SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya Kikwete kufikia Maazimio na Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kulisitisha bunge Maalum la katiba na kupisha Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya katiba iliyopo ya Mwaka 1977,
Nao Umoja huo wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4,kwani kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za Wananchi,
Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la kujadili maazimio kati ya viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),na Rais Jakaya kikwete uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.
Ambapo naye katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo kuendelea hadi Oktoba 4 mwaka huu, kwani huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na yeye Rais Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya,
“Mimi namshangaa jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania zipotee bure kiasi hichi pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga hesabu za Wajumbe wote waliokuwa Bungeni kwenye Vikao vya Bunge garama yake ya posho ni zaidi ya Bilioni 3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi katiba haitopatikana sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana ukweli huko wazi kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge hilo ili fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija”alisema Dokta Slaa,
Dokta Slaa alizidi kusema anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma za watanzania kwani anakubalina na watu mia sita kutoka kwenye bunge hilo laa Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania Zaidi ya Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.
“Huyo ni Rais gani huyo ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma watazania wanaoteseka tena hata kula mlo moja kwa siku ni kazi,yeye anakubaliana na wajumbe mia sita kuteketeza pesa za Wananchi,hivi kweli ndio kiongozi huyu,kwasababu kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha za Chache kwa ajili ya manufaa kwa wananchi wake”alizidi kusema Dokta Slaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi waliyofikia ya kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la katiba litakapohalishwa basi wakubaliane kamaandishi ili Rais ajaye basi aendelee na mchakato huu asiupuuze,
“Sisi ukawa tunakubalina na kwa moyo wate maanuzi tulitofikia katika mkutano na Rais Kikwete,na tunasema wazi tumekubaliana kuhairisha mchakato huu basi tunataka tukubaliane kimaandishi kabisa ili Rais ajaye baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa kusikia eti Rais anayekuja aamue kwa maamuzi yake hatutati kusikia ujinga huo”alisema Mbatia
Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge hilo Maalum la katiba aliongeza kusema wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba endapo Bunge hilo la katiba litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu hawatakubali kuongozwa na mwenyekiti wa sasa ambaye anaongoza Samwel Sitta na kuzidi kusema Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge hilo kutokana na kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.
Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.
“Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa Serika alifanyie ukaguzi wa kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao vyake hivyo kutawaliwa na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe mmoja kwa siku ametengewa bajeti ya chai ya shilingi Eflu kumi kwa siku tena chai ya asubuhi na jioni na hata vipaza sauti pia, vyote hivi ni matokeo ya Ufisadi ndio maana tunamtaka alifanyie ukaguzi wa kimahesabu”alisema profesa Lipumba.
Kuhusu kama Endapo Rais Jakaya asipofanyia merekebisho katiba iliyopo?
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema endepo kama Rais Kikwete asipofanyia marekebisho katiba iliyopo basi atakuwa amefanya usaliti kubwa na ajue ataliweka taifa kwenye machafuko makubwa sana kwani Umoja huo hautokubaliana na yeye.
Katika Hatua nyingene Umoja huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho ya haraka Daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania ambao hawajapata Fursa hiyo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment