Tuesday, July 15, 2014

Wazazi wa wasichana 200 waliotekwa nyara na Boko Haram nchini Nigeria wamekataa kukutana na rais Goodluck Jonathan.


Wazazi wa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wamekataa wito wa kukutana na rais wa taifa hilo Goodluck Jonathan.

Hakuna sababu zozote zilizotolewa na wazazi hao.

Mkutano huo uliotarajiwa kuwa wa kwanza kwa rais Goodluck Jonathan na wazazi hao pamoja na baadhi ya wasichana waliotoroka mikono ya boko haram, tangu Boko Haram kuwateka nyara wasichana zaidi ya mia mbili miezi mitatu iliyopita.

Baadi wanamkosoa rais Goodluck kwa uamuzi wake wakisema umeshinikizwa na Malala

Mnamo siku ya Jumatatu mwanaharakati mdogo wa elimu Malala Yousafzai kutoka Pakistan alimsihi Rais Jonathan kukutana na wazazi wa wasichana hao.

Awali shirika la kimataifa la Human Rights Watch lilisema kuwa zaidi ya raia 2,000 wameuawa nchini Nigeria mwaka huu na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Vifo hivyo vinaripotiwa kutokea katika mashambulizi yaliyofanywa katika zaidi ya miji sabini na vijiji Kaskazini mwa Nigeria.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top