Saturday, August 9, 2014

Umeipata Hii ya Helikopta ya Dr. Slaa na Mnyika kunusurika kulipuliwa Shinyanga.

Naibu Waziri wa Nishati ametajwa kwenye njama za kutaka kumuua Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa pamoja mbunge wa Ubungo John Mnyika kwa kuilipua Helikopta wanayosafiria.

Magazeti ya Tanzania August 9 2014 kama Tanzania Daima na Nipashe yameripoti kwamba Naibu Waziri huyo anadaiwa kupanga njama za kuilipua Helikopta ya Dr. Slaa na Mnyika wakiwa ziarani mkoani Shinyanga kukusanya maoni ya Wananchi juu ya muundo wa serikali mkoani Shinyanga.

Tuhuma hizo zilitolewa na diwani wa kata ya Ngokelo Sebastian Peter kutoka Shinganga ambae anasema yeye na mwenzake Zakaria Mfukwa waliahidiwa shilingi milioni 180 kila mmoja kwa ajili ya kuikamilisha hiyo kazi na walipewa kazi hiyo ya kutoa taarifa zote kuhusu kutua kwa Helikopta hiyo na kazi ya ulipuaji ingesimamiwa na Waziri mwenyewe ambayo hata hivyo haikufanikiwa.
CHANZO: http://millardayo.com/


Bonyeza Like HAPO JUU USHINDE ZAWADI YA BAHATI NASIBU WAWEZA SHINDA HADI MILLION MOJA.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top