Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza.
Timu ya Tanzania Movie Talents (TMT) ikiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya Show ya Tanzania Movie Talents katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliohudhuria kwaajili ya kutazama onyesho la washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Wadau waliojitokeza kwaajili ya Kushuhudia onyesho la Tanzania Movie Talents.
Washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washindi kutoka kanda 6 za Tanzania wamepanda kwa steji katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwaajili ya kuanza kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza. Sasa ni safari kwa washiriki kuelekea kwenye kinyanganyiro cha kuwania Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane.
Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata Taarifa za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678
Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno "TMT ikifuatiwa na namba ya Mshiriki" kwenda namba 15678.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment