Tuesday, August 12, 2014

PADRI WA HISPANIA AFARIKI DUNIA KWA EBOLA.

Padri Miguel enzi za uhai wake.

PADRI raia wa Hispania, Miguel Pajares, 75, aliyeambukizwa virusi vya Ebola wakati akifanya kazi Afrika Magharibi amefariki dunia akiwa hospitalini mjini Madrid.

Padri Miguel alikuwa anafanya kazi katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph iliyopo mjini Monrovia, Liberia.

Alisafirishwa kwenda Hispania kutoka Liberia wiki iliyopita akiwa na mtawa mmoja ambaye naye aliponea chupuchupu kuambukizwa homa hiyo.

Zaidi ya watu 1,000 wamefariki kutokana na homa ya Ebola nchini Liberia, Guinea, Sierra Leone na Nigeria tangu kulipuka kwa homa hiyo mwezi Februari.


Bonyeza Like HAPO JUU USHINDE ZAWADI YA BAHATI NASIBU WAWEZA SHINDA HADI MILLION MOJA.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top