Wednesday, August 6, 2014

TFF yataka vyeti vya Zdravko Logarusic wa Simba na Marcio Maximo wa Yanga haraka sana.

 
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezitaka CV za makocha wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic na Mbrazili wa Yanga, Marcio Maximo pamoja na wa timu zote za ligi kuu na daraja la kwanza ili kutathmini viwango vyao.

PASTOR MYAMBA Afunga Harusi ya Kufuru! KAMATI PEKE YAKE ILIMZAWADIA Million 250;Dada Mtu Nae Million 100.Wapambe ....

Hatua hiyo ya TFF imekuja kufuatia kuwepo kwa wimbi la makocha na madaktari katika timu mbalimbali wasiokuwa na vigezo.Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, amesema wanazikumbusha klabu zote za ligi kuu na daraja la kwanza  kuwasilisha vyeti vya makocha wao pamoja na madaktari kabla ya ligi kuanza ili waweze kuvikagua.

“Tunahitaji kujua uwezo wa madaktari na mameneja. Vyeti viwasilishwe kabla ya ligi kuanza mwezi ujao,” alisema Wambura.
 
Maximo ni mmoja kati ya makocha wanaoheshimika hapa nchini na amekuwa akijizolewa sifa kemkem tangu alipokuwa kocha wa Taifa Stars miaka minne iliyopita. kwa upande wa Loga ambaye alijiunga na Simba msimu uliopita bado anaaminika kuwa ni kocha bora kutokana na staili yake ya kufundisha.
Inaaminika kuwa makocha wote hao wana vyeti vyao kamili vya kufanya kazi na utekelezaji wa kuvipeleka unaweza kufanyika mara moja.Hii siyo mara ya kwanza kwa tff kuomba vyeti vya makocha na madaktari hapa nchini.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya. 

ISOME NA HII USIJIFANYE HUJAIONA

Aunt Ezekiel Afumaniwa na Dansa wa Diamond Ambaye ni Mme wa Mtu waki Du Nyumbani Kwa Wema Sepetu.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top