Monday, August 11, 2014

AUNT EZEKIEL: LAZIMA NIHAKIKISHE NAMPA PENZI MUME WA MTU ILI KUMKOMESHA MKEO.


Makubwa! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amefungukia madai ya kutoka na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moze Iyobo ambaye ni mume wa mtu akisema hakuna ukweli wowote zaidi ya kutaka kuchafuliwa.

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Aunt ambaye gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko liliripoti tukio la kutaka kufanyiziwa na mke wa dansa huyo aitwaye Mwengi Ally, alisema anamshangaa mwanamke huyo lakini ili kumkomoa atahakikisha anafanya kweli ili kama ni kunuka, kinuke kihalali.
Alisema kwamba yeye ni mke wa mtu asiyeweza kujirahisi kwa kutembea na kijana huyo na kwamba kama ni kujuana ni kwa sababu ya Diamond ambaye ni shemeji yake kwa Wema.

PICHA ZA BINTI MREMBO AMBAYE NI MTOTO WA RAIS KAGAME HIZI HAPA;



>“Amenichafulia sana, siwezi kutembea na Moze, najiheshimu. Lakini kwa kuwa ameamua kunipakazia, nitahakikisha namtega mumewe na nikimnasa nampa penzi ili kama ni hizo vurugu azifanye kihalali,” alisema Aunt na kusisitiza:

Dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moze Iyobo (kulia).

“Siwezi kuwa na uhusiano na Moze, yule mwanamke alikuwa na nia ya kuifanya jamii inifikirie vibaya lakini amenoa.” Hivi karibuni kundi la watu likiongozwa na  Mwengi lilifika nyumbani kwa Wema Sepetu likimsaka Aunt ili kumshikisha adabu kutokana na madai ya kutoka na mume wa mtu huyo.


Bonyeza Like HAPO JUU USHINDE ZAWADI YA BAHATI NASIBU WAWEZA SHINDA HADI MILLION MOJA. 

 

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top