Saturday, February 8, 2014

CCM waanza mchakato wa kura za maoni kumtafuta Mbunge wa Jimbo la Kalenga.

 Wagombe hao
 Msanii wa CCM Ally Bin Ahamed maarufu kwa jina la mpemba asilia akitoa mashairi ya kuipongeza CCM
 
Wagombea nao wakijifariji kwa makofi ya wajumbe

KAIMU Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga amewasihi wajumbe wa mkutano huo kumchangua mgombea anayoonekana kukubalika kwa asilimia 60 kwa wapiga kura.

"Falsafa ya chama kwanza, mtu baadaye lazima tuipime vizuri, tunahitaji ushindi na ili tupate ushindi lazima tuangalie wananchi wanataka nini," alisema.

Akifungua mkutano huo, Mtenga aliwataka wagombea ndani ya chama hicho wawe na utamaduni wa kukubali matokeo kwa afya ya chama.

Alisema wagombea wote tisa waliojitokeza katika kura hizo za maoni wana sifa za kuwa wabunge na akawataka wajumbe kutumia busara zaidi wakati wakifanya uamuzi.

Alisema mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho umecchukua siku mbili hali itakayosaidia kukinusuru chama na mipasuko.

“Tulikuwa na kawaida ya kufanya kura za maoni kwa zaidi ya mwezi mmoja; hali hiyo ilikuwa ikiwaacha wagombea  katika majeraha makubwa ya matumizi ya fedha,” alisema.

Alisema majeraha hayo yamekuwa yakichangia hasira kwa wagombea walioshindwa ambao badala ya kukisaidia chama kipate ushindi, hufurahia kinapopoteza nafasi.

Alisema kwa mtaji walionao, CCM wana hakika na ushindi wa kishindo katika jimbo hilo lililoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.


Waliojitokeza kupitia katika chama hicho ni pamoja na Jackson Kiswaga, Hafsa Mtasiwa, Godfrey Mgimwa.

Wengine ni Gabriel Kalinga, Peter Mtisi, Edward Mtakimo, Bryson Kisaba, Msafiri Pagamila na Thomas Mwakoka.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top