Sunday, August 10, 2014

ETI MAPENZI SIO PESA ILA MOYO DUU! Ona Serengeti Boy huyu Toka Kenya alivyomuoa huyu Mother wa kihindi.

  Kumekuwa na msisimko mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Kenya kuhusu taarifa ya msichana wa Kihindi aliyekiuka mila na tamaduni za jamii yake na kuolewa na kijana Mwafrika.

Msichana huyu wa kihindi anaitwa Sarika Patel, na ameolewa na kijana wa kabila la Bukusu Timothy Khamala, jambo ambalo ni nadra sana kwa watu wa jamii ya kihindi. Kilichowashangaza wengi ni kwamba Sarika ametoka katika familia tajiri na kuamua kuishi maisha ya walalahoi kijijini


Kwa Sarika maisha ya umaskini ambayo Timothy anaishi sio kikwazo hata kidogo bali kwake hapo ndipo anapata raha na mapenzi ambayo anasema yamemridhisha na kumtuliza nyumbani kwa kijana Timothy.

Timothy alikuwa anafanya kazi nyumbani kwa kina Sarika kama mjakazi lakini akafutwa kazi na baba ya Sarika baada ya kupendana na msichana wake.Kwa sasa yeye ni tarishi katika ofisi hii ya jimbo.Sarika hana kazi

Wawili hao sasa wapo katika pilka pilka za kuanza maisha mapya ila kwa pingamizi kali . Sarika Patel anasema kulingana na mila yao si sawa kuolewa na mtu asiyekubaliwa au kuchaguliwa na wawazi wako. Wachumba kwa kawaida hutoka jamii sawa.

PICHA ZA BINTI MREMBO AMBAYE NI MTOTO WA RAIS KAGAME HIZI HAPA;

Mbali na tofauti ya rangi zao za ngozi , Sarika anatoka katika familia tajiri kinyume na mumewe Timothy ambaye ni mlalahoi. Licha ya tofauti hiyo, Sarika anasema wazazi wake hawangeweza kumzuia kumpenda amtakaye

Bonyeza Like HAPO JUU USHINDE ZAWADI YA BAHATI NASIBU WAWEZA SHINDA HADI MILLION MOJA. 

 

TOA MAONI YAKO KUHUSU NDOA HII HAPO CHINI INASTAILI AU WAZEE WAIVUNJE???

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top