Thursday, August 21, 2014

FLAVIANA MATATA AZUA UTATA WA UCHUMBA AKISEMA ALIYECHUMBIWA SI YEYE.



MISS Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata amezua utata wa aina yake baada ya picha zinazomuonesha katika tukio la kuchumbiwa kunaswa na mwenyewe kudai si yeye aliyechumbiwa.

Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata.

Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo limedaiwa kufanyika kwa siri hivi karibuni nyumbani kwa miss huyo, Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu wa karibu.

“Inaonesha hawakutaka watu wajue maana hata hakukuwa na watu wengi siku hiyo, hata hao ndugu wenyewe hawakuwa wengi kiivyo lakini picha zinaonesha Flaviana akichumbiwa,” kilisema chanzo hicho.

Kikizidi kumwaga data chanzo hicho kilidai kwamba, mwanaume anayetaka kumuoa mrembo huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja ni Mchaga mwenye fedha zake aishiye Marekani.
“Nasikia huyo bwana wake ni Mchaga lakini anaishi Marekani, atakuwa ana fedha zake si mtu wa hivihivi,” kilisema chanzo.

Amani lilifanikiwa kuzinasa picha hizo ambazo zinamuonesha mrembo huyo akiwa amepiga magoti huku amemshika mkono mmoja wa wazazi wake aliyeshiriki katika hafla hiyo ya kupokea mahari.

KATANGAZE: LIVE! MSANII WA BONGO FLEVA ANASWA AKINUNUA MACHANGU Sinza Africasana Dar.

Baada ya kupata madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Flaviana kwa njia ya simu ya mkononi ndipo alipokataa katakata kuwa si yeye aliyekuwa akichumbiwa bali ni dada yake.

“Hamna kitu kama hicho,  unayesema alikuwa anachumbiwa si mimi ni dada yangu, mila za kwetu Shinyanga nalazimika mimi kumsindikiza hivyo kama umeona picha hizo uelewe hivyo,” alisema Flaviana.

Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa ni la Flaviana na si dada yake hivyo kuzidi kuzua utata juu ya ukweli halisi, Amani linaendelea kufatilia kwa karibu.

American journalist James Foley beheaded by 'British' jihadist in horrific Islamic State video.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

AJALI MBAYA KABISA YA MABASI KUGONGANA USO KWA USO YAUA TAKRIBANI 16 NA KUJERUHI 75 TABORA.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top