamano ya kitaifa iwapo Rais Kikwete hataingilia kati kulisimamisha zoezi la katiba mpya.
 


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU ROSE MUHANDO AFIKISHWA POLISI KWA KUPOKEA PESA YA KUPIGA SHOO NA KUINGIA MITINI.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top