Bango likionyesha picha na majina ya wasanii wa filamu na maigizo waliotangulia mbele ya haki lililowekwa katika viwanja vya Karimjee wakati wa Hitima hiyo iliyofanyika miki iliyopita.
Sehemu ya wasanii na watu wengine waliohudhuria shughuli hiyo.
Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie Unity, Steve Mengere akitoa neno la shukurani wa watu waliojitokeza kwenye hitima hiyo.
Watoto wa kiume walioshiriki kuimba Kaswida
Watoto wa kike walioshiriki kuimba Kaswida
Wasanii mastaa wa filamu Bongo juzi kati walisusia hitima iliyoitishwa kwa ajili ya kisomo cha wenzao waliotangulia mbele ya haki na kufanya Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, kuwapiga dongo kuwa kama ingekuwa shughuli ya pombe na uvaaji wa nusu utupu, wangekuwa wengi.
Dudu Baya: Sijabahatika kumpata mwanamke ninayemtaka, nakutana na machizi tu.
“Nimetumia muda mwingi sana kuwataarifu watu kuwa leo kuna hitima ya kuwaombea wenzetu waliotangulia mbele za haki, lakini ushirikiano wao umekuwa mdogo ila ingekuwa sherehe ambayo ina bia, yaani vitu vya anasa watu wangekuja wengi hadi viti visingetosha,” alisema Steve Nyerere.
Naye mgeni rasmi, Bulembo aliwaasa wasanii wa Bongo Muvi waliohudhuria hitima hiyo kutowatenga ambao hawakuhudhuria, badala yake washirikiane nao na kudumisha upendo na umoja ili kuondoa matabaka.
Baadhi ya mastaa waliohudhuria hitima hiyo Johari, Wastara, Odama, Nisha, Eshe Buheti, JB, Richie, Baba Haji, Cloud, Masanja Mkandamizaji, Mzee Chilo na Mhogo Mchungu.
Imeandaliwa na: Chande Abdallah, Mayasa Mariwata, Rhoda Josiah, Gladness Malya na Shakoor Jongo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment