Wednesday, June 4, 2014

Diamond Platnumz azidi kumburuza davido katika BET Awards.

fans’ wanaweza kufanya lolote kuhakikisha wanampa ushindi msanii wao katika shindano lolote linalohitaji ushiriki wao hasa kwa kupiga kura au maoni, kama kinachofanywa hivi sasa na mashabiki wa diamond platnumz katika tuzo za bet.

BET wanaendelea kuweka majina ya nominees katika page zao za mitandao ya kijamii ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuwaongezea ushawishi wa kupewa ushindi wasanii wao. Kama ilivyokuwa jana picha ya Diamond imeendelea kupata likes na comments nyingi katika Facebook ya BET, mpaka sasa ina likes 2649 na comments 5471 huku Davido akiwa na likes 1465 na comments 619 tu.

Diamond-Davido-Number-One-Remix-4
Upande wa Instagram ya BET Awards picha ya Diamond iliyowekwa jana usiku na maelezo haya:
‘Dbl tap this pic if you want #DiamondPlatnumz to win #BestInternationalAct: Africa @ the #BETAwards this yr’,

Hadi sasa ina likes 3275 na comments 4354 huku picha ya Davido katika akaunti hiyo ya IG ya BET iliyowekwa siku mbili zilizopita ina likes 518 na comments 2.

Cha kushangaza mashabiki wa Diamond wameamua kutoka nje ya kile kinachotarajiwa baada ya kuamua ku-comment jina la Diamond katika picha hiyo ya Davido.
habari kamili :: read more...

Mume wa Frora Mbasha amtuhumu mkewe kumfanyia mchezo mchafu wa kumbambikiza kesi ya kubaka.

Upande wa pili wa shilingi! Kwa mara ya kwanza tangu ahusishwe na skendo ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, mume wa mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameibuka na kuzungumza na Uwazi katika mahojiano maalum dhidi ya kashfa yake hiyo huku akitishia kujiua.

Akizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa moja mwishoni mwa wiki iliyopita huku akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya kuondoka nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni mwimba Injili kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha siri kwamba anajua anachezewa mchezo mchafu baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake na mkewe hadi kutishia uhai wa ndoa yao.

ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma zilizoripotiwa na binti aitwaye... (anamtaja jina) ambaye kweli ni ndugu wa mke wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-Shule (Dar) si za kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu, anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”

KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
“Kweli ndoa yangu na Flora ina matatizo lakini matatizo yetu ya ndani sana hakuwa na sababu ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia gerezani mimi ili yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili. Lakini navijua.”

MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini. Hebu fikiria hapo. Mwanzo alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi saa 4:00 asubuhi. Pia saa 10:00 jioni aliondoka tenda kwenda gym akawa anarudi kati ya saa 3:00 hadi 4:00 usiku.

“Nilipomuuliza alinijibu kuwa ni kwa sababu anatembea umbali mrefu. Hebu ona sababu ilivyo dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe mwandishi, unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke ningepata, iweje nibake?

“Jaribu kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili ambalo linaweza kunifanya nifungwe, nilitarajia mke wangu awe upande wangu, lakini cha ajabu yeye ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu, niamini nini mimi zaidi ya yeye kuhusika na kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake yeye?”

AFUATILIA
“Nilipofuatilia niligundua tayari kuna tatizo kwenye ndoa yetu. Mdudu alikuwa ameingia ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi naye. Anaishi hotelini.
“Anachokifanya mke wangu ni kitu kibaya mno. Alimtengeza yule binti ambaye nilikuwa namsomesha sekondari pale (anataja shule maarufu Dar), akampa semina ya kutosha kwamba aseme nimembaka ili nipate misukosuko na yeye awe huru.

“Kama hiyo haitoshi, akala dili na madaktari,  wakafoji majibu ya vipimo vikionesha kweli yule binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo vilioneshaje kama ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona napandishiwa kizimbani kwa jambo la kutengenezewa.
“Napiga picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi ambavyo vyombo vya habari vitakavyoandika na picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya kweli.

“Dah! Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia vitu vingi sana. Hakustahili kunitendea ubaya huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote mkubwa. Mimi ndiye nimempeleka kwa watu wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka, siamini. Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha hii,” alisema Mbasha kwa uchungu.

HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo mafichoni, sijaambiwa na mtu yeyote nikatoe maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa nahitajika nitakwenda kutoa maelezo yangu kwani sijawahi kutenda kosa hilo na Mungu awe shahidi yangu.”

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar, Marietha Minangi alithibisha kuwepo kwa ishu hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002 hivyo mwaka huu wametimiza miaka 12 wakiwa pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth. Msikilize mwenyewe hapa chini:
habari kamili :: read more...

Picha kali za NICK MINAJI zikionesha umbo lake alvyo mkali zicheki hapa.

Hajawahi kuwa mmoja wa wanaoficha maungo yao kwa nguo kubwa lakini alichovaa siku ya jana ilikuwa ni hataru tupu.Siku ya jumapili kwenye Summer Jam Hip Hop na R&B, Nicki Minaj alionekana akiwa amevaa ki top cha silver chenye kuonyesha maziwa yake kikiwa kimezibwa na alama ya nyota kwenye nipples zake.

Mambo yalizidi kuwaka moto zaidi pale Nicki Minaj alipomrukia Drake kwenye stage na kuzungusha miguu yake kwenye kiuno cha Drake na kumuwekea mikono mabegani na Drake nae kuzungusha mkono wake kwenye kiuno cha Nicki, kitu ambacho hakikumfurahisha Rihanna ambae alionekana kuweka sura ya mbuzi alipokuwa akitazama waliyokuwa wanayafanya stajini. Rihanna na Drake kwa sasa wameachana aada ya kurudiana mda si mrefu tanguwalipoaznza kudate mwaka 2009 baada yakupokea kipigo kutoka kwa Chris Brown.


habari kamili :: read more...

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA KATIKA MAZISHI YA BABA WA MBUNGE MARTHA MLATA JANA.

 Mbunge Martha Mlata akifarijiwa na waliohudhuria mazishi ya baba yake mzazi. Kushoto ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania ‘CHAMUITA,’ Stella Joel na mwakilishi wa wasanii wa filamu, Dokii.

Baadhi ya wabunge na ndugu wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya kaburi la baba mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida ambaye pia ni msanii wa nyimbo za injili, Martha Mlata.
habari kamili :: read more...

Jay Z na Beyonce wachefuana kufuatia mahusiano ysiyokua ya kawaida ya Beyonce na bodyguard wake.


According to recent reports, Jay Z is jealous of Beyonce’s close relationship with her bodyguard Julius(a divorcee with a kid) ,and thinks she’s having an affair with him

.He is the same bodyguard who tried to protect Jay Z in the elevator attack.He is so close to her that, his hands are on her most of the time.  It is understandable why Jay Z would feel uncomfortable.

The guys knows too much ,has been there through it all (since 2009),and is the only one who knows the truth about that elevator fight..He protected Beyonce to the extent that, after the elevator fight, Jay Z wanted to enter her car with Solange but he directed Jay Z to enter another car…
 








habari kamili :: read more...

Kifo cha Tyson chawapatanisha Wema na Kajala.

AMA kweli kufa kufaana! Lile bifu zito lililokuwa likitokota kati ya wapendwa wawili, Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na mwigizaji mwenzake wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja limekwisha kufuatia kukalishwa katika kikao cha siri  kilichofanyika kwenye msiba wa aliyekuwa mwogoza filamu mahiri nchini, marehemu George Otieno ‘Tyson’, Risasi Mchanganyiko limeinasa.

Wema Isaac Sepetu na mwigizaji mwenzake wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja wakiwa pamoja katika hali ya kupatana.

Kwa mujibu wa chanzo makini, upatanishi huo ulitokea baada ya wote wawili kufika kila mmoja kwa wakati wake kwenye msiba huo nyumbani kwa marehemu, Makonde, Mbezi-Baech jijini Dar.
Kabla ya kikao hicho, ‘maadui’ hao kila mmoja alionesha kuwa kivyake huku wapambe wakiwaongoza kwenye ‘kambi’ mbalimbali ili wasikutane.

Ilidaiwa kwamba kufuatia hali hiyo, ndipo baadhi ya mastaa waliamua kujikusanya na kujadili namna ya kuwapatanisha wawili hao huku wakiona kwenye msiba huo ndiyo mahali mwafaka kwa vile wote wapo.

MUDA WA KIKAO
Chanzo kilidai kwamba, kikao cha kuwapatanisha Wema na Kajala kilichukua muda wa saa mbili, kwa maana ya dakika 120 huku kikifanywa kuwa siri nzito ambayo haikutakiwa kufika kwenye vyombo vya habari.

Kajala Masanja

WAJUMBE WA UPATANISHI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wajumbe wasiopungua nane walishiriki kuwaweka chini maadui hao na kusikiliza hoja zao kabla ya kupatanishwa.

“Kikao kilikuwa kizito kidogo, kilianza usiku mwingi, lakini kiliisha salama.
“Kajala alionesha ugumu wa kukubali kupatana kuliko mwenzake (Wema) lakini wajumbe walikuwa ngangari.

“Wajumbe waliokuwepo ambao wote ni watu wa filamu ni Single Mtambalike ‘Richie’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Hartmann Mbilinyi, Vincent Kigosi ‘Ray’, John Lista na mwingine alliyetambulika kwa jina moja la Lamatha,” kilisema chanzo chetu kwa kujiamini.

BAADA YA USULUHISHI
Chanzo kilisema kuwa baada ya kumaliza upatanishi huo, wawili hao walibaki wenyewe ambapo waliongea mambo mbalimbali kuhusu maisha kwa sasa.
“Kusema ule ukweli hawa watu wamepatana kweli, wala si sinema. Hata baada ya usuluhishi, waliachwa wenyewe ambapo walizungumza mambo yao,” kilisema chanzo hicho.

Wema Isaac Sepetu katika pozi.

HISTORIA YA BIFU
Machi 25, 2013, Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka mitano kufuatia kesi yake ya kuuza nyumba iliyowekewa zuio halali na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).
Kesi hiyo ilihukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ambapo Wema alimlipia Kajala faini ya shilingi milioni 13 na kumfanya mshitakiwa huyo kuwa huru.

Baada ya hapo, wawili hao wakawa marafiki wakubwa huku Kajala akifanya kazi ya ukatibu kwenye ofisi ya Wema ya Endless Fame Production, Mwananyamala jijini Dar (kabla haijafungwa).

BIFU
Haikujulikana mara moja nini kilitokea, lakini ghafla wawili hao wakawa maadui. Madai ya chanzo yalisema bifu lao lilitokana na kitendo cha Kajala kumchukua ‘bwana’ wa mwenzake anayejulikana kwa jina la CK au kigogo wa ikulu.

Huyo kigogo wa ikulu, awali alikuwa mpenzi wa Wema na Kajala kuwa shemeji yake ‘automatiki’.
Chanzo kingine kilisema bifu lao lilitokana na kitendo cha Wema kuhamishia ushoga kwa staa mwingine wa filamu, Aunt Ezekiel hivyo kumfanya Kajala kuwa ‘wazamani’.

UKWELI WA BIFU
Hata hivyo, ukweli wa kuwepo kwa bifu lao ulijitokeza siku moja Kinondoni jijini Dar ambapo Wema alikuwa saluni, Kajala naye akafika, Wema alitoka ili kumkumbatia lakini Kajala akamkwepa na kumwambia atamchafua.

Inadaiwa Wema alikasirika na kumtukana Kajala hali iliyokoleza bifu lao ambalo awali lilikuwa chini kwa chini. Ilidaiwa siku hiyo Wema aliamua kutumia nafasi hiyo ya kukumbatiana ili kuondoa minong’ono ya siku nyingi kwamba wana bifu.

Hata hivyo, katika mahojiano maalum na mwandishi wetu, Wema alikiri kuhusu Kajala kumkwepa lakini akaongeza kuwa, bifu lao liliungwa mchuzi kufuatia kitendo cha Kajala kumsema vibaya kuhusu fedha zake.

Wema alisema kuna wakati walikwenda Arusha kwenye shoo iliyoandaliwa na kampuni yake, yeye akawa na uhutaji wa fedha ambapo alimuomba Kajala.
Alisema licha ya kumkopesha ikiwa imepungua kidogo, lakini Kajala alimwita mdogo wake mmoja na kumpa fedha nyingine akimwelekeza akaziweke benki kwa vile anahisi Wema atazimaliza.

SHUTUMA HADHARANI
Kuanzia hapo, Wema na Kajala walikuwa wakiropokeana kwenye vyombo vya habari. Kuna siku Wema alidiriki kutoa tamko kwamba, kwa hali ilivyo anajuta hata kumtolea zile shilingi milioni 13. Akasema angejua angemwacha akafungwe jela.

Habari hiyo iliandikwa na Gazeti la Ijumaa la Aprili 25, mwaka huu ikiwa na habari yenye kichwa; NAJUTA KUMLIPIA KAJALA MIL. 13!

WADAU WASHUKURU
Tukirudi kwenye chanzo, kilisema wadau waliosikia kupatana kwa wawili hao ndani ya msiba wa Tyson walishukuru wakiwaombea kwa Mungu awape uzima.

KUHUSU MWILI WA TYSON
Kwa upande mwingine, mwili wa George Tyson uliagwa jana kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar na kusafirishwa kwa ndege kwenda nchini Kenya kwa mazishi.
habari kamili :: read more...

Tuesday, June 3, 2014

Joseph Olita aliyeigiza kama Nduli Idi Amini Dada amefariki Dunia.


Wakati Tanzania tukiendelea kuwa na majozi ya vifo 3 mfululizo kutoka kwenye tasnia ya filamu Tanzania,wenzetu nao Uganda wamempoteza jamaa aliyeigiza kama Idi Amini,Idi Amini wengi wanamfahamu kutokana na matukio mengi aliyowahi kufanya ingawa kuna kizazi hakikuwahi kumuona.

Kupitia filamu ya  The Rise and Fall of Idi Amin,jamaa alicheza kama Idi Amini  na filamu hii ilikua ikielezea matukio yote aliyowahi kuyafanya Idi Amini enzi za uhai wake.

Joseph Olita ambaye ndiye aliyecheza kama Idi Amini amefariki jumapili ya June 01 akiwa na umri wa miaka 70 kusini mashariki mwa Alego huko kogelo Nchini Kenya na ilikua baada ya kumaliza mazishi ya mama yake mzazi.

TZA JOSEPH OLITA -IDI AMINMmoja wa ndugu wa Joseph,Bi.Risper Odero amesema kifo cha Joseph Olita kimetokana na shinikizo la damu iliyosababishwa na shughuli nyingi na majonzi wakati wa kumuaga marehemu mama yake mzazi.

Bi Odero amesema kifo cha Olita ni pigo kwa familia hiyo hasa baada ya kumuaga mama yao mzazi masaa kadha kabla ya kifo cha olita,Olita alikua anafanana sana na aliyekua kiongozi wa kiimla Uganda bwana Idi Amin Dada.

Miongoni mwa vitu walivyokuwa wanafanana ni pamoja urefu wa futi sita nchi 5.5 na uzito wa kilogramu 150 na ndiyo maumbile pekee yaliyo wafanya wengi kudhani kuwa olita alikua ndiye Idi Amin.

Mbali na filamu ya The Rise and Fall of Idi Amin ya miaka ya 80 iliyobeba maisha ya Idi Amin kama kiongozi wa kimila aliyeingia madarakani mwaka wa 1971 na kutolewa mwaka 1979 pia ameigiza kwenye filamu ya Mississippi Masala mwaka 1991 na amewahi kuigiza kama polisi kwenye filamu ya Sheena ya mwaka 1984.
habari kamili :: read more...

Saturday, May 31, 2014

ROSE NDAUKA AJIBU TUHUMA ZA KUPORA WAUME ZA WATU!



Wiki iliyopita katika Exclusive Interview tuliona sehemu ya kwanza ya Rose Ndauka alivyoeleza kuwa aliwamwaga wanaume na kutulia na Maliki. Wawili hao kwa sasa wanaogelea katika penzi zito na mikakati thabiti ya ndoa imeshaanza, wanatarajia kuoana baadaye mwaka huu.

Msanii wa Bongo Muvi, Rose Ndauka.

Leo tunaendelea, atafungukia skendo za kupora waume za watu.
Risasi: Kuna taarifa zilienea kuwa uliwahi kutoka na baba mtoto wa Snura Mushi (mama Majanga), kuna ukweli wowote?

Rose: Nilishawahi kusikia skendo hiyo lakini aliyekuwa anadhania hivyo ni Snura, hakujua tu kama yule alikuwa ni mshkaji wangu na mimi nilimjua Snura walipokuwa kwenye uhusiano.
Risasi: Mbali na huyo, mbona inatajwa kuwa uliwahi kumnyang’anya mwigizaji mwenzio, Yvone Cherry ‘Monalisa’ mpenzi wake? Tena inasemekana mlikuwa marafiki!

Rose Ndauka akiwa na mume wake Maliki.

Rose: Sijawahi kuwa na urafiki na Mona (Monalisa) na huyo aliyezua hayo maneno ni Richard, siyo kweli kwani tuliwasiliana kawaida yeye akapindisha maelezo, shahidi ni baba mtoto wangu aliyeunganishwa na baba mtoto wangu pamoja na marehemu Kanumba (Steven).

Risasi: Umekuwa ukihusishwa na uvutaji wa bangi mara kwa mara, unalizungumziaje hilo?
Rose: Sijawahi kuvuta bangi ila nimewahi kunywa pombe sana hasa nilipokuwa na ‘stress’ na yote niliyokuwa nayafanya mwisho wa siku nilikuwa nikiyajutia.

Risasi: Ni kitu gani kilikufanya ujutie hasa katika suala zima la kugida ulabu?
Rose: Kuna habari imewahi kutoka gazetini nikiwa nabusiana na Maya, iliniumiza sana kwani tulitafsiriwa vibaya kwenye jamii na haitakuja kufutika kwani nilifanya matendo yale kwa sababu ya pombe na toka siku hiyo kiukweli niliacha unywaji wa pombe za vile, nilijuta.

Risasi: Ukipata nafasi ya kuongea na wasichana wasagaji utawaambia nini?
Rose Ndauka: Nitawashauri kuacha kabisa mambo hayo kwani ni ya kuiga tu, wajisomee vitabu vya kila aina ili kujinusuru kwenye tatizo hilo hasa vyenye mafunzo na kuonesha madhara ya usagaji.
Risasi: Tunafahamu kwamba mumeo mtarajiwa umemkuta na mtoto, unamleaje na hujawahi kupata malalamiko kama mama wa kambo?

Rose: Mimi ni kipenzi cha watoto, nampenda na yeye ananipenda, ninapomuona ana kosa namuadhibu kama mwanangu na sitarajii mtu kunisema vibaya kwani malezi ninayompa ni mazuri kama ambavyo namlea wa kwangu.
habari kamili :: read more...

JOHARI AMTUPIA CHUCHU VIJEMBE MSIBANI.


STAA wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kumtupia vijembe kiaina msanii mwenzake, Chuchu Hans ambaye ‘anabanjuka kimalovee’ na mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya RJ, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’.

Staa wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’.

Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye msiba wa mwigizaji Sheila Haule ‘Recho’ Sinza-Palestina, Dar, hivi karibuni ambapo vijembe viliibuka baada Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kumuuliza kwa lugha ya utani Chuchu kuwa RJ itachangia nini msibani hapo, Johari akadakia:

“Kampuni yangu si ya uchochoroni au ya chumbani, nina TIN namba kabisa siyo kama hiyo nyingine, iweje umuulize asiyehusika...”

Baada ya Johari kutamka maneno hayo, waombolezaji waliokuwepo msibani hapo walipigwa na butwaa na kuhoji kulikoni?

Johari amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano na Ray kipindi cha nyuma huku kukiwa na taarifa kuwa Chuchu ana kampuni iitwayo Chura ikimaanisha Chuchu na Ray hivyo ilitafsiriwa kuwa alikuwa akiipiga kijembe kwa madai kuwa haiwezi kufikia levo za RJ.

Alipofuatwa na mwanahabari wetu ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo, Johari hakuwa tayari kwani alisema ana majonzi ya kuondokewa na kipenzi chake Recho hivyo hakutaka malumbano na watu katika kipindi hiki kigumu.
habari kamili :: read more...

Kijana anayedaiwa kuwa Msukule aonekana nje ya nyumba ya Kikongwe aliyeuawa kwa imani hizo.

Kijana Ndaki Samola akiwa amepandishwa ndani ya gari la polisi kwa ajili ya kupelekwa kwa wataalamu ili kufanyiwa uchunguzi kama ana matatizo ya akili.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mamia ya wananchi wa kijiji cha Ilebelebe kata ya Itilima wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamefurika kushuhudia tukio la kijana mmoja anayesadikiwa kuwa ni msukule aliyeibuka siku moja baada ya kikongwe kuuawa kwa kucharangwa mapanga kwa imani za kishrikina kijijini hapo.

Kijana huyo aliyedai kuwa anaitwa Ndaki Samola alionekana jirani na nyumba ya mwanamke Nyanzala Basu (65-70) aliyeuawa Mei 26 mwaka huu,saa moja na nusu usiku baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana kisha kumcharanga mapanga akiwa nyumbani kwake kisha kutokomea kusikojulikana.
Imeelezwa kuwa siku ya mazishi ya Kikongwe huyo Mei 27 mwaka huu ndipo kijana huyo anayedaiwa kuhifadhiwa na kikongwe huyo alikutwa na wananchi nyuma ya nyumba ya kikongwe huyo saa tatu usiku akizunguka na kusikika akisema kaamua kutoka nje baada ya kukosa chakula.
Walioshuhudia tukio hilo walisema Kijana Ndaki Samola anayedaiwa kuwa ni msukule akizungumza kwa shida alisema anatoka kijiji cha Bubale kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga na alifika kijijini hapo kwa ajili ya kuoa.
Kijana huyo akizungumza bila ya kufafanua ni kipindi gani amekaa katika kijiji hicho alidai alikuwa akiishi kwenye nyumba ya bati ya kikongwe huyo na wenzake wawili na kwamba kutokana na njaa yake ndiyo kaamua kutoka.

Mwenyekitiwa kijiji cha Ilebelebe Thomas Nkindo alisema tukio hilo limewashangaza kwani kijana huyo hajawahi kuonekana kijijini hapo hata siku moja ,hali ambayo imewapa wasiwasi wananchi kutokana na maneno aliyoeleza kwamba alikuwa kwenye nyumba ya kikongwe huyo ambayo ilikuwa imefungwa kwa muda mrefu na haitumiki.

“Baada ya kuhojiwa na jeshi la jadi sungusungu kijana, alidai kilichomtoa ndani ni njaa na kawaacha wenzake wawili mmoja akiwa ni mwanamke,na alikuja kwa ajili ya kuoa na kufikishiwa kwenye nyumba hiyo ya tope ambayo imeezekwa kwa bati iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu”,alieeleza Nkindo.
Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji cha Ilebelebe Emmanuel Asili alisema marehemu Nyanzala Basu kabla ya kufikwa na mauti siku hiyo ya tukio asubuhi alikuwa amealika wanawake, ambao walifanya kazi ya kumsaidia kukata viazi maarufu kama michembe ndipo usiku huo huo alivamiwa na kuuawa majira ya saa 1.30 wakati akimpatia mbwa wake chakula.

“Kilichotushtua zaidi huyo kijana Ndaki alikuwa ananukia harufu ya nyama wakati tunamuona na ukizingatia mchana kwenye mji huo ulipokuwa msiba walikuwa wamechinja mbuzi,moja kwa moja wananchi walimtilia mashaka inawezekana akawa ni msukule kwa kulinganisha na maelezo yake “alisema Asili.

“Kutokana na mashaka hayo tulitoa taarifa kwa jeshi la polisi huku tukimhifadhi kijana kwa muda katika ofisi yangu uangalizi zaidi na polisi walipofika walizungumza na wananchi na kuamuru mlango wa nyumba hiyo uvunjwe ili kuona kilichomo ndani wakakuta beseni,ndoo na bati lililochakaa”,alieeleza afisa mtendaji wa kijiji.

Akizungumza na wananchi mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Kishapu ASP Samwel Kijenga aliwataka kutoa ushirikiano ili kuwabaini watu waliosababisha mauaji hayo ya kinyama huku akiwataka kuondoa wasiwasi kuhusu nyumba waliyokuwa wakihofia kwani wameangalia hawajaona kitu hivyo waendelee na shughuli za maendeleo.

Hata hivyo wakati kijana huyo akiwa tayari amepandishwa ndani ya gari la polisi kwa ajili ya kupelekwa kufanyiwa uchunguzi kama ana matatizo ya akili,alitokea mwanamme aliyejitambulisha kwa jina la Nyalali Chaba mkazi wa kijiji cha Ikoma wilayani Kishapu na kudai kuwa anamfahamu ni mdogo wake anasumbuliwa na tatizo la akili ndipo polisi wakamkabidhi kwa maandishi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga SACP Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji ya kikongwe na tayari watu wanne wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi wakati wakiendelea na upelelezi
habari kamili :: read more...

Breaking!! GEORGE TYSON WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA.

 George Tyson enzi za uhai wake.

George Tyson akimlisha keki Yvonney Chery ‘Monalisa’ wakati mtoto wao Sonia alipopata kipaimara.

Marehemu Tyson akiwa na Monalisa (kushoto), kulia ni Tyson na mwanae Sonia.

NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari eneo la Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa amemlilia Tyson kwa kuandika yafuatayo:


MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MPENDWA WETU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
habari kamili :: read more...

Friday, May 30, 2014

Habari ya kusikitisha; Mwanafunzi wa Chuo kikuu UDSM akutwa Hosteli kitandani amekufa.



TUTAKUPA TAARIFA KAMILI NA ZAIDI HIVI PUNDE.
habari kamili :: read more...

Arsene Wenger ametia saini mkataba wa kuendelea kuinoa Arsenal hadi mwaka 2017.

Arsene Wenger ametia saini mkataba wa miaka miwili kama meneja wa klabu hiyo hadi mwaka 2017.

Wenger, 64, ameongoza Arsenal na kufanikisha ushindi wa mataji 8 tangu kujiunga na klabu hiyo Septemba mwaka 1996.Msimu huu aliweza kuongoza timu hiyo hadi kufuzu kwa mara ya 17 kwa kombe la klabu bingwa ulaya na kupata ushindi aliosubiri kwa hamu kwa miaka tisa dhidi ya Hull City katika fainali ya kombe la FA Cup.

Wenger alikuwa anafika ukingoni mwa mkataba wake mwaka huu

Arsenal ilikuwa haijawahi kushinda taji la nyumbani tangu mwaka 2005 ingawa walifika fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya mwaka 2006.Wenger, ambaye sasa ni meneja mkongwe zaidi katika ligi ya Ulaya baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu, mwezi Mei mwaka 2013, anasifika kwa kuleta mawazo mapya kuhusu michezo na lishe bora katika soka Uingereza.

''Huyu ndiye mtu anayefanya kazi mwa saa 24 kila siku,'' alisema mlinda lango wa zamani wa Arsenal Bob Wilson.

"anachukia sana kushindwa. Alileta mageuzi makubwa, katika kila sekta ya mchezo huo nchini Uingereza. Watu wanadhani kuwa ana mamlaka sana lakini mtu ambaye anajitolea sana kwa mchezo huu ni mtu anayethaminiwa sana.''

Ushindi mkubwa wa Wenger ulikuwa wakati ambapo alishinda kombe la ligi ya Premier kati ya mwaka 2003-04 alipokuwa na wachezaji kama vile Thierry Henry na Patrick Vieira.

Wenger alimsajili Mesut Ozil kwa kima cha dola milioni 42.4 kwa msimu ambao umekamilika.

Lakini licha ya hali ya suitofahamu kuhusu mustakabali wa Wenger mwezi Januari, mkurugenzi mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alitabiri kuwa Wenger huenda akaongezewa muda Arsenal.
habari kamili :: read more...

AGNES MASOGANGE AVISHWA PETE YA UCHUMBA YA MIL.16 BAADA YA KUDUNGWA MIMBA AFRIKA KUSINI.


Habari mpya ni kuwa Agnes Masogange ambaye ni video queen maarufu nchini amevishwa pete ya uchumba yenye thamani ya shilingi mil.16 za kitanzania. 

Habari zaidi zinadai kuwa Masogange kwasasa ni mjamzito na alipoenda Afrka  Kusini hivi juzi kati kumuambia jamaa aliyempa mimba kuwa ana ujauzito wake Jamaa huyo alifurahi sana na kumvisha Masongange pete inayoonekana pichani ambayo Agnes mwenyewe aliweka picha hiyo katika mtandao mmoja wa kijamii na kuandika maneno yasemayo "mama kijacho".
habari kamili :: read more...

Mchawi mtanzania jela miaka 3 nchinin Kenya.

Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.

Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18. Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.

Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe maradufu

Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa

Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu Nairobi.

Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba.
habari kamili :: read more...

Italy yathibitisha kuwa umri wa Minala ni miaka 17 sio 42.

 
Uchunguzi wa shirikisho la soka la Italia umebaini kuwa mchezaji tineja wa Cameroun Joseph Minala ana umri wa miaka 17 wala sio 42 kama ilivyodhaniwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari.
Mnamo mwezi Februari mtandao mmoja wa michezo barani Afrika ulichapisha habari ambayo ilizua dukuduku iwapo kiungo huyo alikuwa amedanganya umri wake .
Mtandao huo ulichapisha habari za kuashiria kuwa hakuwa tineja bali mtu mwenye umri wa miaka 42.
Uchunguzi uliofwatia ulimlazimu kukatiza kwa muda mipango yake ya kucheza soka ya kulipwa hadi pale matokeo ya uchunguzi yangewekwa wazi na maafisa wa shirikisho la soka la Italia.
Minala alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Rome na hata alishiriki mchuano wa vijana wasiozidi umri wa miaka 23 wa Viareggio mnamo mwezi wa Februari.
habari kamili :: read more...

Mume amshtaki mkewe kwa kumnyima ngono.

Majaji waliamua kuwa mkewe Mason hakufanya kosa lolote
Kuna kisa kimeibuka nchini Uingereza ambapo mwanamume mmoja kwa jina David Mason, mwenye umri wa miaka 30, alimshitaki mkewe Brenda kwa kumnyima haki yake ya kingono au kukataa kushiriki tendo la ndoa.

Mwanamke huyo alimfanyia mgao wa wiki moja kila mwezi wa kitendo cha ndoa mumewe kwa hofu ya kushika mimba kwa mara ya tatu.

Kwa mujibu wa jarida la mtandao la Mirror, la Uingereza, Bwana Mason, ambaye kazi yake ni fundi mitambo alishinda kesi hiyo mwaka 1980.

Lakini mkewe alikataa rufaa ambapo Mason alipoteza kesi hiyo baada ya majaji kusema kuwa mahakama isingeweza kuamua kuwa mkewe Mason alimkosea.

Nini maoni yako kuhusu tukio hili?

Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili
habari kamili :: read more...

Majibu ya Zitto Kabwe juu ya madai ya kambi ya upinzani kuhusu Lekadutigite na Gombe Advisors haya hapa.

Kwenye Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo aliyoiwasilisha Bungeni leo hii muda mfupi uliopita. Waziri Kivuli Joseph Mbilinyi  ‘Sugu’ alimtaja Zitto Z. Kabwe kama Mmiliki wa Kampuni ya Leka Dutigite aliyofanya biashara isivyo halali na Mashirika ya Umma ya NSSF na TANAPA.

Hivi ndivyo ilivyokuwa sehemu ya hotuba hiyo.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 13 Agosti, 2012, Msajili Msaidizi wa Makampuni katika Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni (BRELA) alitoa Hati ya Usajili (Certificate iof Incorporation) kwa kampuni inayoitwa Leka Dutigite Limited. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, Leka Dutigite Ltd. ina ofisi zake katika ghorofa ya kwanza ya jengo la City House lililoko katika Mtaa wa Mkwepu, Dar es SalaaM.

Mheshimiwa Spika,Katiba yaani Memorandum and Articles of Association, ya kampuni ya Leka Dutigite Ltd. iliyosajiliwa BRELA tarehe 13 Agosti, 2012 inaonyesha kwamba mwenye hisa nyingi katika kampuni hiyo ni kampuni nyingine inayoitwa Gombe Advisors Ltd. ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za kibenki ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imezipata, mnamo tarehe 10 Desemba, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha jumla ya shilingi 12,200,000 kwenda kwenye akaunti na. 0150357447800 iliyoko CRDB Bank tawi la Pugu Road, Dar es Salaam, inayomilikiwa na Leka Dutigite Ltd. Hifadhi ya Taifa ya Saadani inamilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), ambayo ni shirika la umma. Siku moja baadae, fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo.

Baada ya hapo, kati ya tarehe 14 Januari na 7 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa jumla ya shilingi 28,600,000. Fedha hizi zote ziliingizwa kama fedha taslimu na mtu aitwaye Mchange (shilingi 3,600,000 tarehe 14 Januari, 2013) na Leka Dutigite (shilingi 25,000,000 tarehe 23 Januari na 7 Februari, 2013). Kufikia tarehe 7 Februari, 2013, fedha hizo zote zilikwishatolewa benki.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 28 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa shilingi 32,367,000 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kwa mujibu wa taarifa za kibenki, siku hiyo hiyo, fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadae, yaani tarehe 4 Machi, 2013, NSSF ilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite Ltd., kwa mikupuo miwili, ya jumla ya shilingi 46,663,000. Siku hiyo hiyo, fedha hizo nazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Kwa hiyo, katika kipindi cha miezi mitatu katika ya tarehe 10 Desemba, 2012 na 4 Machi, 2013, Leka Dutigite Ltd. ililipwa shilingi 119,930,000 kwa utaratibu huo huo wa ingiza na toa fasta. Kati ya fedha hizo, shilingi 12,200,000 zililipwa na TANAPA na shilingi 79,027,000 zililipwa na NSSF.

Mheshimiwa Spika, Katika mazingira ya kawaida, sio kitu cha ajabu kwa mashirika ya umma kama NSSF na TANAPA kufanya biashara na watu au taasisi mbali mbali kama makampuni binafsi. Ukweli ni kwamba, kwa upande wa malipo yaliyofanywa na TANAPA, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imeweza kupata nakala ya mkataba unaohusu Maandalizi ya Filamu (Documentary) kwa Ajili ya Kuhamasisha Shughuli za Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa Kutumia Wasanii Kutoka Kigoma. Mkataba huo umesainiwa tarehe 5 Desemba, 2012, kati ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Leka Dutigite Ltd. na una thamani ya shilingi 12,200,000, kiasi kile kile kilicholipwa na Hifadhi hiyo.

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mazingira ya malipo haya sio ya kawaida. Hii ni kwa sababu ya uwepo wa kampuni ya Gombe Advisors Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, kampuni hii ilisajiliwa tarehe 24 Novemba, 2011. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ofisi za Gombe Advisors Ltd. ziko kwenye jengo la City House, Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam, ziliko ofisi za Leka Dutigite Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, wakurugenzi wa Gombe Advisors Ltd. ni Zitto Zuberi Kabwe ambaye kazi yake inatajwa kuwa ‘mchumi’, na Raphael Ongangi ambaye anatajwa kuwa ‘mchambuzi wa fedha na vitega uchumi’ (Financial and Investment Analyst). Bwana Ongangi aliwahi kutajwa na gazeti la kila wiki la —– la tarehe 26 Desemba 2013 kuwa ni mmoja wa washauri wa Zitto Zuberi Kabwe na anasemekana kuwa msaidizi wake.

Mheshimiwa Spika, Zitto Zuberi Kabwe sio ‘mchumi’ anayetajwa katika nyaraka za BRELA zinazoihusu kampuni ya Gombe Advisors Ltd. pekee, bali pia ni Mbunge, tangu mwaka 2005, wa Bunge lako tukufu. Kama Mbunge, Mheshimiwa Zitto Kabwe ni ‘kiongozi wa umma’ kwa mujibu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, 1995. Sheria hii inawalazimu viongozi wa umma, wanapokuwa madarakani, kuwa “waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali.”

Aidha, viongozi wa umma “… watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi kwa umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu.” Vile vile, kuhusiana na maslahi binafsi, Sheria hii inaelekeza kwamba “… viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya.

Mwisho,kuhusiana na maslahi ya umma, viongozi wa umma wanatakiwa, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, kupanga masuala yao “kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma.” Kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu, Mheshimiwa Zitto Kabwe hajawahi kutangaza maslahi aliyonayo kwenye mikataba ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd. na NSSF na TANAPA.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe sio tu ni Mbunge anayebanwa na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bali pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC). Kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu, mojawapo ya majukumu ya PAC ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Wizara na Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. NSSF na TANAPA ni baadhi tu ya Mashirika ya Umma yaliyo chini ya usimamizi wa kibunge wa PAC.

Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Kabwe, kwa kutumia makampuni yake ya Leka Dutigite Ltd. na Gombe Advisors Ltd., amefanya biashara na TANAPA, shirika la umma analolisimamia kama Mbunge na Mwenyekiti wa PAC. Mheshimiwa Zitto Kabwe na wanamuziki washirika wake, kwa kutumia makampuni ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd., wamelipwa fedha za umma za TANAPA na NSSF.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo juu ya madai ya ukiukwaji wa Sheria uliofanywa na viongozi wa umma na mashirika ya umma katika kashfa hii. Pamoja na maelezo yatayotolewa , Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum juu ya matumizi ya fedha zilizotolewa na TANAPA na NSSF; msukumo uliofanya fedha hizo zitolewe na matumizi ya fedha hizo kwa kuzingatia masharti yanayosimamia fedha za umma na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma. Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ifanye uchunguzi juu ya malipo na matumizi husika kwa kurejea masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Sheria nyingine zinazohusika. Kwa upande mwingine, kwa kuwa suala hili linahusu mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na usimamizi wa fedha za umma, Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge nayo ifanye uchunguzi wake juu ya madai ya masharti ya Katiba ya Nchi, Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kanuni za Bunge juu ya maadili ya kiongozi wa umma ikiwemo yahusuyo utangazaji wa maslahi.

Mheshimiwa Spika; Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inatoa rai kwa wanamuziki na wasanii wengine wote nchini kuwa waangalifu na watu wanaotaka kutumia umaarufu wao kama wanamuziki na wasanii kwa lengo la kufanikisha dili za kifisadi. Bila kuchukua tahadhari ya kutosha, wasanii hao wanaweza kujikuta wakipoteza sifa na umaarufu wao ambao wameujenga kwa jitihada zao wenyewe.

Zitto Kabwe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amepost ujumbe huu usiku wa Mei 29 ambao unaonyesha kuwa na majibu juu ya maswali yaliyoulizwa na kambi ya upinzani juu ya umiliki wa Lekadutigite na Gombe Advisors,Hii ndiyo status yake.

Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.

Leo tarehe 29 Mei, 2014 Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni amenituhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika Shirika la TANAPA na NSSF.

Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa nitatoa maelezo kwa ufupi ili kuondoa upotoshaji.

Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii 15 ambapo kila mmoja ana hisa 5% ambazo niliwalipia ili waweze kushirikiana katika kazi zao. Hisa 25% zilizobakia zinamilikiwa na kampuni ya Gombe Advisors ambayo ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara (not for profit company). Hivyo Mimi binafsi sina maslahi yeyote ya kifedha zaidi ya kuwasaidia wasanii hawa katika kazi zao mbalimbali.

Wasanii wa Kigoma AllStars wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo. Kwa upande wa TANAPA wasanii hawa waliandaa kazi ya kuitangaza Hifadhi ya Saadani na walilipwa. Kwa upande wa NSSF wasanii hao walitunga wimbo na video yake na wimbo huo unatumika katika Shirika hilo.
Vile vile walifanya matamasha mbalimbali ya kuhamasisha watu kujiunga na NSSF. Wasanii wa Kigoma All Stars wote ni wanachama wa Mfuko huo.

Katika kazi zote hizi Mimi binafsi sijafaidika kwa namna yeyote ile kifedha. Kauli yeyote ya kujaribu kuonyesha kazi hizi za wasanii ni ufisadi ni kauli za kusikitisha na kukatisha tamaa kwa mtu ambaye anajaribu kusaidia wasanii kufaidika na kazi zao za sanaa.

Katika kazi zote hizi Mimi binafsi sijafaidika kwa namna yeyote ile kifedha. Kauli yeyote ya kujaribu kuonyesha kazi hizi za wasanii ni ufisadi ni kauli za kusikitisha na kukatisha tamaa kwa mtu ambaye anajaribu kusaidia wasanii kufaidika na kazi zao za sanaa.

Toka mwaka 2012 nilipoanza kujitokeza kusemea wasanii watu kadhaa wenye maslahi na tasnia hii wamekuwa wakinikatisha tamaa na hata wengine kuona nimewaingilia kazi zao.
Hivi sasa wasanii wa Kigoma AllStars ni wanahisa katika kampuni ya PERA Africa limited ili kufaidika na biashara ya miito ya simu. Yote haya nilifanya kwa uchungu nilionao kwa vijana wetu na sio kwa kutaka kufaidika kifedha. Nimeumizwa sana na tuhuma hizi za kuokoteza okoteza.

Inaniumiza zaidi kutokana na ukweli kwamba ninamwuguza mama yangu mzazi, kipindi ninachohitaji kutiwa moyo na kuombewa hata na maadui zangu kisiasa. Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama ambacho watoa tuhuma wanatoka, pole ninayopewa ndio hiyo. Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.

Najua wajibu wangu ni kusimamia Mashirika ya Umma na nikiwa mpigania uwajibikaji nipo makini sana kuhakikisha sina mgongano wa maslahi katika mambo yangu. Ndio maana sina biashara yeyote ile ili kuhakikisha natimiza wajibu wangu kwa uadilifu mkubwa. Napata ‘moral authority’ ya kutaka uwajibikaji kwa sababu nafanya kazi zangu kwa misingi hiyo ‘at arms length’.

Hivyo ninataka mara moja CAG afanye ukaguzi wa kazi za wasanii hao kwenye NSSF na TANAPA. Pia achunguze kama Gombe Advisors ( company limited by guarantee) ina maslahi yeyote ya kifedha katika kazi hizo za wasanii. Nataka pia Shirika la NSSF na TANAPA waweke wazi mchakato wa kazi zao na wasanii hawa kupitia LEKADUTIGITE Limited.

Zitto Kabwe
Mei 29, 2014
Dar Es Salaam.
habari kamili :: read more...

Wasichana watatu wabakwa na kuning'inizwa kwenye mt huko India.

Takribani wanaume watatu akiwemo afisa mmoja wa polisi tayari wamekamatwa kuhusiana na tukio la kubakwa kwa wasichana wawili wadogo na kundi la watu na kuning’inizwa juu ya mti huko nchini India.

Mamlaka katika Jimbo la Utter Pradesh limesema kuwa bado linamsaka mtu mmoja ambaye anatuhumiwa kuwepo katika kundi hilo lililohusika kufanya tukio hilo la kusikitisha.

Familia za wahanga wa tukio hilo zimesema kuwa mara ya kwanza polisi walikataa kuwasaidia katika kuwatafuta watoto hao baada ya kupotea ambapo matukio ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake nchini India bado yameendelea kuwa tatizo kubwa.

Wanakijiji walikuta miili ya wasichaa hao wenye umri wa miaka 14 na 15 ikiwa inaning’inia juu ya mti wa maembe saa chache baada ya kupotea nyumbani katika kijiji cha Katra kilichopo kwenye jimbo la Utter Pradesh.
Wasichana hao walikuwa wamekwenda vichakani kuoga kutokana na kutokuwa na vyoo nyumbani kwao ambapo mamia ya wanakijiji wenye hasira walikusanyika katika eneo hilo la mti kwa siku nzima wakiandamana kushinikiza polisi kukabiliana na vitendo hivyo.
habari kamili :: read more...

Vazi la lulu akitembea huku akiwa ameachia mtindi out hizi hapa.

 MSANII wa filamu Bongo, Elizaberth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni aliwashangaza watu baada ya kuvukwa na gauni alilokuwa amevaa na kulazimika kutembea huku sehemu kubwa ya kifua chake ikiwa wazi.

Msanii wa filamu Bongo, Elizaberth Michael ‘Lulu’.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika kiwanja kimoja kichopo mjini Arusha ambapo mmoja wa watu aliyemtia machoni Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:

“Yaani nilimuona Arusha akiwa amevaa gauni lililoacha wazi matiti yake, kaficha chuchu tu na inavyoonekana gauni lilimvuka, akaonekana akihangaika kulirudishia bila mafanikio.”

Ijumaa lilimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi bila mafanikio ila juzikati akatundika picha kwenye mtandao wa instagram akiwa amevaa gauni kama lile aliloonekana nalo Arusha.
habari kamili :: read more...

Thursday, May 29, 2014

HUYU NDIE MREMBO ALIYENASWA AMETINGA NGUO ZA MAREHEMU KUAMBIANA.

Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa.Mary Njombe aliyenaswa akiwa amevaa nguo za marehemu Adam Phillip Kuambiana.
 Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki.“Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary.

Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani).Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye.“Mwaka 2008 ndiyo tulianza rasmi uhusiano kwani mimi nilikuwa sina mwanaume na yeye hakuwa na mtu hivyo tulikubaliana na alikuwa akijulikana nyumbani kwetu,” alifunguka Mary.

Mwanadada huyo alisema kuwa yeye na Kuambiana walikuwa wakikutana kwenye Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar na mara nyingi alikuwa akimpikia chakula na kumpelekea ‘lokesheni’.

“Nimeumia sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema Mary huku akiangua kilio.


Alipoulizwa kama kweli nguo hizo ni za marehemu Kuambiana, alizama ndani akatoka akiwa amevaa pensi na shati la ‘drafti’ alilokuwa anapendelea kulivaa staa huyo ambalo ni maarufu sana.
Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na kusumbuliwa vidinda vya tumbo.

Adam Phillip Kuambiana enzi za uhai wake akiwa amevaa shati alilonaswa nalo mrembo.
habari kamili :: read more...

AIBU YA MWAKA, ANGALIA ALICHOKIFANYA BWANA HARUSI HUYU BAADA YA KUINGIA UKUMBINI.

Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firahuni ndo kama hiiiii.
habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top