Monday, August 4, 2014

JEURI NYINGINE YA FEDHA YA DIDA WA Radio Times FM HII HAPA!

Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, Hadija Shaibu ‘Dida’ akipozi kwenye gari yake mpya.
Zimemtembelea! Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ ameonesha jeuri nyingine ya fedha baada ya kununua magari mengine mawili kwa mpigo.

Hadija Shaibu ‘Dida’ akiikagua gari yake.

Dida amefanya kufuru hiyo ikiwa imepita miezi kadhaa tangu atangaze kuwa ana nyumba mbili maeneo ya Goba na Kigamboni pamoja na kuyaanika magari manne anayomiliki (Toyota Verossa mbili, Toyota Noah nyeusi na Toyota Vitz.)

MUONEKANO MPYA WA VERA SIDIKA KUTOKA KENYA HUU HAPA.


Akizungumza na Ijumaa Wikienda, rafiki wa karibu wa Dida aliyeomba hifadhi ya jina alisema ameshtushwa na kitendo cha shosti wake huyo kununua magari mawili kwa mpigo kiasi cha kumfanya ahisi kuna biashara nyingine anaifanya tofauti na utangazaji.

“Kanunua magari mawili, Toyota Noah na Toyota Brevis New Model. Yaani hata sisi mashosti zake anatufanya tuhisi labda anafanya ile biashara ya unga kama watu wanavyohisi.

“Ni kweli anafanya biashara zake lakini ndiyo apate fedha za kuonesha jeuri hiyo? Ila kama ni kupambana na maisha, sasa hivi anapambana kikwelikweli, hata akijiita Boss Lady ni sahihi kabisa,” alisema mtoa habari huyo.

Gari jingine la ‘Dida’ aina ya Toyota Noah.

Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Dida ili kujua ukweli wa magari hayo, alipopatikana alifunguka:

PICHA ZA BINTI ALIYELIWA KA.....BANG BAADA YA KUKOLEZESHWA POMBE.

“Siwezi kujiita Boss Lady kimdomomdomo tu, huwa napenda kufanya kitu watu ndiyo waseme, nimeongeza magari mengine mawili. Moja ni Noah kwa ajili ya biashara zangu na lingine ni Toyota Brevis la kutembelea,” alisema Dida aliyetengana na mumewe, Ezden Jumanne siku chache zilizopita. 

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top