Wednesday, July 2, 2014

KAIMU BALOZI WA LIBYA NCHINI TANZANIA AMEJIUA.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Lbya.
Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini.
Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho. Maiti imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.
    IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
    Dar es Salaam,
    Julai 2, 2014

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top