Ya leo inaweza kuwa moja kati ya
zilizowahi kukushangaza zaidi, inahusu mwanamke Janina Kolkiewicz raia
wa Poland, mwenye umri wa miaka 91 ambaye amekaa kwa muda saa 11 katika
chumba cha kuhifadhia maiti huku mwili wake ukiwa ndani ya jokofu baada
ya kuthibitishwa na daktari wa familia yake kwamba amefariki, muda mfupi
baadaye wahudumu wa mochwari waligundua kwamba ni mzima baada ya kuhisi
anatikisika ndani ya mfuko alimowekwa.
Baada ya kurudi nyumbani kwake akitokea mochwari, alilalamika kuhisi baridi kali na kupatiwa bakuli la supu ya moto na mkate.
Daktari aliyethibitisha mauti ya mtu
huyo anasema hata yeye anashangazwa na tukio hilo kwani vipimo vyote
vilionyesha kuwa mapigo ya moyo yalisimama na hakuwa hai.
Taarifa za kuwa hai mwanamke huyo
zilimshtua kila mtu kwenye familia yake na kujikuta ikibatilisha hati ya
kifo iliyotolewa kwa ajili ya mazishi yake ambayo yalipangwa kufanyika
siku mbili baadaye..
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment