Mtokeo ya kura za maoni ndani ya
CCM yametangazwa, mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga
Godfrey Mgimwa akishinda kwa kishindo katika nafasi hiyo huku
Jackson Kiswaga akifuatia katika matokeo hayo.
Mtoto wa Mgimwa amepata kushinda kwa
kura 342 huku Kiswaga akipata kura 170 na mkuu wa wilya ya Pangani
Hafsa Mtasiwa akiambulia kura 42 .
matokeo hayo yametangazwa usiku wa jana
katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa mjini Iringa huku
mgombea Peter Mtisi akipata kura 33 ,Msafiri Pangagira kura 8,Bryson
Kibasa kura 7,Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment