Saturday, September 6, 2014

Maximo atoa siku nane Yanga.


Kocha  Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo,akisisitiza jambo.

Na Wilbert Molandi
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, ametamba kuwa, siku nane zilizobaki kabla ya kukabiliana na Azam FC, zinamtosha kabisa kuifunga timu hiyo.

Timu hizo zinatarajiwa kujitupa uwanjani Septemba 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Hadi kufikia leo Jumamosi zitakuwa zimebaki siku nane kufikia mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, ambayo kila timu inahitaji ushindi ili iweke heshima.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Maximo alisema kuwa kikosi chake kinahitaji maboresho kidogo ambayo kuanzia leo (Jumamosi) kwenye mazoezi yake hadi kufikia siku hiyo ya mechi kikosi kitakuwa kimeshaimarika.

Maximo alisema, safu ya ushambuliaji pekee ndiyo yenye upungufu inayohitaji maboresho pekee, ambayo anaamini hadi kufikia mechi hiyo atakuwa ameiboresha.

Aidha, alisema kuwa, safu ya ulinzi haina matatizo ambayo katika mechi nne za kirafiki alizocheza imeruhusu bao moja pekee dhidi ya Shangani huku ya kiungo ikitengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo washambuliaji wake wamekosa.

Aliongeza kuwa, katika ligi kuu ana ‘deby’ mbili ambazo ni dhidi ya Simba na Azam FC mara atakapokutana nazo kwenye mechi mbalimbali.

“Timu yangu sehemu yenye upungufu ni moja pekee ya safu ya ushambuliaji ambayo yenyewe inatengenezewa nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuzitumia vyema.

LUNDENGA NA MISS TANGA WAZICHAPA KAVU KAVU KISA KIKIDAIWA NI MICHEPUKO.

“Nimeanza kuiboresha safu hiyo ya ushambuliaji katika mazoezi ya leo (jana) na kuendelea kesho (leo) na hadi kufikia siku hiyo ya mechi na Azam FC tayari nitakuwa nimeiimarisha vyema katika kufunga mabao.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga inaundwa na Geilson Santos Santana ‘Jaja’, Jerry Tegete, Said Bahanuzi, Husein Javu na Hamis Kiiza.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

MFALME MSWATI AOA TENA BINTI WA 14 KATIKA SHEREHE ZILIZOWASHINDANISHA WAREMBO ELFU 80 WENYE BIKRA.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top