"Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na amekupa maandalizi mazuri. Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema mtaalamu huyo.
Ingawa tendo la ndoa lisipofanywa kwa kuzingatia kanuni na
taratibu, sambamba na umakini, linaweza kusababisha maradhi, lakini kwa
wanandoa, tendo hilo linatajwa kuwa na manufaa mengi kiafya tofauti na
faraja ya kawaida iliyozoeleka kwa wengi.
Imefahamika kuwa tendo hili likifanyika ipasavyo
husaidia kuondoa msongo wa mawazo, maradhi ya moyo, maumivu ya kichwa
yasiyokoma na kupunguza kasi ya saratani ya tezi dume.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya
Tiba Muhimbili (Muhas), Dk Yahya Kishashu anasema inategemea tendo
linafanywa na nani na mhusika yupo kwenye mazingira gani.
“Kwa mfano, tendo la ndoa linaondoa msongo wa
mawazo iwapo unayetenda naye unampenda na amekupa maandalizi mazuri.
Sidhani kama alimradi utende hilo tendo na yeyote litakusaidia,” anasema
mtaalamu huyo.
Mazoezi
Si hivyo tu, utafiti uliofanyika Canada hivi
karibuni umebainisha kuwa kufanya tendo la ndoa kwa kipindi cha dakika
25 kwa wanamume kunachoma kalori 100 na kwa wanawake kalori 69.
Tendo hilo likifanyika kwa nusu saa, linaweza
kupunguza kalori za mwili kuliko kutembea kwenye mashine ya mazoezi ya
‘treadmill’.
“Ni sawa na kucheza mpira wa tenisi au kutembea
ukipanda mlima kwa dakika 20 au kucheza gofu kwa kasi kwa dakika 33 au
zoezi la yoga kwa dakika 40,” sehemu ya utafiti hiyo inasema.
Utafiti huo wa Canada ulishabihiana na kampeni
iliyofanywa na Taasisi ya Moyo ya Uingereza ambayo ilisema kuwa dakika
30 za tendo la ndoa kwa siku ni muhimu kama mazoezi ya kutembea kwa
mashine.
Kwa undani zaidi utafiti huo ulichambua na kusema kuwa, tendo la ndoa, lina manufaa kwa moyo na mapafu.
Kama ungependa kusoma habari hii kiundani basi tembelea http://www.mwananchi.co.tz/Tendo-la-ndoa--Tiba-mbadala-ya-maradhi-ya-moyo--ubongo-/-/1596774/2196600/-/3p5i0c/-/index.html
kama huwezi andika url hiyo basi bofya hapa
CREDIT:MWANANCHI.
Tiba kwa moyo, mapafu na ubongo
Inaelezwa kuwa tendo la ndoa, linasaidia kuondoa msongo wa mawazo hivyo kupunguza hatari ya maradhi ya moyo.
Si hivyo tu, bali tendo hilo husaidia mapafu kufanya kazi yake vyema, kuingiza na kutoa hewa chafu.
Kitaalamu, upo mchakato uitwao ‘Neurogenesis’
ambao husaidia kulinda seli za ubongo zinazokufa kutokana na uzee. Kuna
eneo kwenye ubongo linaloitwa ‘hippocampus’ ambalo ni eneo
linalotengeneza kumbukumbu.
“Kazi kubwa inafanyika kwenye ubongo, wakati wa
tendo la ndoa, kiasi kikubwa cha viamsha raha huanzia kwenye ubongo na
kuleta taarifa kwenye maeneo mengine ya mwili.
Ndiyo maana watu wengi hupotea kiufahamu wakati wa kilele” anasema Dk Gosh, ambaye ni mtafiti.
Hata hivyo, wanaume ambao wanaendelea na tendo la
ndoa mara kwa mara hadi wanapofikisha miaka 50 na zaidi, kwa maana ya
kutoa mbegu za kiume mara kumi kwa mwezi, wapo katika hatari ndogo ya
kupata saratani ya tezi dume. Inaelezwa kuwa mbegu za kiume hazitakiwi
kukaa mwilini kwa muda mrefu.Zinatakiwa zitolewe mara kwa mara ili
kuzifanya seli mpya zizalishwe. Ni kama kusafisha mpira, inasaidia
kusitisha ujenzi wa seli za zamani ambazo zaweza kuwa chanzo cha
saratani.
Kwa wanawake, tendo la ndoa husaidia kuundwa kwa
misuli ya nyonga ambapo misuli hiyo ikiwa imara huondoa hatari ya
kushindwa kuzuia mkojo,(urine incotinence) jambo linaloathiri mwanamke
mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka zaidi ya 50.
“ Wakati wa tendo la ndoa, kwa kawaida sakafu ya
nyonga za mwanamke hubana na kuachia. Hii husababisha misuli hiyo kuwa
imara’ anasema mtafiti huyo.
Kama ungependa kusoma habari hii kiundani basi tembelea http://www.mwananchi.co.tz/Tendo-la-ndoa--Tiba-mbadala-ya-maradhi-ya-moyo--ubongo-/-/1596774/2196600/-/3p5i0c/-/index.html
kama huwezi andika url hiyo basi bofya hapa
CREDIT:MWANANCHI.


0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment