Wednesday, November 19, 2014

HALI ILIVYO HONG KONG LEO.

 Polisi wakikabiliana na waamdamanaji waliotaka kuingia bungeni jijini Hong Kong leo.

Baadhi ya silaha walizotumia waandamanaji kujaribu kuingia bungeni.

VURUGU zimezuka kati ya polisi na kundi dogo la waandamanaji waliokuwa wakitaka kuingia bungeni asubuhi hii jijini Hong Kong nchini China.

Baadhi ya waandamanji hao wakiwa wamevaa mask walitumia vyuma kujaribu kuvunja mlango mmoja wa pembeni wa bunge kabla ya kudhibitiwa na polisi walioamua kutumia maji ya kuwasha kuwatawanya.

Takribani wiki nane sasa waandamanaji wamekuwa wakiandamana kudai demokrasia katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo la Hong Kong.

Tazama Video ya gari Mupya kabisa la aina yake lililotengenezwa Afrika Mashariki.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online