Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
LICHA YA DIMPOZI KUTAJWA VANESSA NA JUX YADAIWA NI WAPENZI.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Agostii 25, mwaka huu katika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ikiwa katika pitapita zake ilinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi madaktari hao.OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
Vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa na madakta hao katika zoezi la utoaji wa mimba.
Daktari Shengena alipoona kamera ya OFM alitaka kukimbia licha ya kuwepo kwa askari ndani ambapo walitumia nguvu za ziada kuwadhibiti vyema na kuingizwa ndani ya chumba alichokuwemo mwenzake ambaye naye alinaswa akiwa na vifaa vilivyodaiwa ni vya kuchomolea mimba akiwa amevificha kwenye mfuko wa rambo.
Madaktari wakiwa chini ya ulinzi wa makamanda wa OFM.
Baada ya maafande kuwaweka chini ya ulinzi, madaktari hao walizua kituko kufuatia kuzitupa chini shilingi 40,000 walizopewa na denti huyo kama malipo ya kazi hiyo wakidhani ni za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘Takukuru’.

Binti (denti) aliyekusudiwa kutolewa mimba.
Akijibu kuhusu kwa nini alivificha vifaa va kutolea mimba kwenye mfuko, Dokta Chacha alijiumauma na kusema denti huyo alifuata taratibu zote kama wagonjwa wengine, lakini alishindwa kuonesha risiti au cheti cha kumsajili mgonjwa huyo kwa ajili ya matibabu.
Kichekesho kingine kilikuwa wakati OFM na wanausalama wakitoka nje ya zahanati hiyo na watuhumiwa na kukuta kwenye maeneo mengine kukiwa kweupe na kusemekana kuwa, madaktari na manesi walioshuhudia wenzao wakitaitiwa walitoka nduki kwa kuogopa ushahidi.
Mwishowe watuhumiwa hao walifikishwa katika Kituo cha Kidogo cha Polisi Buza na kufunguliwa jalada lenye Kumbukumbu Na. BUZ/RB/32/2014 kabla ya baadaye kufikishwa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Dar kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusiana na sakata hilo.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment