Monday, July 21, 2014

Kijana acharazzwa Fimbo mchana Kweupe baada ya kufumwa akila Mgahawani huko Pemba.

Mtu mmoja kisiwani Pemba ambae hadi sasa bado jina lake halijafahamika amejeruhiwa vibaya baada ya kupata kipigo kutoka kwa askari jamii.

 Mkasa huo umetokea katika kijiji cha Msingini Chake chake mkoa wa kusini pemba ambapo Polisi jamii wa Shehia hio waliamua kumpiga mtu huyo baada ya kuoneka akila mchana akiwa pamoja na wenzake watatu ambao wamefanikiwa kukimbia na kutokomea kusiko julikana. Mtoa taarifa wetu akizungumza na mazui media amesema watu hao walikua ndani ya nyumba wakipika sembe na kujidunga madawa ya kulevya mchana wa leo katika shehia ya hio ya Msingini.

 ‘’Unajua tunawashukuru sana hawa Polisi jamii wetu wanajitahidi mno hususani kipindi hichi cha Ramadhani hatuwezi kukubali kuona watu wanakula ovyo katika kisiwa chetu’’alieleza mtoa taarifa hii ambae hakupenda jina lake litajwe. Aidha Polisi jamii hao kwa sasa wananmfikisha mtu huyo katika kituo cha polisi Chake chake ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria zaidi.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya. 

Kwa Staili hii hawa Makahaba watakomeshwa hapa Mjini.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top